Kijana Amiri Mtoi mhanga wa bomu la Arusha amezikwa leo Mkuzi - Lushoto.

Mtoto wetu huyu amekufa bila hatia, moja kwa moja huyu anakuwa miongoni mwa malaika ila kitu cha kukumbuka damu hizi safi changa zisizo na hati huwa zinalia na majibu yake ni haraka sikilizia tuu siku chache zijazo utasikia kilio kutoka upande wa pili! Amir ni kiongozi, umetuongoza vyema pumzika kwa amani!!
 
Poleni sana Mkuu Mohamedi Mtoi, Mungu azilaze mahali pema peponi roho za marehemu wote walioaga dunia kwenye mlipuko wa bomu hapa Arusha.
 
Poleni sana wafiwa, watoto waachwe majumbani kuwatumia kwenye Mambo ya kisiasa si busara hakuna tofauti na wale wanaowatumia kwenye Vita, Mtoto mdogo masikin ya Mungu katolewa Kafara ili watu wapate Umaarufu wa kuitwa Wapambanaji, Ameir nenda kwa Amani ila waliokutoa kafara nao Lazima watolewe Kafara hata kama wana Mapembe makubwa kiasi gani, wengine bado wamejificha wanatengeneza Movie na kupanga Uongo!
 
Poleni sana wafiwa wote. Sote tunaungana katika majonzi haya makubwa ambayo yangeweza kuhepukika kama tungekuwa na utawala unaojali utu na kuthamini uhai wa raia wake. Tunawaombea Mungu awape faraja zake na kuwapa ujasiri wa kulikabili tukio hili la kinyama na la kusikitisha sana. Mungu amlaze pema kijana wetu mpendwa Amiri Mtoi, AMEN.
 
Kama namwona Mwigulu saa izi na lile vazi lake la kishirikina anavyofurahia sadaka aliyoitoa vile! Lakini akumbuke kuwa kila nafsi itayaonja mauti.
 
aisee! pole sana ma bro mohamed mtoi.

naomba hili pia liwe angalizo kwetu sisi wazazi, watt sio vyea kuwapeleka kwenye mikutan ya kisiasa kwasabbu hatuna uhakika na usalama wetu. ni busara kumfundisha mtoto kuwa raia mwema na kumfundisha elimu ya uraia akiwa nyumba lakin maeneo ambayo mtoto kama mtoto hawez kusikika msiwapeleke jamani. kumbuka kwamba mtoto huyu mdogo hata kura hapigi maskini ya Mungu halafu anatolewa uhai kwa kitu asichokijua kabisa tena ambacho yeye kwa utash wake hajui hatima yake ni nini.

nimeumia sana kwa hawa watoto mie niseme wanangu waliopoteza maisha. but why kids??
 
Last edited by a moderator:
Pole sana kaka kwa yote na pia mpe pole kakayetu kwa kuondokewa na kijana pasipokutarajia, kwakeli ina uma sana ila ngoja tumwachie MOLA.
 
Pole sana kamanda Mohamedi Mtoi kwa msiba huo ambao umesababishwa na binadamu waliokosa ubinadamu. Kwa hasira nilizo nazo naomba niishie hapo tu.
 
Last edited by a moderator:
Naomba Mungu niwe hai ili niuone utawala mpya jinsi utakavyowakomboa wanyonge.EEEeeh Mungu sikiliza kilio chetu naweka mbele yako damu hii isiyokua na hatia iliyomwagwa kwa hila uipe haki yake.
 
...Inna Lillahi wa inna ilaihi raji'un...

Tuko pamoja na familia yako kaka Mtoi katika janga hili linaloikabili nchi yetu. Kila chenye mwanzo kina mwisho.
 
msiba wako ni msiba wetu sote mkuu,natuma salama za rambirambi kwako na kwa familia yako"Tulianza na Mungu na tutamaliza na Mungu"


I CAN FEEL THE PAIN,ILA YOTE YANA MWISHO,POLE SANA MOHAMEDI MTOI NA PIA RIP MTOI jr
 
Tupowe sote kwa msiba Huu. Wale madhalimu hawazidi kitu ila khasara tu ndio IMO kwenye Qurani. Kwa hivyo, kuwa wenye kusubiri na Mungu atawaumbua hapa hapa Duniani
 
Pole zangu kwa familia nzima ya Mtoi.
Pumzika kwa amani Amir.
Tulikupenda, tunakupenda na tutazidi kukupenda, daima utakumbukwa kama SHAHIDI wa mabadiliko.
Haujafa Bure!
 
Back
Top Bottom