Kijana auawa na kuporwa simu

KISIWAGA

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2015
Posts
8,020
Reaction score
16,603
Mkazi wa Mwananyamala, Manjunju mkoani Dar es Salaam, Billal Hoza (21), amefariki dunia baada ya kuvamiwa na kundi la vijana waliomchoma kisu sehemu mbalimbali za mwilini na kumpora simu.

Vijana hao wapatao watano walimvamia kijana huyo aliyekuwa amekaa nje ya nyumba yao na kumchoma kisu mgongoni, upande wa moyo. Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo lililotokea juzi saa 3:30 usiku, wakati Hiza na rafiki yake wakiwa wamekaa barazani nyumbani kwao, wakichezea simu.

“Wakati wanachezea simu walipita vijana kama wanne, kati yao mmoja akamfuata huyu kijana (Hoza) akampokonya simu, akaendelea kutembea na wenzake, ndipo Hoza akamfuata, akambana na kumtupa chini na mmoja wao akatoa kisu na kumchoma."
 
Awekwe korokoroni kwa kushindwa hata kutoa msaada wa kupiga yowe
Suspect namba 1. Maana ata hao watu watano nadhani ni statement yake. Sasa ebu polisi wafanye Intelijensia yao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…