Kiini macho cha Kamati ya January Makamba na Dowans


what makes it being crap?
Unataka mpaka CDM wakisema ndio manakubali?
tunapingana kwa hoja sio chuki binafisi zisizoweza kujenga nchi yetu
Unaweza kunyea kambi wewe? Usilaumu tu ndugu. Hata Salva akitoka ikulu usishangae akaigeuka

 
ntajiua akigombea:bump::msela::hungry:

Kiduku؛‎ unataka kuniliza mapema, uwe mwangalifu. Kumbuka Sugu yu bungeni licha ya viapo vya watangazaji wa radio maarufu. Kumbuka ukoo huo hauna hiana maana kama wangekuwa wanajitazama basi ccm ingekuwa na katibu. Kwa faida yako tu angalia hili: katibu mkuu wa chama-Baba, katibu mwenezi-kaka, mfadhiri mkuu wa miradi ya maendeleo ya wananchi jimboni-dada................ Kwa nini lolote lisiwezekane?!
 
Mbwa mwitu kuvaa ngozi ya kondoo. Amekuwepo Ikulu na yote yaliyokuwa yanafanyika alikuwa anayaona na kuyajua, leo anaibuka na hayo, mbona alipogombea ubunge hakuongelea hayo, sasa upepo unawageukia ndio unaona wanaanza kuhaha.

Kumbukeni hotupa ya Kikwete kule dodoma juzi alivyosema wanageuka sasa kuanza kuambaa kama nyoka ili kujenga upya chama. Hii ni janja na mbinu yao kuteka hoja ya Chadema.
 

Huyu Mhesimiwa Makamba si alikuwa ikulu, yote si aliyaona, ua anatupiga changa la macho?????????????????? Ashinikize kura ya kutokuwa na imani na swahiba wake basi, apambane na mwenye mali asimuue mtumwa bure!!!
 
..tatizo lugha aliyotumia ni ya KUBEMBELEZA.

..hivi January anataka tuamini kwamba hajui kuwa JK ndiye mhusika mkuu wa Dowans?

..hiyo barua yake inalenga ktk kuwabebesha mzigo wa lawama watu wasiohusika, na kuwasafisha wanaohusika
 
Hivi Seacliff haya uliyatoa wapi??
Interesting....eeh
 
Hoja nzito kutoka kwa upinzani tu ndio zinazojadiliwa humu ndani. Ingawa huyu kijana wa Makamba kasema kwamba tumewalipia IPTL 20 Million USD kwa mwaka bila hata kuproduce umeme kwa sekunde moja, lakini great thinkers hawataki kujadili hoja, ila mtoa hoja. Amongst other things.

This is some place.
 

Ukiumwa na nyoka hata ukiona kamba unashtuka. Wengi hatuamini labda kuna mchezo nyuma yake kama ilivyo CCM! Ni nyoka kubadili magamba .....Kikwete Feb 5 2011 DODOMA
 

Selemani,

..huyo kijana wa Makamba anapenda kuandika-andika.

..if he really means business aitishe press conference na kuwatoa nishai makada wenzake wa chama.

..halafu barua yenyewe kaandika kwa lugha ya KUBEMBELEZA utafikiri anamuandikia ...
 
Mimi akili yangu inanipeleka kuamini kwamba hii ni mbinu madhubuti ambayo inataka kutumika kushusha habari mbaya kwa wananchi na watu wengine kubebeshwa mzigo. Haikai kabisa akilini. Ila lazima nikubali kama ipo kama ambavyo nahisi basi wameamua geuza hili suala zima kuwa kama mchezo wa 'Chess'.

All in all it is a very smart move ambayo mwisho wa siku itatufanya Watanzania wa chini kama mimi na wewe tubaki tunalaumiana wenyewe... Jambo la msingi zaidi hapa ilikuwa ni watendaji waliovurunda kuwajibishwa kabla ya mambo mengine. Naungana na Ng'wanangwa kusema hii ni 'real smart crap.'
 
what makes it being crap?
Unataka mpaka CDM wakisema ndio manakubali?
tunapingana kwa hoja sio chuki binafisi zisizoweza kujenga nchi yetu

kwel uyasemayo,lakini kwa hali ilivo sasa inakuwa ngumu kuwaamin wabunge wa chama tawala na watendaj wake,c umeona uvccm walivyosh2kiwa?binafsi naona hakutakuwa na jipya,january makamba anapayuka tu,kwni ni nani alosaini IPTL?kwani sakata la dowanz halielewek?rais anajua kuwa richmond waz a ghost but leo anakubali dowanz,so ngeleja afanyeje?kumpelekea barua ndo kutafanyaje?mi nilipoisoma hbr ya january,nikaona ni porojo tu,tambua kuwa hakuna mbunge atakaeikosoa au kuihoj serikali toka chama tawala,weng wataunga mkono hoja kabla ya kuchangia kwa % zote,waikosoe wakose ulaji?
 

Selemeni, na wewe upo hapa; jadili au unataka kina nani wajadili? Maana wengine wakianza kujadili haichelewi kuonekana wanapinga tu! Kama unaona kuna hoja ijadili, ichambue, iongeze nguvu n.k Usisubiri wengine hapa kufanya hivyo...
 
We have attached Mr. Makamba's letter in the original posting.
 
Wanjaribu kuondoa attension yetu kwenye mambo mengine..........Hakuna lolote.........like father like son
 
Nimeisoma barua nzima na kuipitia kwa makini nina mambo mawili tu ya kusema "nice try" na la pili "try again". I'm impressed though na jaribio lenyewe lilivyo. Sidhani kama kuna lolote ambalo limesemwa ambalo lilikuwa halijulikani tayari. Ninachojaribu kutafutia majibu ni kuelewa tu:

a. Kwanini amemuandikiwa Waziri kutaka maelezo tu (fungu la mwisho la barua linatoa jibu) ila nimejiuliza tu tena.

b. Kwanini anafikiri jukumu lake kama mbunge ni kushauri na "kuomba" serikali?

c. Hajaeleza yeye mwenyewe hisia zake kuhusu masuala hayo ziko vipi; kwa mfano serikali ikitoa maelezo ya kina ya majibu yake na wananchi wakajua then what? kwa mfano serikali ikianza kuzungumza kwa kauli moja (wasipopingana) itakuwa imeondoa tatizo lake la serikali kugongana katika kutoa misimamo?

d. Maswali ambayo hakutaka kuyauliza: uhalali wa Dowans na malipo yake, uhalali wa mkataba wa Dowans, uongozi wa serikali katika suala zima; maana inaonekana kama analaumu serikali kutengeneza "perception" ya kutokuweza. Kwamba majibu ya serikali kwa barua hiyo yatasaidia kuwaelewesha Watanzania juu ya nini kinachoendelea. Kama mwandishi anavyosema:


Naamini angeweza kwenda mbali (labda anapanga kwenda mbali huko mbele) lakini barua haitudokezi hilo. Nice try, but try again buddy! One can not be blamed for attempting..
 
Mh. January Makamba, kwenye hili nakupa kudos bila kujali dhamira yako ni ipi au mchezo gani unachezwa. Kwa ufupi umemtaka Ngeleja aeleze bungeni huu upumbavu wa mgao utaisha lini TZ?? Kwa nini kugenerate extra 500MW inakuwa kama ni suala gumu wakati ni kitu kiko ndani ya uwezo wa serikali??

Ngeleja akieleza bungeni itawapa wabunge nafasi ya kumhoji na kutoa mapendekezo ya nini kifanyike.

Issue kubwa TZ ni kuondoa MGAO PERIOD. Lazima tununue mitambo ya gas 250MW Wartsila na 250MW GE, mwaka huu 2011 ili itakapokuja online by say mid 2012, tuwe na miaka angalau 10 ijayo bila kudeal na mgao.

At the same time hoja za kutolipa dowans nk nazo ziendelee, lakini mgao lazima iwe history TZ in the next 12 months otherwise serikali na sisi wananchi wote tuitwe WAJINGA na tuwe proud na ujinga wetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…