Kijana badilika acha huu ujinga mara moja

Kijana badilika acha huu ujinga mara moja

Sasa au anaowaona washamba wa matumizi wakiamua kuacha matumizi sijui hayo magunia yake ya mahindi atayauza wapi! Fikra za kijinga sana hizi..
 
Ndio wale wale wanaoza vitabu vyenye mbinu za utajiri,halafu wanasubiria mauzo ya vitabu badala ya kuzitumia hizo mbinu walizoandika humo.
Ila uko sawa ni kama kibao kimeandikwa Mwagauno pub ukikisoma na kufata uelekeo kinavyoelekeza utafika Mwagauno pub ingawa chenyewe toka kimetengenezwa na kuandikwa hakijawahi kufika wala hakitakaa kifike huko kinapoelekeza.
Huu uzi umeifanya bia yangu iwe chungu.
 
Habar za muda huu, wana JF ujumbe huu uende kwa kijana yeyote anaitaka kesho iliyo njema.

Matajiri wanaishi kama masikini na masikini kama matajiri, Tajiri ananunua simu ya sh 300,000/= na anatoa 4p airtime ya mwezi mzima.

Masikini ananunua simu ya sh 1,200,000 na anajiunga kifurushi cha tsh 1000/= kwa siku mfanyakazi anapokea mshahara wa tsh 750,000/= na anafanya birthday part ya sh 1,000,000/=

Vijana wa shamba wanaoishi mikoani kazuramimba kila mwisho wa mwezi ananunua debe 6 za mchele, debe moja ni sh 30, 000/= kwa mwezi ni 180,000 Tayari ni gunia moja.

Baadhi ya vijana wa dar wanaweka akiba 180,000/= ya kutumia kila ijumaa na masister duu na kupiga picha za kuweka Instagram.

Kijana wa kigoma anayenunua debe 6 za mchele kila mwezi kwa mwaka anakuwa na jumla ya debe 72 ambazo ni sawa na gunia 12 za mchele mwisho wa mwaka.

Mwaka mmoja una weekend 52 kama wewe ni mzee wa kula bata na kila weekend anatumia sh 100,000 basi kwa mwaka anakuwa anatumia sh 5,200,000/= je hii pesa kama ungeitumia kama yule kijana wa kigoma anayenunua debe 6 kila mwisho wa mwezi unafikiria ungekuwa wapi?

Je unajua magazeti yanayoandika bei za mazao Tanzania? Unajua maana ya standing order back. Tumepewa akili kubwa sana na mwenyezi Mungu ila baadhi ya vijana wanaweka akiba 180,000/= ya kutumia kila ijumaa na masister duu na kupiga picha za kuweka Instagram.

Tumepewa akili kubwa sana na mwenyezi Mungu ila social media imetufanya tupende kusoma udaku na mapenzi.

Badilisha mfumo wa matumizi ya smart phone, ubadili fikra na ufute marafiki wanaokupa habari za umbea.

Change today for the better tomorrow.
usitufundishe matumiz
 
Back
Top Bottom