Kijana aliyefiwa na wazazi wake kutokana na mabomu anatafuta wanasheria kufungua kesi

DENYO

JF-Expert Member
Sep 14, 2010
698
57
Kuna kijana yupo gongo la mboto wazazi wake wote wawili wamelipuliwa na kufa kwa mabomu ya gongo la mboto, anatafuta wanasheria ili afungue kesi dhidi ya serikali kwa uzembe huu uliopindukia madai yake ni,

1. Familia yake ina hati ya makazi husika

2. Wazazi wake wote wamefaliki kwa mabomu

3. Anadai mwinyi na mwamunyange kufikishwa mahakamani

4. Anadai watu hao watimuliwe kazi

5. Anadai serikali ihudumie maisha yake mpaka kufa au imuue na yeye

6. Anadai tamko la serikali kuhusu kuhamisha maghala haya maeneo ya watu

7. Anadai bendera ishushwe nusu mlingoti kwa siku 100

8. Anadai wale wengine wote waliosababisha tukio hili kufukuzwa kazi na kufikishwa mahakamani.

Je wanasheria mpo? Wapi marando, wapi wakongwe wote wa sheria? Wapi mtikila? Wapi tls? Wapi haki za binadamu? Anatafuta msaada amesema haiwezekani viongozi wanamtembelea wanachekacheka kana kwamba wamefurahia tukio hili kubwa na lisilo sahaulika kwake maisha yake yote.
 
Dah maskini!
Nafikiri atapata ila nashauri ungeipeleka jukwaa la sheria.
Kule nahisi wanasheria wanatembelea tembelea.
 
i would love to see this...
I would even send money to support his cause...
 
Anaweza kufanya hivyo lakini tatizo ni fedha za kuendeshea hiyo kesi, nani atalipa? Any way, ngoja tusubiri wanasheria tusikie wanasemaje. Lakini madai ya huyo kijana, kama kweli yupo, yana mantiki.
 
Nipe contact zake, nitamwunganisha kwa wakali wa sheria wanaotafuta umaarufu tu, wala hawana haja na fedha zake. Ila asiwe na haraka, kwa vile jamaa wanaweza kuwa tayari kushika kesi yake baada ya miezi mitatu au zaidi.
 
Kati ya vitu ambavyo vimenifurahisha leo ni hii habari ya huyu kijana. Hivyo ndo tunataka jamii i-react kufuatia kauli za kibabe za wahusika za kusema "Hajihuzulu mtu hapa". Wacha sheria ifanye mambo yake.

Swala la cost siyo issue, kwa swala la msingi kama hili, wasamalia tupo wengi, cha msingi taratibu zote kuanzia mwanzo zifuatwe kama sheria inavyosema. Hii imekaa vizuri, nimeipenda. Pole sana ndugu yetu, msiba ni wetu wote, Tunakuunga mkono, please go ahead. Wanasheria: hapa ndo pa kutema cheche za ukweli.
 
Back
Top Bottom