Kijana; Usibabaishwe na wanawake

Kijana; Usibabaishwe na wanawake

Ryan The King

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2016
Posts
2,789
Reaction score
2,706
Habari wakuu.


Wapo vijana wanaobabaishwa na wanawake. Utakuta kijana anahangaika Kwenda Gym kutengeneza kifua kwaajili ya kuwaridhisha wanawake.

Wengine hujipodoa na kuvaa hereni kwaajili ya kupendeza ili wawavutie kina dada.

Wapo wengine wanaojifanya mabingwa wakuhonga japokuwa pesa hawana. Mtu anapokea kimilioni moja basi kwa udogo wa akili huhonga akidhani ndio uanaume kumbe ni ujinga uliovuka mipaka.

Babu yangu aliwahi kuniambia; Michael Mjukuu Wangu wewe ni mwanaume, usije ukawa mtumwa wa wanawake. Usibabaishwe nao. Wao wapo kwaajili yako lakini si wewe kwaajili yao.


Maneno hayo nikiyakumbuka ndio yamenijenga mpaka hivi Leo.

Sibabaishwi na mwanamke yoyote yule.

Kuanzia kuvaa, kula, kunywa. Sifanyi kwaajili ya mwanamke yeyote.

Nilipokuwa Chuo niliishi maisha yangu. Nilinunua suruali tano, sharti tatu na fulana tatu.

Suruali mbili zilikuwa za kanisani. Mbili za chuo na moja ya kushindia.halikadhalika na sharti na fulana.

Nguo hizo zilikaa mwaka mzima. Ndipo niliweza kununua nguo nyingine.

Niliachwa na mademu kisa sikuwa mhongaji. Hilo halikunibadilisha tabia yangu ya ubahili.

Nilikumbuka neno moja tuu, nisiwe mtumwa wa wanawake.

Kwa vile sikuwa Mlevi na mademu walinipiga chini. Hivyo pesa yangu ilikuwa haina pakutokea zaidi ya kwenye miradi yangu.

Wapo mademu waliotaka kunibabaisha kwa kuniambia kwa nini narudia nguo Mara mbili. Wengine wakisema sijawahi watoa hata Lunch moja Cafteria lakini mwanaume niligangamala. Niliweka masikio pamba.

Mwaka Wa kwanza nilinunua shamba heka tano kwa laki mbili kwa kila heka huko Morogoro na kuyasafisha kabisa kwa gharama ya laki tano.

Mwaka wa pili nilizidisha ubahili hata kwangu mwenyewe ili kusave. Nilisikia aibu kumuomba hela mama.

Muda huu ndio wanawake walinikimbia kabisa. Na Mimi niliwaambia hamnibabaishi. Nilishirikiana nao katika ishu za kitaaluma tuu.

Nikalima tikiti heka zote tano, Mungu si Athumani nikapata kiasi kwa vile ilikuwa Mara yangu ya kwanza. Nilipata Milioni tisa.

Kiukweli nilifurahi. Ilikuwa mwaka 2015 nilipopata fedha hizo. Sasa nilipanga bajeti ya 2015/2016. Nikaandika vipao mbele vyangu.

Nikanunua cherehani tano za laki nne. Nikatafuta Fremu nikaziweka. Ikawa kila nikirudi chuo kwa vile ninauzoefu na najua kushona aina zote za nguo za kike nikawa nafungua fremu na kujipatia kipato.

Nikatafuta mafundi wa nne na Mimi nikiwa watano. Nawalipa kwa siku elfu 30 na wao kila siku lazima washone nguo tatu.

Tenda nazitafuta mwenyewe kupitia njia mbali mbali kama mitandao, kupitia kuhudhuria semina na mikutano ya watu wakubwa wenye uwezo.

Kwa kweli usipobabaishwa na wanawake kufanikiwa kwenye maisha ni lazima.

Nilipoanza kazi ya ufundi nguo walisema na kutoa maneno ya karaha. Nilipokuwa nauza matikiti yangu barabarani nikiwa nimeyapanga huku nimechomekea na tai shingoni mademu walinishangaa. Hawajui mwenzao napiga pesa wao wanashangaa tuu na kunipiga vibomu.

Sasa chuo tumemaliza, ajira zimekuwa adimu sana. Wanakuja wenyewe. Wanataka niwaajiri kwenye Stationary yangu.

Nawaambia wauze matunda ambayo nayaweka kwenye vibakuli na kusambaza wanasema wanasikia aibu.

Nawaambia wasambaze chupi,bikini, na boxer ninazozitengeza hawataki. Wakati Mimi nazipeleka kwa vijana wa karume na Matching Guys(Machinga).


Kwa sasa naandaa Bajeti ya kujenga katika kiwanja changu kilichopo Goba.

Pambano bado linaendelea.

Kijana mwenzangu usikubali kubabaishwa na wanawake.

Usikubali kuwa mtumwa Wa wanawake.


Kwa hisani ya Kiumeni.
 
Kweli wewe gangwe mkuu. Ila umekuwa tofauti kidogo asee, wanaume wengi wanakuwa na suruali chache mashati mengi ila wewe ulikuwa na suruali nyingi mashati machache!

Hongera kwa ugumu.
Yaa mkuu.

Shida ni kuwa Suruali za kanisani Hazivaliwi sehemu nyingine. Nikitoka church navua.
 
Ujue ni ngumu sana kumbadilisha mtu kwa kile alichoamua kukichagua katika maisha yake.

Kama mtu kaamua maisha yake yawe ya kubabaishwa achana nae. Kuna usemi unasema "aliyelala usimuamshe ukimuamsha utalala wewe"
 
Acha fix hakuna kijana wahivyo bongo hii
Kama umefika chuo unaweza kukubaliana na Mimi endapo ulikuwa ukijichanganya na vijana wenye uelewa wa maisha lakini kama ulikaa na wale wanaobadilisha simu kila bumu na kulala hostel bila kuhangaika ndio maana unasema hivyo.

Njoo hapa makumbusho uone mabinti wachuo wakisimamia biashara zao.

Njoo hapa Mbezi kwa msuguri uone vijana na mabinti wa chuo wenye akili za pesa.

Wewe kalia hivyo hivyo
 
daah mkuu... sio kwa ubahili huo but all in all nikupongeze kwa kupiga hatua mkuu... huo ndio uanaume.... ukimaliza kujenga vuta jiko weka ndani endelea kupiga pesa all the best mkuu
Kila kitu ni maamuzi tuu.

Ukiwaendekeza wanawake unaweza jikuta unatoka katika mstari.

Wanawake wanaweza kukufanya ununue vitu vya hasara tuu. Vitu visivyokuingizia pesa. Embu fikiria kijana ananunua kiatu cha laki moja na simu ya laki sita wakati yeye hana mshahara wala pakuingizia pesa.

Kila kitu kitafanyika kama Kilivyopangwa Mkuu
 
Ujue ni ngumu sana kumbadilisha mtu kwa kile alichoamua kukichagua katika maisha yake.

Kama mtu kaamua maisha yake yawe ya kubabaishwa achana nae. Kuna usemi unasema "aliyelala usimuamshe ukimuamsha utalala wewe"
Kweli kabisa mkuu. Lakini ili hili taifa liendelee linahitaji watu wasiobabaishwa na vitu vya kijinga.

Hata wanawake wasiobabaishwa na wanaume ndio wenye maendeleo na elimu ya kutupa.
 
Angalia huo ubahili usije ukauendeleza hadi kwenye familia yako, mke anachakaa kisa ubahili.
Hahaaaa!!!

Ubahili una wakati wake mkuu.

Kuna wakati wa kukusanya na wakati wa kutawanya. Kwa sasa mama yangu na wadogo zangu wanapata 20% ya mapato yangu.

Mke Wangu lazima afaidi Mali zangu. Kwani atakuwa naye katika upangaji wa bajeti ya mwaka
 
Back
Top Bottom