Kijana epuka kutoa pesa hovyo, jinsi ilivyo ngumu kupatikana pia iwe ngumu kutoka

General Mangi

JF-Expert Member
Dec 21, 2013
15,301
23,025
Heri ya Mwaka Mpya waungwana.

Leo napenda kushare na ninyi wana MMU hasa wanaume ambao wana ndoto ya kufika mbali.

Imekuwa kawaida sana kwa mwanaume kutoa pesa au kuhonga (nazungumzia kwa wale mabachela). Vijana wengi tumekuaa wepesi sana kutoa pesa kwa mwanamke ambae huna malengo nae au hata kama una malengo naye lakini matumizi yamekuwa makubwa sana kwake.

Kwa kijana ambae umezaliwa kwenye familia duni, ni wazi kwamba kama inataka kuwa na mapesa mengi kuna vitu lazima uviweke kushoto.

1. Kuhonga
2. Starehe
3. Michango isiyo na umuhimu.

Mwaka 2017 niliamua kufanya maamuzi ya magumu ambayo yalinifanya nionekane tofauti lakini ni mwaka ambao nilipata mafanikio.

Kwanza nilipunguza idadi ya wanawake, nikabakia na mmoja ambaye hata hivyo tulishindwana kutokana na kupenda kutumia pesa pasipo kuitafuta.

Ilikuwa ngumu sana kuamua hivi kwani hakuna kiti kigumu kama kumweleza mpenzi wako kuwa huna pesa, lakini mwishowe nikazoea.

Nilimu kupunguza marafiki wasio na umuhimu. Marafiki wengi ni mzigo, mara leo nirushie elfu 5, mara vocha. Unaweza dharau vipesa hivyo lakini nikwambie ndugu, HAKUNA PESA NDOGO. Wengi waliniona naringa, mchoyo, najitenga lakini ndiyo njia ambayo kwa hali yangu nimeamini itanifikisha mbali, na nimepata matokeo mazuri.

Niliamua kutoshiriki kwenye michango isiyo na umuhimu mfano harusi. Mimi naamini harusi ni jambo binafsi, kama unafanya harusi unapaswa kugharamia kila kitu.

Kutumia pesa za watu kufanya anasa ni ujinga. Mimi kama nitafanya harusi sitomchangisha mtu, hivyo nami sitachangia harusi ya mtu.

Niliamua kupunguza matumizi yasio na lazima, mfano kwenda club, kupiga vyombo, vyakula vya gharama, kupenda vitu vya kisasa n.k

Nilimua kuacha usharobaro, kujifanya classic, msomi, hii ilileta ugomvi hata na mpenzi wangu niliye kuwa naye.

Anyway, nchotaka kuwambia vijana wenzangu, heshimu sana pesa. Pesa ina hitaji nidhamu sana.
Usiendeshwe na hisia za kimwili vinginevyo hutaki kuwa na mapesa mengi au kuja kuishi maisha mazuri.

Ukifikia ujasiri wa kufanya hayo hapo juu, stori za vyuma kukaza utasikia kwa wenzio.

2018 lazima tufanye kweli.

Mangi.
 
Kweli kabisa mkuu am a lady but kwa hili naunga mkono hoja ukiheshimu matumizi hakuna kitachoharibika na njia nzuri ya kutunza pesa ni kupunguza matumizi yaso msingi wazungu wanaitaga luxury ukiweza hapo basi malengo na mafanikio ulojiekea utayaona na kuyafikia. Bora uonekane bahili lakin kuna vtu vya msingi unafanyaa.

Asante kwa kutukumbusha tena
 
Aisee uko kama Mimi Mwaka 2015. Hela kama Milioni Milioni hizi nilishika sana Ila Nikaja kuharibu Nikampa mimba mdada wa watu .. Akaja kujifungua kwa Kisu ... Aisee imenicost sana Najutaaaa Hawa wanawake Waangalie tu kwa Macho Leo hatakuja kwenye siku zake Ila Kesho atakuletea ukipiga Tayari Mimba .......

Nilikuwaga Stoagi hela Mimi tatizo nilikosea Nilikuja kufanya nae Mpenzi Ndani kwangu (room ya kupanga ) akaaona Assets nilizonazo so akafikiri Ntamuoa .... Aiseeee Hakutaka kuniambia Ila nilikuja kujua baada ya kupata mimba anataka aishi na Mimi ndani ..... Aiseee Wanawake Hawa Hawajui ugumu wa maisha tujitahidi kuwaepuka Saiv na Make Money nalea Mtoto wangu ...kuoa bado bado sana ..... Namshukuru Mungu Hela bado Nazipata 770k per Month
 
Kweli kabisa mkuu am a lady but kwa hili naunga mkono hoja ukiheshimu matumizi hakuna kitachoharibika na njia nzur ya kutunza pesa ni kupunguza matumiz yaso msing wazungu wanaitaga luxury ukiweza hapo basi malengo na mafanikio ulojiekea utayaona na kuyafikia, bora uonekane bahili lakin kuna vtu vya msingi unafanyaa.

Asante kwa kutukumbusha tena

Vijana wengi kuna kipindi wanapata pesa sana, tena nyingine hujui zimetoka wapi lkn hawajui hicho kipindi kitapita na kama hukufanya jambi la maana hupati tena. Inakuwa kama laana flani hivi.
 
Kama ulizaliwa na moyo wa kutoa, kujali hii mbinu huwezi kabisa binafsi mimi nilishashindwa kabisa kumnyima mtu hela kama ninazo. ikitokea nimemnyima basi nitaumia sana nafsini mwangu.

Kama we ni mbahili ni mbahili
 
Aisee uko kama Mimi Mwaka 2015 ... Hela kama Milioni Milioni hizi nilishika sana Ila Nikaja kuharibu Nikampa mimba mdada wa watu .. Akaja kujifungua kwa Kisu ... Aisee imenicost sana Najutaaaa Hawa wanawake Waangalie tu kwa Macho Leo hatakuja kwenye siku zake Ila Kesho atakuletea ukipiga Tayari Mimba .......


Nilikuwaga Stoagi hela Mimi tatizo nilikosea Nilikuja kufanya nae Mpenzi Ndani kwangu (room ya kupanga ) akaaona Assets nilizonazo so akafikiri Ntamuoa .... Aiseeee Hakutaka kuniambia Ila nilikuja kujua baada ya kupata mimba anataka aishi na Mimi ndani ..... Aiseee Wanawake Hawa Hawajui ugumu wa maisha tujitahidi kuwaepuka Saiv na Make Money nalea Mtoto wangu ...kuoa bado bado sana ..... Namshukuru Mungu Hela bado Nazipata 770k per Month
Pole mkuu, hiyo ni mitihani unapaswa kutafuta majibu yake kwa umakini. Sasa ni kukaza zaidi
 
Nimeshangaa kuiona hii post.
Nimetoka kutuma elfu 25 kwa Jamaa zangu wawili muda huu.

Mtoa Mada una lengo zuri la kuwafanya watu kuwa wabahili kwa maendeleo yao. Lakini fahamu kusaidia kunakuweka sehemu nzuri ya wewe kusaidiwa pia.
Mi nashauri utoe pesa pale unapoona Mtu anaekuomba anashida ya kweli.

Mi huwa najisikia raha napotoa pesa kwa mtu mwenye shida haswa. Najua hawezi nisahau. Ipo siku atanipa msaada pia, unaweza kuwa sio wa fedha.
 
Back
Top Bottom