Kiingereza Cha Mama Anna Makinda.....

Ukishajua Kiingereza Unapata Nini? Sasa Wewe unajua Hicho Kiingerereza ila Huna Hadhi Kama Ya Mama Makinda na Utakufa na Umasikini Wako Huo Huo Pamoja na Kiingereza Chako hicho. Halafu Mbona Wanaokijua Huwa Hawashoboki na Wala Huwa Hawapendi Kujionyesha Kama Wanakijua na Wanakiongeza Isipokuwa tu Pale Inapobidi? Ndio Tatizo Ukizaliwa ktk Ukata na Siku Ukizibahatisha tu Nyodo Nyingi Mitaani. Mwacheni Mama wa Watu na Isitoshe Tunamwelewa Mno tu Akiwa Anazungumza ila Huwa Napenda Sana Mfano wa Mama ASHA ROSE MTENGETI MIGIRO Kwa Kupenda Sana Kuzungumza na Kukisifia KISWAHILI chetu Wakati ni Mzungumzaji Mzuri Sana Wa Kiingereza Pale Inapobidi tu ila Hakitukuzi Hicho Kiingereza Chenu. Mmekuwa Wepesi Sana Kuwashambulia Viongozi Kuwa Hawajui Kiingereza Wakati Usishangae hata Wewe Mwenyewe Hujui Kuongea Vizuri Kiingereza na Hata Wazazi Wako au Ukoo Wako Wote Nao Hawajui bali ni Wewe tu Ndiyo Umeona Mwezi na Umetoa Tongotongo. Mnaudhi na Ndiyo Maana Nawapaka na Mkinichukia Shauri Yenu Washamba Wakubwa.
Nakumbuka kuna siku hapa UK uliandaliwa mkutano wa watainzania waishio huku na wahutubiaji waliokuwa viongozi wa chama cha watanzania wakati huo

Kikao kilihudhuriwa na watanzania watupu kasoro fundi mitambo tu ndio alikuwa mhindi.

Basi hapo ilikuwa kama mashindano ya watoto kuongea kiingereza, kila aliepanda jukwaani alikuwa anashuhsa ung'eng'e wa kila aina. lakini mwisho wake hakuna lolote la maana waliloongea. Mimi nilisimama na kuuliza swali kiswahili wakanicheka sana, lakini jiulize, hao hapa UK wanafanya kazi gani?
 
Badala ya kuwa proud na lugha yako ya taifa unauliza kama wengine wanajua kuongea lugha za watu.

Anyway, uliwahi kusikia wazungu wakishindana kuongea kiswahili?

Wazungu hawahitaji kujua kiswahili lakini sisi tunahitaji kujua kiingereza. Hivi huko uliko huwa ukienda kubeba hayo mabox unaongea kiswahili au kiingereza?
 
Asnan Murji darasa la 7-he is zero!! Bt good in business making

Hata Bill Gates wasn't good in class but in business is fantastic! Murji ni form four na sio darasa la Saba lakini kwa akili ya biashara hakuna anayempata katika mikoa ya Lindi na Mtwara!
 
Na watu wanaongoza kuongea kiingereza kibovu ni vijana Pro Chadema! Yaani wakiongea utadhani ni darasa la pili wa Karume Primary school!
 
Sijui kwanini ikija mada ya kidhungu watu wanajifanya wazalendo.....ni uoga wa kujifunza ama vipi?...nawaza tu kwa maandishi...

Uko sawa mkuu, yani kizungu kikitajwa tu utasikia
'Kiswahili lugha ya mtz halisi..mi mzalendo..lugha za wakoloni ha ha haaa hatukosi excuse
 
Ungenge wito, siku bunge likiamua kutumia ngeli kama lugha ya mijadala basi kuna waheshimiwa watamaliza miaka mitano bila kuchangia. na wengine kuachana na siasa kabisa.
Kwani kutokujua kiingereza ndio umbulula?We kama unakijua hicho ulichokiandika kwa kiswahili hapo kitafswiri kithungu tuone kama hujaweka present tense na future tense pamoja.
 
Waraka wa Zitto na wenzake unasema...''Elimu ya mwenyekiti ni ya magumashi, hana vision na hana uwezo wa kujieleleza'' ....Tundu Lissu.
mambo ya kutambiana Elimu mimi nilishakoma kabisa, wewe kama unaona una ka-elimu basi ka chini tulia, maana kuna watu wana vyeti lukuki hadi maPHD ila kichwani ni matikiti maji tena yale ya kimbiji.
 
Kwani kutokujua kiingereza ndio umbulula?We kama unakijua hicho ulichokiandika kwa kiswahili hapo kitafswiri kithungu tuone kama hujaweka present tense na future tense pamoja.
mimi sijui kithungu, la nakwambia hata matusi yataisha bungeni!! watu watakuwa mabubu kuanzia spika hadi baadhi ya waheshimiwa!! Mfano hebu mwambie Jamaa arudie lile tusi lake la juzi juzi kwa ungenge.

"Siongei na mbwa naongea na mwenye mbwa"
 
Hata likuvi na mulugo ndo walewale... Hahahaa.. Hao ndo viongozi wetu bana
 
Napata taabu sana kuelewa kiingereza anacho ongea mama Makinda au sijui ni kwa sababu kiko deep sana ama kinasound kibantu zaidi?.....yote tisa kumi ni kwamba sijawahi kuwasikia mh Mkuchika,Asnain Murji, Shibuda Anna Abdala wakiongea kizungu hongereni kwa kukienzi kiswahili.
Wewe komaa na kiingereza ujue mwenzio anaingiza salio na ulinzi wa kutosha.
 
Itakua ana mix na kibena kiaina..

Hahaaaahaaaaahaaaa kwikwkiwi! eeh nye wabungezi naombazi mtuliezi please, beee!

wanafichamia kwenye kukienzi kiswahili but deep down in their stomach they know that speaking English even for minute makes them stammer and want to cry! mi hapa nipo na dictionary hadi kuandika hivi. CL nouma!
 

Similar Discussions

5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom