Wewe kwa mtazamo wako unalionaje,inakuaje utakapojkuta unawasiliana na mtu PM ukidhani wa kike kumbe wa kiume,utafikiria nini kuhusu huyo mwanaume?
Well, ndo maana huwa sivamiagi watu au vitu hovyo hovyo. Niko mwangalifu sana maishani. Nimeshasema mara nyingi sana kuwa JF ni msitu, tena ulio mnene.
Kwa sababu hiyo, kwanza , sina sana mazoea ya kuwasiliana na watu humu kwa njia ya PM. Pili, hata nikifanya hivyo nakuwa niko mwangalifu sana kuhusu mambo ninayowasiliana.
Amini usiamini watu huwa wananitumia PM kuniomba mambo mbalimbali yakiwemo kuwafundisha Kiingereza, kuwanunulia vi-gadgets ili kama narudi Tanzania niwaletee, kuwafanyia proof readings za kazi au assignments zao za shuleni au kazini, na mengineyo mengi tu.Kawaida yangu huwa nazipotezea tu PMs kama hizo.
Tatu, huwa nina machale sana. Unapowasiliana na mtu kuna mambo ambayo mtu unaweza kuyang'amua endapo utakuwa mhalisia. Kuna mambo huwa haya-make sense hata kidogo. Sasa uwezo kama huu haufundishiki. Ni wa kuzaliwa nao pamoja na tajiriba yako ya kimaisha.
Nikiona mtu haeleweki eleweki napotezea au namchukulia hivyo hivyo tu. Hakutakuwa na seriousness yoyote ile. Sasa itokee kuwa huyo ninayewasiliana naye kuwa ni wa kiume ilhali anajiwasilisha ki-kike, nitampotezea tu kwa kunipotezea muda wangu.
Maana sababu za yeye kujifanya hivyo anazijua mwenyewe na kwa kweli haitanistahili mimi kupoteza muda wangu kuanza kuwaza na kuwazua kulikoni huyo mtu yuko hivyo. To each his own.
After all, JF ni msitu hivyo kutegemea visivyotegemewa ni hali ya kawaida. Dawa ni kuwa mhalisia tu, basi.