MpiganiaUhuru
JF-Expert Member
- Mar 31, 2012
- 777
- 911
Wadau,
Nimekaa, nikatafakari juu ya taarifa inayohusu mlipuko huko Arusha na kujiuliza maswali haya bila jibu:
Naomba mnisaidie kupata majibu ili roho yangu itulie kwenye msimamo mmoja! Ahsanteni.
Nimekaa, nikatafakari juu ya taarifa inayohusu mlipuko huko Arusha na kujiuliza maswali haya bila jibu:
- Ni kwa nini Polisi waende kwenye mkutano wa hadhara (kama huo wa huko Arusha) huku wakiwa na silaha za moto?
- Je? Sheria za ulinzi na usalama hasa zile zinazowasimamia Polisi zinasemaje kuhusu ubebaji na utumiaji wao wa silaha za moto?
- Hata kama ni kwa kujihami na fujo za raia, yale maji ya kuwasha, risasi za plastic, virungu, n.k viko wapi mpaka watangulize silaha za moto?
- Hao viongozi wetu (Pinda, Kikwete, Lukuvi, n.k) ambao mara kwa mara wamekuwa wakiwakingia kifua hawa Polisi wanaoua raia mara kwa mara nao hawajui hizo sheria? Au wao ndio wanaowatuma? Mbona watu kama Pinda na Kikwete hawafananii kuwa na roho kama hizo? (Labda Lukuvi).
- .........? :shock:
Naomba mnisaidie kupata majibu ili roho yangu itulie kwenye msimamo mmoja! Ahsanteni.