Kikao cha CCM, UKAWA chavunjika

Kikao cha CCM, UKAWA chavunjika

amakyasya

JF-Expert Member
Joined
Jun 26, 2013
Posts
3,480
Reaction score
918
KIKAO kati ya Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na viongozi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kimeshindwa kupata muafaka baada ya pande hizo mbili kuendelea kuvutana hadi jana jioni.

Kikao hicho cha siri kilichoanza jana saa nne asubuhi katika Hoteli ya Sea cliff iliyopo Masaki jijini Dar es Salaam, kiliongozwa na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Fransis Mutungi.

Jaji Mutungi aliingilia kati suala hilo, baada ya kuona muafaka wa Ukawa kurudi bungeni umekwama kutokana na madai ya wajumbe wa CCM wanajadili mambo yasiyokuwamo ndani ya rasimu ya Katiba iliyowasilishwa na Jaji Joseph Warioba.

Madai mengine ya Ukawa ni pamoja na Mwenyekiti wa Bunge hilo, Samuel Sitta kutumia madaraka yake vibaya ikiwa ni pamoja na kupindisha kanuni za Bunge hilo.

Kutokana na hali hiyo, Jaji Mutungi alilazimika kuwaita viongozi wa CCM na Ukawa ili waweze kuwapatanisha ikiwa ni pamoja na kuwataka Ukawa warudi bungeni katika kikao kijacho ambacho kinatarajiwa kuanza Agosti 5, mwaka huu.

Ukawa unaundwa na vyama vitatu vya Chama cha Wananchi (CUF), Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na Chama cha NCCR-Mageuzi.

Akizungumza na MTANZANIA kwenye mahojiano maalumu yaliyofanyika jijini Dar es Salaam, Mwanasheria wa Chadema, Tundu Lissu, alisema mpaka jana jioni hakuna muafaka katika kikao hicho kutokana na kuendelea kuvutana.

"Nimetoka kwenye kikao lakini hakuna muafaka, hii inatokana na pande mbili kuendelea kuvutana, kwa hiyo nimewaacha waendelee kujadili suala hilo," alisema Lissu.

Alisema msajili ndiye aliyeitisha kikao hicho ikiwa ni pamoja na kutafuta muafaka wa suala hilo, lakini kwa dalili zinazoonekana hakuna muafaka hapo.

Hivi karibuni, Ukawa walidai kuwa hawawezi kurudi tena kwenye Bunge hilo mpaka wajumbe hao wa CCM watakapokubali kujadili rasimu ya Katiba iliyowasilishwa na Jaji Warioba.

Kumekuwa na juhudi mbalimbali za kutafuta muafaka kuhusu suala hilo ikiwa ni pamoja na viongozi wa dini, taasisi za kiraia na wadau mbalimbali ambao kwa pamoja wamekuwa wakiwasihi Ukawa warudi bungeni ili kujadili rasimu hiyo.

Source: Mtanzania
 
Naona bora tubaki na katiba hihi ya 1977
Hii katiba mpya itatugawa japo nililuwa napenda tupate katiba mpya
 
Katika maisha yangu naamini katika muafaka.kama chama chetu hakitakubaliana mchakato wa katiba mpya ukabaki njia kuu nawahikikishia itatutesa sana uchaguzi ujao 2015! Wapinzani itakuwa agenda yao kutumaliza.take it from me!
 
Hawana ubavu. Maana akili ya mbunge mmoja wa ukawa,sawa na akili za wabunge 10 wa ccm. Ila akili ya Tundu Lissu sawa na ma-ccm cabinet nzima.
haya ni mawazo ya wasiyokwenda shule kama wewe, elimu gani hiyo inasema akili ya fulani+akili ya fulani =akili ya fulani?. haya ni mawazo hata ya teja ni nafuu, ni mawazo ya mtu ambaye ana mapungufu fulani(shoga/mtindio wa ubongo) n.k. watu kama.wewe ni wa kupuuza kabisa, huwezi kuwa na msaada wowote katika jamii
 
Katika maisha yangu naamini katika muafaka.kama chama chetu hakitakubaliana mchakato wa katiba mpya ukabaki njia kuu nawahikikishia itatutesa sana uchaguzi ujao 2015! Wapinzani itakuwa agenda yao kutumaliza.take it from me!

Wewe ni mnafiki mkubwa tu, huna lolote, watu 200 hawawezi kuyumbisha taifa.taifa hili halikuota kama uyoga, litalindwa kwa gharama yoyote madam hila za vibaraka wa.wazungu watanzania tumeshazing'amua
 
Acha unafiki interahamwe wewe! Toka lini maccm wakataka katiba mpya?

Chguwa jina la kunipa ww
Ikifika uchaguzi hutasema tena tume ya uchaguzi haifai?
Nakulalamika tunataka tume iliyo huru?
Kama leo ww unataka madiliko kwa nn hutaki majadiliano na mwenzako?
Binadamu siku zote usipendi kile ulichosimamiya ndio kiwe kizuri ilihali wengine hawakitaki
Jambo zuti ni maridhiano tu
Imani ndio itakayo tupeleka mbele
Baki na imani ya vyma ww kila siku na chama tu
Hata mimi ninachama lakini mawazo yangu yanaweza yakafikiti na nikapingana na mawazo ya chama changu au viongozi wangu sio
Hiyo ndiokazi ya ubongo wangu niliopewa na mwenyezimungu
Niweze sumbuwa ubongo wangu kwa kufikiri na kuwaza
 
Hata wakiacha poa tu, tena ikibidi wasusie kabisa na uchaguzi mkuu mwakani ili wajifute kwenye ramani ya siasa.
Wamechanganyikiwa.
 
Back
Top Bottom