Kikao cha Kamati Kuu ya CCM chaahirishwa

TandaleOne

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2010
Posts
1,644
Reaction score
709
Kikao cha Kamati Kuu ya halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi kilichokuwa kikutane leo saa tano asubuhi, kimeahirishwa kutokana na kikao cha Maadili chini ya Mwenyekiti wake Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete kilichokaa mapema asubuhi kuchukua muda mrefu kuliko ilivyotegemewa kwenye ratiba.

Hivyo Kikao cha Kamati Kuu kinatarajia kufanyika majira ya saa kumi jioni ya leo, na kwamba wajumbe ambao walishafika eneo la ukumbi wa mikutano wa ofisi za Makao Makuu ya CCM maarufu kama whitehouse wametakiwa kuondoka na kurejea tena baadae saa kumi alasiri.

Kwa taarifa sahihi za mijadala na maazimio ya kikao hicho cha Kamati Kuu, fuatilia akaunti rasmi ya twitter ya Chama Cha Mapinduzi kwa anuani hii;
attachment.php

CFm6dWqUkAA4OJ1.jpg

CFm5rc4UgAEh6uN.jpg

CFm6vQTWIAAMgat.jpg

wajumbe wa Kamati Kuu wakijiandaa na Kikao kinachotegemea kuanza muda mfupi ujao.

CFnWcG4W8AAPc4s.jpg
 
Attachments

  • nec.png
    nec.png
    36.8 KB · Views: 6,749
Wana hofu gani hao magamba au yule mbunge wa monduli anawachanganya huu mwaka wa ccm kuanguka wameenda kujimaliza huko dodoma
 
Kiapo namba nne cha mwanachama wa CCM: "Rushwa ni adui wa haki, sitapokea wala sitatoa rushwa". Rais akitoka CCM, ndiye pia anayekuwa Mwenyekiti wa CCM. Sasa basi Mtoa rushwa NA.1 Lowassa, anawezaje kuwa Rais na pia Mwenyekiti wa CCM, bila kufuta kwanza kiapo hicho???? Lowassa tupa kuleeeeeeeee!!!!!!!
 
"Rushwa ni adui wa haki, sitapokea wala sitatoa rushwa". Hayo ni maneno tu hata kwenye kanga yapo. Haya maneno yalikuwa halali wakati wa awamu ya JULIUS K. NYERERE tu.
 
Maccm yanatukanana yenyewe.... Mlishindwa kumvua gamba mtaweza kumzuia asigombee?

Ni kitu gani ccm ilishawahi kuweza au hata kujaribu kukifanya juu ya wanachama wake mafisadi.
 
Mwenzenu mwingine huyo.......

Ni jambo lililo wazi kuwa kuna kundi la viongozi wanaoondoka madarakani wanamuhofu Lowassa.Hofu yao huenda inatokana sana na jinsi walivyomtenda siku za nyuma.Wanaogopa kulipiziwa yale waliyomtendea !

Lowassa si mtu wa visasi,najua hawezi kuwadhulu kama wanavyodhani.Ukweli ni kwamba Lowassa anataka kuijenga nchi,anataka kuendeleza cheche zake za maendeleo alizozionesha 2005-2008 kabla hajaundiwa zengwe na kutoswa.

CCM ninawasihi sana,ninawaombeni sana kuwa msimuache Lowassa, ni kete muhimu ya kukibakisha chama madarakani na kuijenga nchi.

Kila palipo na watu 10, 8 kati yao wanamjua Lowassa kuliko mtu mwingine yeyote yule, huyu ni muhimu,haifai kumuacha hata kidogo.

Sijapata kuwasikia UKAWA wakifoka dhidi ya Lowassa,sijawasikia. Ninaamini na ni kweli kuwa hata UKAWA wanamkubali Lowassa.UKAWA wameamua kusubirisha taratibu zao za kumteua rais ili kutaka kujua kwanza ccm itafanya nini kwa Lowassa,na ikiwa ccm watafanya dhambi ya kumtosa Lowassa,UKAWA watambeba na atapita bila kupingwa KAMA ILIVYOKUA KWA mWAIKIBAKI KULE kENYA ALIPOTOSWA NDANI YA KANU!

Lowassa anakubalika sana na watanzania wengi kwa sasa.CCM msimuache Lowassa,huyu akiteuliwa atapita bila kupingwa!

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
 
tatizo ni fisadi, afu afya mgogoro.. hii imewatia shaka hao wachaguaji wakihofu yaliyotokea ZAMBIA
 
Back
Top Bottom