Maboresho ya elimu ni pamoja na Walimu

ichumu lya

JF-Expert Member
Aug 11, 2016
2,605
2,729
Good morning.
MABORESHO YA ELIMU BILA WALIMU

Kinachotushinda nini! Nimatumizi mazuri ya akili. Sioni sababu ya kuagiza mitungi hii India na china? Ni kukosa ubunifu na Elimu mbovu inayotolewa nchini inayomfanya kijana kuwa tegemezi anasoma ili afaulu mitihani na kuajiriwa ajira pekee inayolipa Tanzania na Africa kwa ujumla.

1.Siasa
2.Dini

Aya maeneo yanategemea unavyoweza kutumia mdomo wako.

Kama tunataka kwenda na dunia hii tukubali kuandaa wataalamu kuanzia elimu ya msingi maana mali ghafi tunazo tunahitaji utashi wa kisiasa na uthubutu.

Aya mambo ya kuajiriwa yabaki mengineyo ili tuondoe vijana wengi kukimbilia mijini kutwa wanazunguka na bahasha za kaki kutafuta vibarua.

Ukienda China utakuta bettery za magari na charger za simu zinatengenezwa na watoto wadogo tena wa primary lakini Tanzania mtu mwenye digree hawezi kutengeneza ata njiti za meno (tooth picks)
yaani full vichekesho Professor wa uchumi hawezi ata kuendesha saccos ama kibanda cha Mpesa lakini mtaji ule ukimpatia kijana aliyefeli darasa la saba baada ya miaka mitano atamuajili msomi wa digree.

Mfumo wa Elimu nchini ni mbovu unandaa wapiga maneno sio watendaji ndiyo maana wasomi wetu waliobahatika kuingia kwenye siasa na kuingia bungeni wanazidiwa na waliofeli form IV katika kuwaza na kujenga hoja hii inatokana na aina ya elimu ya juu wanayokutana nayo inayowanyang'anya wasomi wetu uwezo wa kujiamini.

Nini kifanyike:Viongozi acheni maneno na maandishi mareefu yasiyotekelezeka boresha Elimu ya msingi mtoto anapomaliza Elimu ya msingi awe na uwezo wa kutengeneza kitu maamuzi yabaki kwake aendelee mbele au aingie mtaani kuanzisha kiwanda kidogo na baadaye kiwanda kikubwa acheni kulazimisha elimu ya sekondary na vyuo ibakie kuwa utashi sio lazima.

Nashukuru kwamba baada ya miaka mingi sasa kuna Rasimu ya Elimu yenye matumaini lakini isiishie kwenye maneno tunataka utekelezaji. Juzijuzi Waziri wa Elimu alitangaza mabadiliko ya shule za bweni kwamba watoto wadogo kuanzia chekechea mpaka darasa la tano wasikae bweni lakini wenye shule za bweni wana ela na ushawishi mkubwa wakapinga mpango huo na Waziri akasalimu amri ndio maana ata kwenye Rasimu ya Elimu hakuna kabisa mpango huo.

Narudia kusema Elimu ya Tanzania iko mikononi mwa wafanyabiashara wa mashule tena wasio na Elimu kubwa/wamiliki wa mashule. Serikali haina mpango mkakati wa kunusulu Elimu ya nchi yetu hatuwezi kuzungumzia maboresho ya Elimu uku Walimu wakichukuliwa kama chombo kisicho na thamani walimu wanaongoza nchi hii kwa stress kutokana na madeni makubwa wanayokopa kwenye taasisi za kifedha zenye riba kubwa ili waweze kumudu ghalama za maisha kutokana na mfumko wa bei nchini.

Kama tunataka matokeo mazuri ya kielimu tuanze na walimu walipe mishahara sawa na kazi zao kima cha chini kabisa Mwalimu alipwe milioni mbili (2, 000, 000/) tukifanya ivi tutainua hali na moyo kwa walimu watafanya kazi bila kuwaza kuuza kashata, ubuyu na kabaragala watakuwa karibu na wanafunzi watataka kujua tatizo la kila mwanafunzi lakini pia tutakuwa tumewaondolea mikopo umiza na kuwarudishia heshima katika jamii.

@katikabakama.

 
Back
Top Bottom