ALEXANDRE KAHUMBA
New Member
- Aug 25, 2017
- 4
- 1
Kati ya wanaume wenye uelewa wewe wa Kwanza.....wanawake wengi wameingia kwenye Matatizo kwa kupenda wanaume wa Maonesha
Samahani kwa kutumia lugha ya kebehi.Daaah..... Kimilioni kimoja...
Mkuu wewe unapokea ngapi
Mkuu amini Usiamini Kilimo kinalipa. Usikubali kupitwa mkuu.Kama ni kweli hongera.ila ukitaka kuwasaidia vijana hawa nenda inst huku hawapo kabisa kiukweli vijana wanachezea mitaji sana.
Pamoja kamanda[emoji56] [emoji56] [emoji56] [emoji56] usiwaze mkuu
Hii ni kwa wenye Uelewa tuu.Kati ya wanaume wenye uelewa wewe wa Kwanza.....wanawake wengi wameingia kwenye Matatizo kwa kupenda wanaume wa Maonesha
Ni kweli mkuu.maisha nikuchagua ulichagua ivyo na wengine wanachagua kwingine
hapa sawaMkuu amini Usiamini Kilimo kinalipa. Usikubali kupitwa mkuu.
Ukikosa kabisa Kwenye kilimo unapata chakula cha nyumbani cha mwaka Mzima.
Siri hii ni kwa wenye kufikiri si wenye kuona
Sasa hapo utumwa kwa wanawake unatoka wapi?? Labda ungesema kuwa mtumwa Wa mwili wako..Habari wakuu.
Wapo vijana wanaobabaishwa na wanawake. Utakuta kijana anahangaika Kwenda Gym kutengeneza kifua kwaajili ya kuwaridhisha wanawake.
Wengine hujipodoa na kuvaa hereni kwaajili ya kupendeza ili wawavutie kina dada.
Wapo wengine wanaojifanya mabingwa wakuhonga japokuwa pesa hawana. Mtu anapokea kimilioni moja basi kwa udogo wa akili huhonga akidhani ndio uanaume kumbe ni ujinga uliovuka mipaka.
Babu yangu aliwahi kuniambia; Michael Mjukuu Wangu wewe ni mwanaume, usije ukawa mtumwa wa wanawake. Usibabaishwe nao. Wao wapo kwaajili yako lakini si wewe kwaajili yao.
Maneno hayo nikiyakumbuka ndio yamenijenga mpaka hivi Leo.
Sibabaishwi na mwanamke yoyote yule.
Kuanzia kuvaa, kula, kunywa. Sifanyi kwaajili ya mwanamke yeyote.
Nilipokuwa Chuo niliishi maisha yangu. Nilinunua suruali tano, sharti tatu na fulana tatu.
Suruali mbili zilikuwa za kanisani. Mbili za chuo na moja ya kushindia.halikadhalika na sharti na fulana.
Nguo hizo zilikaa mwaka mzima. Ndipo niliweza kununua nguo nyingine.
Niliachwa na mademu kisa sikuwa mhongaji. Hilo halikunibadilisha tabia yangu ya ubahili.
Nilikumbuka neno moja tuu, nisiwe mtumwa wa wanawake.
Kwa vile sikuwa Mlevi na mademu walinipiga chini. Hivyo pesa yangu ilikuwa haina pakutokea zaidi ya kwenye miradi yangu.
Wapo mademu waliotaka kunibabaisha kwa kuniambia kwa nini narudia nguo Mara mbili. Wengine wakisema sijawahi watoa hata Lunch moja Cafteria lakini mwanaume niligangamala. Niliweka masikio pamba.
Mwaka Wa kwanza nilinunua shamba heka tano kwa laki mbili kwa kila heka huko Morogoro na kuyasafisha kabisa kwa gharama ya laki tano.
Mwaka wa pili nilizidisha ubahili hata kwangu mwenyewe ili kusave. Nilisikia aibu kumuomba hela mama.
Muda huu ndio wanawake walinikimbia kabisa. Na Mimi niliwaambia hamnibabaishi. Nilishirikiana nao katika ishu za kitaaluma tuu.
Nikalima tikiti heka zote tano, Mungu si Athumani nikapata kiasi kwa vile ilikuwa Mara yangu ya kwanza. Nilipata Milioni tisa.
Kiukweli nilifurahi. Ilikuwa mwaka 2015 nilipopata fedha hizo. Sasa nilipanga bajeti ya 2015/2016. Nikaandika vipao mbele vyangu.
Nikanunua cherehani tano za laki nne. Nikatafuta Fremu nikaziweka. Ikawa kila nikirudi chuo kwa vile ninauzoefu na najua kushona aina zote za nguo za kike nikawa nafungua fremu na kujipatia kipato.
Nikatafuta mafundi wa nne na Mimi nikiwa watano. Nawalipa kwa siku elfu 30 na wao kila siku lazima washone nguo tatu.
Tenda nazitafuta mwenyewe kupitia njia mbali mbali kama mitandao, kupitia kuhudhuria semina na mikutano ya watu wakubwa wenye uwezo.
Kwa kweli usipobabaishwa na wanawake kufanikiwa kwenye maisha ni lazima.
Nilipoanza kazi ya ufundi nguo walisema na kutoa maneno ya karaha. Nilipokuwa nauza matikiti yangu barabarani nikiwa nimeyapanga huku nimechomekea na tai shingoni mademu walinishangaa. Hawajui mwenzao napiga pesa wao wanashangaa tuu na kunipiga vibomu.
Sasa chuo tumemaliza, ajira zimekuwa adimu sana. Wanakuja wenyewe. Wanataka niwaajiri kwenye Stationary yangu.
Nawaambia wauze matunda ambayo nayaweka kwenye vibakuli na kusambaza wanasema wanasikia aibu.
Nawaambia wasambaze chupi,bikini, na boxer ninazozitengeza hawataki. Wakati Mimi nazipeleka kwa vijana wa karume na Matching Guys(Machinga).
Kwa sasa naandaa Bajeti ya kujenga katika kiwanja changu kilichopo Goba.
Pambano bado linaendelea.
Kijana mwenzangu usikubali kubabaishwa na wanawake.
Usikubali kuwa mtumwa Wa wanawake.
Kwa hisani ya Kiumeni.
Huwezi elewa kwa ubongo wa nyama Mkuu.Sasa hapo utumwa kwa wanawake unatoka wapi?? Labda ungesema kuwa mtumwa Wa mwili wako..
Haahhaa!Du Maendeleo Tilonda.
We kuwa bahili tu,mwisho wa siku ukifa mali zako zitaangukia kwa wafujajiHabari wakuu.

We kweli Bandu bandu. Mbona wanipa huzuni mkuu.We kuwa bahili tu,mwisho wa siku ukifa mali zako zitaangukia kwa wafujaji
Upo sahihi Mkuu.
Wapo wanaotoka na wanawake wengi lakini hawababaishwi.
Hakuna faida ya kutembea na wanawake wengi Mkuu. Mwisho wake si mzuri zaidi ya majuto.
Nakutania tu lakini ni kweli kabisa nimependa hiyo kauli ya kuwa wanawake wako kwa ajili yetu na siyo sisi kwa ajili yao nimeipenda sana na huwa ninaitumia sana mpaka mademu wananiambiaga naringa oooh mara mkorofiWe kweli Bandu bandu. Mbona wanipa huzuni mkuu.
Daah!