Kijana aliyeambukizwa UKIMWI mahabusu

Kijana aliyeambukizwa UKIMWI mahabusu

Na wazazi wamebaki kimya bila kuchukua hatua? Shule gani iyo ilishindwa kwenda kumdhanini mtoto wakijua anatoka nje ya nchi? Dah watu wana moyo mm ingeeleweka
 
hii sio story ya kweli mkuu labda alikuwa Zimbabwe...South Afrika huwezi kukaa police station kwa siku 5 mfululizo tena ukiwa ni mwanafunzi
 
Sasa hapo wazazi waangalia malezi kivipi tena, yani ni kama balaa tu limeamua kutokea, walimpeleka kusoma kwa lengo jema, yaani hapa wakulaumiwa ni shule husika, hivi kweli mtoto unamuwekaje jela ya watu wazima??? Mama alipaswa kuishtaki shule husika sema ndio hivyo tena.
Kwani Tanzania hakuna shule nzuri. Mbwembwe na sifa za kijinga za wazazi zimegharimu maisha ya kijana. Aibu kubwa sana kuwa mtumwa wa mawazo. Shenzy zao hao wazazi.
 
Inasikitisha sana....! Wazazi tuangalie malezi ya Vijana wetu....!

Sasa malezi katika hali kama ile yanahusikaje? Angelikuwa kalelewa vibaya bila shaka asingepambana kule mahabusu. Lakini kitndo cha kupambana, kupiga kelele, kuenda kushtaki polisi, kulia na kuendelea kukosa amani hata wakati ametoka South yuko nyumbani, kijana wa watu kalelewa katika maadili sahihi kabisa ya kifamilia. Haya mengine huwa ni malimwengu tu yanawakuta watoto hata bila wao kupanga wala kupenda.

Kama shule nzima iliandamana, wakakamatwa wanafunzi, wenzake wakawekewa dhamana, yeye hakuwa na mtu wa kumdhamini, akaenda kubakwa mahabusu nje y aridhaa yake. Akawaeleza wazazi wake kwa huzuni. Kosa la mtoto na mzazi liko wapi?

Labda kumpeleka nje ya nchi akiwa mdogo. Lakini sasa yuko secondary, kitu ambacho kingetokea hata akiwa TZ. Mungu aikumbuke dunia!.
 
Kwani Tanzania hakuna shule nzuri. Mbwembwe na sifa za kijinga za wazazi zimegharimu maisha ya kijana. Aibu kubwa sana kuwa mtumwa wa mawazo. Shenzy zao hao wazazi.

Tanzania watoto hawapelekwi mahabusu? Mahabsu Tanzania hawabakwi? Unakumbuka habari ya mashehe wa Zanzibar? Tena wengine hawabakwi mahabusu. Angalia shule wanazosoma watoto wa kawaid a huku wakiwa wamechanganyikana na waarabu. Ni hatari sana. Mungu alinde watoto wetu. Inaumiza sana!
 
Kwani Tanzania hakuna shule nzuri. Mbwembwe na sifa za kijinga za wazazi zimegharimu maisha ya kijana. Aibu kubwa sana kuwa mtumwa wa mawazo. Shenzy zao hao wazazi.
Hata boarding za Tanzania watoto wanafanyana wakubwa kuwafanya wadogo labda huajwahi kumbana na hizi kesi, hii ni story tu ulosikia ila hata humo majumbani wajomba na wageni wanaume wanaokaribishwa hulazwa na watoto na pia huwaaribu n.k...hi ni ajali kama ajali nyengine ilomkumba kijana ....SHENZI ZAO POLISI WA SOUTH NA WALIMU, PAMOJA NA SHULE.
 
Ugenini ni ugenini tuu angekuwa hapahapa hayo yasingemkuta
Angalisho! Ukiwa nje YA Nchi kimasomo kimaisha kikazi, Tuepuke maandamano migomo etc yana hatari kama hizi.
 
Ni kijana aliyetokea kwenye familia yenye uwezo kiasi, wazazi wake walijitahidi kuhakikisha mwanao anapata elimu iliyobora wakaamua kumpeleka South Africa Johannesburg mtoto alisoma huko kuanzia primary mpaka Sec School.

Akiwa form 2 kuna maandamano na vurugu yalitokea shuleni kwao yakihusisha wanafunzi wote wakipinga maswala ya chakula kuwa si kizuri.Maandamano yale yalipelekea polisi kufika shuleni pale na kuwakamata baadhi ya wanafunzi akiwa ni pamoja na huyo kijana waki Tz.

Walipofikishwa pale polisi wanafunzi wengine wazazi wao walifika pale na kuwatoa watoto wao kwa dhamana maana wengi wao walikuwa ni wazawa wa huko akabaki yule wa kitanzania.

Ilipofika usiku mtoto yule akiwa amechanganywa na wahalifu wengine.Mhalifu mmoja akamwita ili alale nae na akawa kama anamsaidia maana wahalifu wengi walikuwa wakimsakama sakama kijana yule.

Kijana yule akaamini muhalifu yule aliemwita ndiyo atakae msaidia akienda akawa amelala karibu yake.Ilipofika usiku wa manane muhalifu yule akaanza kumvua yule kijana suruali kijana akapambana nae huku akipiga kelele bila msaada wowote akavuliwa suruali na yule mhalifu akamwingilia kinyume na maumbile.Kesho yake akaenda kushtaki kwa askari lakini hata hakusikilizwa.

Ikawa mchana ikawa usiku tena yule mhalifu akamwingilia tena.Mhalifu yule ndiye alikuwa kama kiongozi kwenye chumba kile waliopo kwahiyo akawa anajifanya kumsaidia yule kijana kupata chakula kizuri na kwa wakati.

Basi kijana alikaa wiki pale na kila usiku akawa anaingiliwa hivyo hivyo bila msaada wowote.Baada ya week mama yake akawa ameshafika akitokea Tz akaruhusiwa kumdhamini mtoto wake.

Ila akaona afya ya mtoto imedhoofu sana mama yule alilia kwa uchungu mno akamchukua mwanae na kurudi nae Tz kijana yule alizidi kudhoofu afya sana.Mama akakaa na mtoto wake akamuuliza kwanini mbona huna raha una mawazo mno.Mtoto ndiyo akamwadithia mama ake kisa kilichomkuta akiwa mahabusu kule South Africa.

Mama alilia mno akamwambia baba mzazi wa mtoto baba aliumia mno.Wakampeleka hospital wakakuta ni kweli mtoto aliingiliwa na akakutwa yuko na ugonjwa wa fungus akatibiwa na akapima UKIMWI akakutwa hana.

Ila ilipofika miezi kama 4 hivi akaenda kupima tena akakutwa aliambukizwa HIV na mpaka sasa anaendelea kutumia dawa hizo, ila kijana ni mtu wa kulia tu hana raha kabisa.
isee tufanyeni usela wote ila jela hapafai isee,
 
Sisi binadamu tunapitia mitihani sana hapa dunian.. Ila mkasa huu kama ni wa kweli huyo kijana amepitia magumu zaidi. Mungu ampe faraja ya maisha asikate tamaa. Anawesa kuishi umri mrefu zaidi kuliko hata mtu asiye na maambukizi
 
Maisha ni kama mtihani,kila mtu ana maswali yake,hakuna kuangalizia na kila mtu atajibu maswali yake!Pole sana Mungu ataleta wepesi

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
somesheni watoto wenu hapa nchni mbona kuna shule nzuri tu za international kwann umpeleke mwanao nchi ya mbali kwa kuwa unayo hela tu...hayo ndo madhara yake, pole yake ila tujifunze.
 
Back
Top Bottom