Kikao cha Kamati Kuu CHADEMA, Anthony Komu, Kubenea na yatarajiwayo

Wanasiasa ni watu ma-boya sana...

Yani hata hao unaowatetea leo hujui kesho watakua upande gani(kumbuka kipindi kile ulivyokuwa ukimchafua EDWARD LOWASSA,vp leo hali ikoje?)
 
Kuelekea Kamati Kuu, Kubenea Saed na Anthony Calist Komu wasipate nafasi ya huruma, bali Chama na umma ndio upate nafasi ya huruma kwakufutwa machozi yao ya kukitumikia chama hiki kwa jasho na damu, na kufutwa kwao kuwe ni kwakufukuza wasaliti wote ndani ya Chama.

Naandika haya usiku huu nikijaribu kuwarejesha nyuma kidogo, juu ya usaliti wa watu hawa wawili, na namna chama kilivyojaribu kuwasamehe mara kadhaa lakini imeonekana wao wanautafuta sana mlango wa kutokea.

Kwanza visa na vitimbi vya wabunge hawa vilianza baada ya uchaguzi, na Chama kilipofanya mabadiliko ya kurugenzi zake kama sehemu ya utaratibu wa kawaida wa baada ya miaka mitano hubadili safu za kiongozi za chama makao makuu nk.

Baada ya mabadiliko hayo, Komu aliyekuwa ni mkurugenzi wa fedha wa chama hiki aliondolewa katika nafasi hiyo na ikachukuliwa na mwanachama mwingine, Pia mke wa Kubenea (hawara), aliyekuwa mtumishi makao makuu aliondolewa na nafasi yake ikashikwa na mwanachama mwingine.

Sera ya muundo mpya wa mabadiliko kwamba wabunge wasiwe wakurugenzi wa idara makao makuu, iliasisi wa na Katibu Mpya Mh Dr. Mashinji na ikaungwa mkono kwa nguvu zote na Kamati Kuu ya Chama. Wabunge wengi waliokuwa wananafasi za kiuongozi wa walipoteza nafasi zao isipokuwa naibu katibu mkuu Bara na Mwenyekiti.

Hatua hii iliwaudhi sana Komu na Kubenea na kwakuwa ni wabia kibiashara, walipokutana kujadili kilichojiri kupoteza nafasi pale makao makuu, Wakajiridhisha kuwa mbaya wao ni Mwenyekiti wa Chama, hivyo wakaanzisha vita ya chini kwa chini iliyoenda sambamba na kibri na kumvunjia heshima kupitia mitandao ya kijamii (wanakikundi cha vijana wasaliti) na magazeti yake ya mwanahakisi nk.

Naomna nitoe sehemu ndogo tu ya matukio, nitawakumbusha, naamini na Kamati kuu kesho itawasomea haya na mengine mengi.

1. Miezi sita tangu apotee Ben Saanane huku Chama na Watanzania nchi nzima wakiwa kwenye hekaheka ya kumtafuta Ben, na huku wakishinikiza serikali iharakishe kumtafuta Mtanzania mwenzetu, Saed Kubenea akishirikiana na Antony Komu aliyejitambulisha katika taarifa ya gazeti kama mjumbe wa Kamati kuu, waliandika kuwa Ben hajatekwa, yuko vijiweni kajificha tu, Mbowe anajua alipo.

Taarifa hii kwa shemu kubwa ilikichafua chama, ilififisha juhudi za Watanzania kuishinikiza serikali, na kwa namna yoyote ile taarifa hii ilipunguza spidi ya Jeshi la Polisi katika kuendelea na uchunguzi. Kwa taarifa hii tu Kubenea na Komu walistahili kufukuzwa katika chama na kuwakabidhi kwa mamlaka za nchi wasaidie kuonyesha Ben Saanane alipo.

2. Baada ya Lissu kupigwa risasi na kukimbizwa Nairobi, huku Chama na umma ukiendelea na harambee ya kuchangia matibabu ya Lissu, Saed Kubenea na Antony Komu kwakushirikiana na watesi wetu, walianzisha kampeni ya kumchochea Lissu na kutengeneza mgogoro kati ya chama na Lissu,mpaka Lissu alipowashushua wakaingia mitini kabisa. Hili tu lilitosha Antony Komu ma Kubenea kufukuzwa katika Chama hiki.

3. Antony Komu na Saed Kubenea wakijua wazi ni kosa kwamjibu wa Katiba ya Chama, Wameanzisha ziara za kuzunguka mikoani kutengeneza Mtandao wa kuasi chama huku wakisambaza habari za kuchafua uongozi uliopo madarakani kikatiba. Hatua hii ni kosa linalostahili kufukuzwa uanachama.

4. Huku wakijua ni mwiko kikanununi na kimaadili ya chama, Kubenea na Komu walipoitwa mbele ya mamlaka za kinidhamu za chama na kuonywa, katika hali ya kustaajabisha na kuonyesha wanatafuta kufukuzwa kwa nguvu, wakavujisha barua zao za kujieleza walizoandikiwa na chama kama hatua za kinidhamu. Kwa hatua hii tu walishahili kufukuzwa kabisa katika chama.

5. Huku tayari wakiwa wameshaandikiwa barua za maonyo kama nilivyoeleza hapo juu, Kubenea na Komu hawakujali wala kusikia, Wakanaswa na teknolojia ya mzungu, Sauti (Audio) ya Njama za kuwabambikia kesi viongozi wenzao na kupanga kuwapoteza baadhi ya wajumbe (Boniface Jacob), ikiwemo kumtengenezea kesi ya utakatishaji fedha Mwenyetiki wa Chama Mh Freeman Mbowe. (Rejea kusikiliza hiyo audi hapo chini).

Hayo ni machache ninayoamini hayatakuwa na mjadala mrefu zaidi ya kuwasomea mashitaka, kuwasikiliza na kuchukua kadi zao tu.

Chama hiki sio Cha mtu au kikundi, yeyote anayetusaliti watanzania ni lazima tumsailiti kabla hajatusaliti. Fukuzeni wote waende kumtumikia anayewapa jeuri huko ccm.

LETS GO BACK TO OUR ROOTS!

Na Yericko Nyerere

View attachment 900563
Gawaneni fito ili iwe alfa na Omega ya CHADEMA.Maana uzushi na majungu ndio sifa yenu kuu
 
Aliyewaroga watanzania ni yule aliyeifanya siasa iwe kila kitu kwa maisha ya mtanzania. Eti ili jamii iendelee inahitaji vitu vinne
1. Watu
2. Ardhi
3. Siasa safi
4. Uongozi bora
Alisahau kitu cha muhimu kabisa ... Elimu + Muda
 
..CDM mnahitaji kupatana kuliko kufukuzana.

..Majuzi mlitangaza SERA mpya ya chama.

..badala ya kutangaza sera mnatangaza maugomvi yenu.
.
Chadema wana asili ya ugonvi. Vita dhidi tao na chama tawala (pamoja na uongozi wa nchi) imewashinda dhahiri shahiri. kwa vive wanapenda vita wameamua waanzishe vita ya wao kwa wao.
Wacha watafunane
 
Hivi Mbowe na Magufuli nani ana umri mkubwa?
Acha kukulupuka...magufuri hata miaka mitano ya uwenyekiti hajamaliza...haya huyo babu wenu kwenye uenyekiti ana miaka mingapi...assume angepewa urais si angebadili katiba nakua mfalme...
Nilikua namaanisha kashazeeka kifikla kua mwenyekiti....ambaf ww
 
Kuelekea Kamati Kuu, Kubenea Saed na Anthony Calist Komu wasipate nafasi ya huruma, bali Chama na umma ndio upate nafasi ya huruma kwakufutwa machozi yao ya kukitumikia chama hiki kwa jasho na damu, na kufutwa kwao kuwe ni kwakufukuza wasaliti wote ndani ya Chama.

Naandika haya usiku huu nikijaribu kuwarejesha nyuma kidogo, juu ya usaliti wa watu hawa wawili, na namna chama kilivyojaribu kuwasamehe mara kadhaa lakini imeonekana wao wanautafuta sana mlango wa kutokea.

Kwanza visa na vitimbi vya wabunge hawa vilianza baada ya uchaguzi, na Chama kilipofanya mabadiliko ya kurugenzi zake kama sehemu ya utaratibu wa kawaida wa baada ya miaka mitano hubadili safu za kiongozi za chama makao makuu nk.

Baada ya mabadiliko hayo, Komu aliyekuwa ni mkurugenzi wa fedha wa chama hiki aliondolewa katika nafasi hiyo na ikachukuliwa na mwanachama mwingine, Pia mke wa Kubenea (hawara), aliyekuwa mtumishi makao makuu aliondolewa na nafasi yake ikashikwa na mwanachama mwingine.

Sera ya muundo mpya wa mabadiliko kwamba wabunge wasiwe wakurugenzi wa idara makao makuu, iliasisi wa na Katibu Mpya Mh Dr. Mashinji na ikaungwa mkono kwa nguvu zote na Kamati Kuu ya Chama. Wabunge wengi waliokuwa wananafasi za kiuongozi wa walipoteza nafasi zao isipokuwa naibu katibu mkuu Bara na Mwenyekiti.

Hatua hii iliwaudhi sana Komu na Kubenea na kwakuwa ni wabia kibiashara, walipokutana kujadili kilichojiri kupoteza nafasi pale makao makuu, Wakajiridhisha kuwa mbaya wao ni Mwenyekiti wa Chama, hivyo wakaanzisha vita ya chini kwa chini iliyoenda sambamba na kibri na kumvunjia heshima kupitia mitandao ya kijamii (wanakikundi cha vijana wasaliti) na magazeti yake ya mwanahakisi nk.

Naomna nitoe sehemu ndogo tu ya matukio, nitawakumbusha, naamini na Kamati kuu kesho itawasomea haya na mengine mengi.

1. Miezi sita tangu apotee Ben Saanane huku Chama na Watanzania nchi nzima wakiwa kwenye hekaheka ya kumtafuta Ben, na huku wakishinikiza serikali iharakishe kumtafuta Mtanzania mwenzetu, Saed Kubenea akishirikiana na Antony Komu aliyejitambulisha katika taarifa ya gazeti kama mjumbe wa Kamati kuu, waliandika kuwa Ben hajatekwa, yuko vijiweni kajificha tu, Mbowe anajua alipo.

Taarifa hii kwa shemu kubwa ilikichafua chama, ilififisha juhudi za Watanzania kuishinikiza serikali, na kwa namna yoyote ile taarifa hii ilipunguza spidi ya Jeshi la Polisi katika kuendelea na uchunguzi. Kwa taarifa hii tu Kubenea na Komu walistahili kufukuzwa katika chama na kuwakabidhi kwa mamlaka za nchi wasaidie kuonyesha Ben Saanane alipo.

2. Baada ya Lissu kupigwa risasi na kukimbizwa Nairobi, huku Chama na umma ukiendelea na harambee ya kuchangia matibabu ya Lissu, Saed Kubenea na Antony Komu kwakushirikiana na watesi wetu, walianzisha kampeni ya kumchochea Lissu na kutengeneza mgogoro kati ya chama na Lissu,mpaka Lissu alipowashushua wakaingia mitini kabisa. Hili tu lilitosha Antony Komu ma Kubenea kufukuzwa katika Chama hiki.

3. Antony Komu na Saed Kubenea wakijua wazi ni kosa kwamjibu wa Katiba ya Chama, Wameanzisha ziara za kuzunguka mikoani kutengeneza Mtandao wa kuasi chama huku wakisambaza habari za kuchafua uongozi uliopo madarakani kikatiba. Hatua hii ni kosa linalostahili kufukuzwa uanachama.

4. Huku wakijua ni mwiko kikanununi na kimaadili ya chama, Kubenea na Komu walipoitwa mbele ya mamlaka za kinidhamu za chama na kuonywa, katika hali ya kustaajabisha na kuonyesha wanatafuta kufukuzwa kwa nguvu, wakavujisha barua zao za kujieleza walizoandikiwa na chama kama hatua za kinidhamu. Kwa hatua hii tu walishahili kufukuzwa kabisa katika chama.

5. Huku tayari wakiwa wameshaandikiwa barua za maonyo kama nilivyoeleza hapo juu, Kubenea na Komu hawakujali wala kusikia, Wakanaswa na teknolojia ya mzungu, Sauti (Audio) ya Njama za kuwabambikia kesi viongozi wenzao na kupanga kuwapoteza baadhi ya wajumbe (Boniface Jacob), ikiwemo kumtengenezea kesi ya utakatishaji fedha Mwenyetiki wa Chama Mh Freeman Mbowe. (Rejea kusikiliza hiyo audi hapo chini).

Hayo ni machache ninayoamini hayatakuwa na mjadala mrefu zaidi ya kuwasomea mashitaka, kuwasikiliza na kuchukua kadi zao tu.

Chama hiki sio Cha mtu au kikundi, yeyote anayetusaliti watanzania ni lazima tumsailiti kabla hajatusaliti. Fukuzeni wote waende kumtumikia anayewapa jeuri huko ccm.

LETS GO BACK TO OUR ROOTS!

Na Yericko Nyerere

View attachment 900563
Wafukuzeni ili muendelee kuifurahisha CCM kwa manufaa na ustawi wa CCM. Viginevyo uongozi wowote wa upinzani wenye hekima hata kidogo tu hauwezi kufukuza mwanachama katika kipindi hiki kigumu kwao. Yatakuwa maamuzi yenye kushinikizwa na CCM na naaza kuamini Chadema itakuwa imeanza kukubali kusambaratishwa kwa propaganda ndogo sana. kwa hili tusiilaum CCM walaumiwe viongozi kwa kukubali kutegeka na kunaswa kirahisi sana.
 
Kama kweli Kubenea anataka kwenda ccm bas ni hatar Sana,watu wamemtia umakengeza hafu anawafuata tena huko ama kweli mungu akunyime pesa lkn sio akili! Hakuna hatuta fika kokote,kama watu hujijali wao na sio wenzao
 
Kuwa na akili,aliyemtia makengeza yuko chadema saiz. Ni maajabu Kubenea kuendelea kuishi na mtu aliyemtia makengeza
 
Chadema ni noma
FB_IMG_1539778480328.jpeg
 
MAAMUZI YA KAMATI KUU KUHUSU KOMU NA KUBENEA.

Na Yericko Nyerere,

Jumamosi ya tarehe 13 Oktoba 2018, ilisambaa ‘audio clip’ iliyodaiwa kuwa ni ya wabunge wawili wa Chadema, Anthony Komu (Moshi Vijijini) na Saeed Kubenea (Ubungo). Mazungumzo katika clip hiyo yalihusisha mipango anuai ambayo kwa ujumla ililenga kukihujumu chama cha demaokrasia na maendeleo, ambacho ndicho kilichowapa dhamana ya uongozi.

Baada ya kusambaa kwa ‘clip’ hiyo baadhi ya watu walitoa maoni tofauti. Wapo waliodai sauti hizo zimetengenezwa kwa teknolojia maalumu ili kuwachafua viongozi hao, na wengine wakidai ni sauti zao halisi. Je Ukweli ni upi?

Ukweli ni kwamba zile ni sauti zao HALISI na hazijatengenezwa. Sababu za kuamini kuwa zile ni sauti zao halisi ni kama ifuatavyo:

MOSI; Aliyevujisha clip hiyo kwenye mitandao ni Mhe.Anthony Komu mwenyewe kimakosa kupitia kundi la Whatsapp liitwalo ‘Kanda ya Kaskazini’ ambalo lina wanasiasa na viongozi wa vyama mbalimbali wanaotoka kanda hiyo. Inavyoonekana ni kwamba simu ya Komu hakuwa amelock screen kwahiyo ikawa inajibonyeza wakati akiendelea na mazungumzo na Kubenea. Kabla ya kutuma audio hiyo, Komu alituma meseji yenye maneno yasiyoeleweka. Wakati watu wakitafakari imekuaje, ndipo akatuma audio hiyo.

Kwahiyo ‘audio’ hii ni halisi na haijatengenezwa. Ukweli ni kwamba mzee wangu Komu teknolojia ilimshinda kidogo akajikuta amefanya makosa makubwa ya kimkakati.

Baada ya Komu kutuma audio hiyo watu walimshauri aifute, na kiongozi mmoja wa BAVICHA aliwasiliana nae akamwambia ameshaifuta. Lakini ikawa inaendelea kuonekana kwenye group. Tulichokigundua ni kwamba Komu alifuta kwake badala ya kufuta kwa wote (delete for all). Kwa mara nyingine tena teknolojia ikampiga teke mzee wangu Komu. Kwahiyo wanaosema clip hiyo imetengenezwa wanatoa maoni kwa mihemko bila kujua chimbuko la hiyo clip.

PILI; Jumapili ya tarehe 14 Oktoba, siku moja baada ya clip hiyo kuvuja majira ya saa 2 na dakika 33 hadi saa 2 na dakika 51 usiku Kubenea alizungumza na mzee mmoja anayeheshimiwa sana ndani ya chama (ninamhifadhi jina) kupitia namba yake ya simu +255782072292 location yake ikisoma 76W2+7P Kinondoni data centre ambapo ndio CL site aliyokuwa akitumia kuaccess data.

Kubenea alimuomba mzee huyo amuombee msamaha kwa Mbowe (ushahidi ninao). Mzee huyo alipomuuliza kama clip hiyo ni ya kweli au imetengenezwa alikiri kwamba ni ya kweli. Lakini Kubenea huyohuyo akaja kwenye group la Friends of Bavicha siku hiyohiyo na kusema haitambui clip hiyo, na inayosikika sio sauti yake. Nikacheka sana. Na vijana wake walivyo mazuzu wakamtetea kuwa sio sauti yake, kumbe boss wao ameshakiri na kuomba aombewe msamaha.

TATU; Leo kwenye kikao cha kamati kuu kinachoendelea hadi hivi sasa watuhumiwa wote wawili (Kubenea na Komu) walipopewa nafasi ya kujieleza wamekiri kwamba audio clip hiyo ni yao na wameomba masamaha. Bahati nzuri wamerekodiwa. Wapambe wanaobwabwaja kwamba clip hiyo sio yao wako uninformed tu. Kuna mengi yanayoendelea hawayajui.

Kwahiyo hoja kuhusu uhalali wa clip hiyo sio suala linalohitaji mjadala. Wanasheria wanasema the matter is not disputable. Mjadala hauwezi kuwa kwenye uhalali wa clip hiyo kwa sababu wahusika wameshakiri kwamba ni yao. Mjadala unaweza kuwa kwenye maudhui ya hiyo clip.

Kwa ujumla clip hiyo ina hoja mbili kubwa. Ya kwanza ni kumteka na kumpoteza Meya wa Ubungo Boniface Jacob ili kumpunguzia nguvu Mbowe, na ya pili ni kufanya mpango ili Mbowe ashtkakiwe kwa kesi isiyodhaminika (unbailable case).

Tuanze na hili la kumteka na kumpoteza Bonny. Hili ni jambo linalohitaji tafakuri pana sana hasa kutokana na matukio ya utekaji yanayoendelea hapa nchini. Kwanini wafikirie namna nzuri ya kumpunguzia nguvu Mbowe ni kumteka Bonny? Wana uzoefu gani na utekaji? Nani atakayefanikisha mpango wao huo? Kwa malipo gani? Utekaji huo ulipangwa kufanyika lini, wapi, saa ngapi na kwa kuwatumia kina nani?

Kwa vyovyote vile Kubenea na Komu hawawezi kuwa na ujasiri wa kumteka mtu bila kuwa na backup ya taasisi nyeti zitakazowalinda. Na kama wananchukia Mbowe kiasi cha kupanga kumteka na kumpoteza Bonny kwanini tusiamini kwamba wao pia ndio waliohusika kwenye kumteka na kumpoteza msaidizi wa karibu wa Mbowe, Ben Saanane?

Kabla Ben hajapotea alikuwa na ugomvi binafsi na Kubenea. Na Kubenea amemchafua sana Ben kupitia magazeti yake wakati akifanaya kazi makao makuu ya chama. Kubenea aliwahi kutunga uongo kupitia gazeti la Mwanahalisi kwamba Ben alitumwa na Dr.Slaa kwenda kumuwekea sumu Zitto Kabwe, lakini walipokutana Zitto akashtukia mpango huo na akakataa kunywa wala kula chochote eneo hilo. Lakini Zitto akaja kumuumbua Kubenea baada ya kusema hajawahi kukutana na Ben Saanane katika mazingira yoyote nje ya ofisi.

Hata Ben alipopotea Kubenea alishindwa kuficha chuki zake. Alihakikisha anahujumu zoezi la kumtafuta na akasema BEN AMEJIFICHA ILI KUJITAFUTIA UMAARUFU WA KISIASA. Akafika mbali kwa kusema BEN AMEONEKANA KWENYE VIJIWE VYA KAHAWA jijini Dar. Kubenea huyuhuyu leo anajadili kumteka na kumpoteza Meya Boniface Jacob, kwanini tusiamini anahusika pia na kumpoteza Ben?

Na kama wana ujasiri wa kujadili kuteka viongozi wenzao, ni wazi kuwa hili sio tukio lao la kwanza. Pengine wameshatekeleza matukio mengi ya aina hiyo. Halafu kama wanaweza kupanga kumteka mtu mkubwa kama MEYA bila kujali chochote, vipi kwa wanachama wa kawaida? Ikitokea mwanachama wa kawaida ametofautiana nao si ndio atapotezwa tu kama upepo? Hii inatilia Mashaka sana.

Inaonekana kuna nguvu kubwa sana nyuma ya hawa watu. Na hawafanyi haya kwa maslahi yao, bali ya aliyewatuma. Ingekuwa kwa maslahi yao wasingefikiria kuteka na kupoteza watu kwa sababu tu ya madaraka ya kisiasa. Lazima kuna nguvu kubwa nyuma yao inayowapa backup na kuwalinda dhidi ya uharamia wao.

Hoja ya pili katika mazungumzo yao ni kuhusu Mbowe kupewa kesi isiyodhaminika. Wanaamini hiyo itasaidia kumng’oa Mbowe madarakani na kumpachika Mwenyekiti wanayemtaka. Kwa lugha rahisi ni kwamba fitina zao zote za kumng’oa Mbowe zimeshindwa kwa hiyo wameamua kutumia umafia. Wanataka apewe kesi isiyodhaminika ili aozee jela.

Katika mapendekezo yao walionesha kusikitishwa sana na Kiongozi mmoja wa serikali ambaye walimuita ‘DHAIFU SANA’ wakidai anashindwa kumshughulikia Mbowe kwenye mambo makubwa badala yake anamshughulikia kwenye mambo waliyoyaita madogo. Mambo hayo madogo ni kesi za uchochezi zinazomkabili mbowe kwa sasa. Kubenea na Komu wanaona kesi hizo haziwezi kummaliza Mbowe, kwa sababu zinadhaminika.

Wanataka kesi ambayo haina dhamana, ambayo itamfanya Mbowe asote jela wakati kesi ikiendelea kusikilizwa. Na katika mapendekezo yao wakataja kesi ya uhujumu uchumi kupitia ruzuku za chama. Komu akinukuliwa akimwambia Kubenea kwamba ukimchomekea Mbowe kesi ya uhujumu uchumi, kupitia ruzuku unanmaliza.

Na kwa sababu wamepanga kumkomoa, kesi hiyo inaweza kuendeshwa polepole ili kumfanya aendelee kusota rumande. Kwahiyo hata akija kushinda atakuwa tayari ameshasota miaka mingi ndani. Just imagine anakamatwa leo halafu anakuja kushinda kesi mwaka 2024, ndipo anaachiwa huru kwamba hana hatia. Hatma yake kisiasa itakuaje? Na hatma ya CHADEMA itakuaje? Hapa ndipo unapogundua wabunge hawa wawili wanatumika kukihujumu chama chao, kwa maslahi ya watu wengine.

Hata kuhusu ruzuku wabunge hawa wanajua kwamba hakuna hata senti moja inayopita mikononi mwa Mbowe. Komu amekuwa Mkurugenzi wa fedha wa Chadema maika 10 anajua kuwa Mbowe ni signatory tu kama ambavyo yeye Komu alikuwa signatory. Ukiwa signatory huwezi kufanya maamuzi ya fedha peke yako.

Komu anajua kwamba kuwa Chadema ina watumishi walioajiriwa Makao makuu, ofisi za kanda na ofisi za mikoa (Sektretarieti, makatibu wa kanda na mikoa, maafisa makao makuu na kanda, wakurugenzi na madereva) wasiopungua 300 kwa nchi nzima na wanaopilwa mishahara kila mwezi. Kama kila mmoja angekuwa analipwa average ya milioni moja tu kwa mwezi maana yake ruzuku yote ingeishia kulipa mishahara.

Hapo bado kodi za pango kwa ofisi za kanda na mikoa. Bado mafuta kwenye magari, bado safari za nje ya nchi kwa viongozi, bado operesheni mbalimbali za chama kama uzinduzi wa sera mbadala uliofanyika majuzi, bado kuendesha mabaraza ndani ya chama. Hivi vyote vinahitaji fedha, na ni hizohizo milioni 300 za ruzuku zinazotegemewa. Hivi hizo Mbowe anazokula ni zipi?

Tatizo watu wanaongelea milioni 300 kama vile Chadema ni grocery ama pub. Milioni 300 kuendesha grocery ni pesa nyingi sana, lakini kuendesha chama kikuu cha upinzani chenye machinery, chenye ofisi kila kanda, kila mkoa, kila wilaya na kila jimbo, chenye watumishi, chenye wanachama zaidi ya milioni 6 ni fedha kidogo sana.

Mwaka 2014 nilishiriki kikao cha baraza la usuluhishi cha mkoa wa Mwanza ambapo Komu alibanwa kuhusu ruzuku wakati huo akiwa Mkurugenzi wa fedha na utawala. Nakumbuka alijibu kwa hisia namna ambavyo ruzuku za chama hicho hazitoshi na mara nyingi wanalazimika kutafuta wafadhili wa nje ya ndani ya nchi.

Akasema wakati mwingine wanakubali kufanya kazi kwa kujitolea kwa sababu fedha hakuna. Akaeleza kuwa Mbowe hajawahi kulipwa mshahara hata mara moja tangu aingie madarakani mwaka 2004. Kwa miaka yote amekuwa akifanya kazi kwa kujitolea ili pesa iliyokuwa imlipe mshahara ikajenge chama.

Komu aliongea kwa hisia sana na kusababisha ukumbi mzima kuzizima, na baadhi ya wajumbe kudondosha machozi. Lakini leo anasema Mbowe anakula pesa za ruzuku na atafutiwe kesi ambayo haina dhamana. Huu ni ushetani. Nilimpigia simu juzi ili nimkumbushe kuhusu tukio hili la Mwanza, lakini nilipojitambulisha tu kuwa mimi Yericko akakata simu.

Kwahiyo kwa kifupi wabunge hawa wawili ni miongoni mwa mamluki wengi walio ndani ya chama ambao wana mkakati maalumu wa kukihujumu chama na ikiwezekana kukiua. Mkakati huo inaonekana unafadhiliwa na kikundi fulani chenye nguvu nje ya chama.

Wabunge hawa walienda Ubelgiji na kumwambia mke wa Lisuu kuwa eti Mwenyekiti Mbowe anahusika na tukio la Lissu kupigwa risasi. Lengo lao lilikuwa ni kutengeneza conspiracy na kuhamisha lawama kutoka serikalini na kwenda kwa Mbowe na kutengeneza mgogoro ndani ya chama. Bahati nzuri mke wa Lissu ni ‘genius’ akawatimua na upuuzi wao.

NINI KIFANYIKE?

Kamati Kuu iwafukuze uanachama watu hawa leo ili iwe fundisho kwa wengine. Wamekihujumu chama kwa muda mrefu na mara zote wamekuwa wakijitetea hakuna ushshidi. Sasa leo Mungu mwenyewe ameleta ushahidi, hawana pa kuchomokea. Mungu hamfichi mnafiki.

Kwahiyo naishauri Kamti kuu ya CHADEMA isiwaonee huruma hawa waasi. Kupanga kumteka mtu na kumpoteza ni pamoja na kumtafutia kiongozi wenu kesi isiyodhaminika huo ni uasi, na muasi hatakiwi kuonewa huruma.

NINI KITARAJIWE?

Ikiwa Kamati kuu ya Chadema itawafukuza uanachama wabunge hawa, watakimbilia mahakamani. Taarifa za kina nilizonazo ni kwamba walifanya kikao na watu wa ‘system’ ambao ndio wanaowatumia. Wakawa na option ya kuunga mkono juhudi kabla hawajafukuzwa. Lakini wakaambiwa wakiunga mkono juhudi ni kukimbia vita, kwa sababu mpango wa kuisambaratisha Chadema utakuwa umefeli.

Kwahiyo wameambiwa wasubiri wafukuzwe kisha wakimbilie mahakamani, kisha mahakama itawarudishia ubunge wao. Na Spika ataendelea kuwatambua kama wabunge kupitia Chadema. Wanaamini hii itatengeneza mgogoro mkubwa zaidi ndani ya Chadema kwa sababu zitaibuka pande mbili zinazosigana. Upande unaowatetea na upande unaowapinga. Wanaamini wanachama watagawanyika na hivyo kumpunguzia nguvu Mbowe.

Lakini ukweli ni kwamba wakijaribu kufanya hivyo wataaibika kwa sababu hawana ushawishi wowote ndani ya chama. Kubenea na Komu kwa pamoja wakiambiwa waitishe mkutano wa siasa hawawezi kumobilize watu 100, labda wasaidwe kwa kuletewa mamluki.

Zitto alikuwa na nguvu sana kwenye chama na wafuasi maelfu lakini alishindwa kuipasua Chadema, sembuse hawa vibaraka ambao hawana ushawishi hata kwenye familia zao?
 
Komu ana bahati mbaya sana ametafuta ubunge muda mrefu na yuko hatarini kuupoteza ikiwa chama kitamfukuza ubunge.hayupo technical .... ni mwepesi sana, na sijui kwa nini anajiingiza kwenye chokpchoko asizomudu
 
Back
Top Bottom