Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 34,059
- 79,413
Mpo Salama!
Kumhudumia Mchumba au mpenzi wako huwezi Sifiwa Wala kuonekana mwanaume wa maana mahali popote pale zaidi ya kuonekana kijana asiyejitambua.
Wazazi wako wenyewe waliokuzaa wakisikia kitu kama hicho watakuona hamna kitu.
Ukitaka ujue Jambo hili, siku huyo mwanamke akuache ndio utajigundua kuwa ulikuwa mpimbwe (mtu maamuma).
Kama mwanamke hawezi kujihudumia kwa matumizi yake binafsi huyo hakufai. Kama wao wenyewe wanavyokuona wewe nawe waone vivyohivyo. Kipimo wanachokupimia kitumie hichohicho kuwapimia. Hiyo ndio namna ya kuyakabilia maisha yako kijana wangu.
Akikuambia atachukuliwa na mtu mwingine mwambie aende tuu salama. Nawe utapata mwingine. Usiwe Mjinga.
Kama hawezi kujihudumia mwenyewe achana naye. Atakusumbua huyo.
Hudumia Mkeo. Huo ndio uanaume. Lakini sio kuhudumia mpenzi au Mchumba huko ni kutokujitambua.
Kama unahisi unakiherehere cha kuhudumia muweke ndani awe Mkeo umhudumie huyo mtoto mzuri.
Moja ya ishara ya kuwa huna Akili na kizazi chako kitakuwa Maskini ni kuangalia matumizi yako binafsi. Vipaombele vyako.
Mwenye jukumu la kumtunza mwanamke ambaye hajaolewa ni Babaake, au ndugu zake wa kiume.
Ukishamuoa ndio unakuwa na huo wajibu.
Kupeana zawadi ni Jambo la kawaida kwa Watu wanaopendana.
Lakini kumhudumia mtu ni suala la kiwajibu na kimajukumu na yapo chini ya Sheria za asili, za Dini na Sheria za nchi.
Sheria zote hizo hazikuruhusu kumhudumia Mchumba au mpenzi. Ogopa matapeli!
Jioni njema