Kigwangalla ana hoja. Zijibiwe

technically

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
11,975
48,843
Sometimes wabongo sisi ni wapumbavu sana kwenye kuhoji maslahi.

Kigwangalla ana hoja za msingi sana, Mo anaishije na timu anayoimiliki kwa 49% bila kulipa cost za hisa?

Yaani bilion 20 hajalipa hata mia halafu mnasema aachwe tu atumie club kama anavyotaka.

Siku akiondoka timu ianze kutembeza bakuli?

Uwanja wa mazoezi kajenga, je unaitwa Simba kwanini uwe na jina lake na sio la club.

Washabiki wa Simba acheni kuwa wapumbavu timu inatumiwa kisiasa, timu inatangaza biashara za mtu asiye na hisa kihalali?

Simba mjitafakari, Kigwangalla anazo hoja za msingi.
 
Kigwangala ana hoja za msingi sana Mo anaishije na timu anayoimiliki kwa 49% bila kulipa cost za hisa?....
Kwan sportpesa Simba inaingiza kiasi gani ili tujue matangazo ya sportpesa na ya Mo yapi yanatija kwa Simba
 
Kama umejiita "mpumbavu" uko sahihi kabisa.Ila si watanzania wote ni wapumbavu kama wewe

Mchakato bado unaendelea,Mo alipe 20B wapi?Kwa ajili ya nini?

Alipe Simba sports club au alipe Simba company limited.

Akilipa Simba sports club,ni nani atamuhakikishia usalama wa pesa hizo.Maana hadi mchakato uje kukamilika,unaweza kuta akaunti haina pesa ,hakuna kiwanja,na hata ukakuta hata makombe hakuna,ila unaachiwa mahesabu tu.Tunajuana sana sisi wabongo.

Hoja kwamba Mo amepata wapi nguvu ya kuajiri msaidizi wake kuwa CEO ni hoja dhaifu kwani haina ukweli wowote. Kuwa msaidizi wa Mo au hata kama angekuwa mwanae,anaweza kuajiriwa tu kwa uwezo wake.

Mwisho niseme huu uswahili tunafahamu madhara yake.Na huwa unaonekana tu pale kunapokuwa na dalili ya mafanikio.Wakati Simba ina matatizo,hakuna mtu katika hao wanaojitokeza sasa,wanaotoa hata maji tu kwa wachezaji.

Pole sana kwa kujiona mtanzania mpumbavu kama ulivyojiita hapo juu.Tupo tusio wapumbavu na tunajua janja janja ya manyang'au kama wewe na wenzio mbaozitamani mali za mwanaume
Sometimes wabongo sisi ni wapumbavu sana kwenye kuhoji maslahi.

Kigwangalla ana hoja za msingi sana, Mo anaishije na timu anayoimiliki kwa 49% bila kulipa cost za hisa?

Yaani bilion 20 hajalipa hata mia halafu mnasema aachwe tu atumie club kama anavyotaka.

Siku akiondoka timu ianze kutembeza bakuli?

Uwanja wa mazoezi kajenga, je unaitwa Simba kwanini uwe na jina lake na sio la club.

Washabiki wa Simba acheni kuwa wapumbavu timu inatumiwa kisiasa, timu inatangaza biashara za mtu asiye na hisa kihalali?

Simba mjitafakari, Kigwangalla anazo hoja za msingi.
 
Hizi habari za kutuambia fuatilia interview yangu ni udhaibu na inaonyesha kuna mapungufu ambayo yapo yaliyofichwa, mtu ajibu maswali ayaweke wazi hakuna anyechoka kusikia ukweli na kujua nini kinachoendelea
 
Sometimes wabongo sisi ni wapumbavu sana kwenye kuhoji maslahi.

Kigwangalla ana hoja za msingi sana, Mo anaishije na timu anayoimiliki kwa 49% bila kulipa cost za hisa?

Yaani bilion 20 hajalipa hata mia halafu mnasema aachwe tu atumie club kama anavyotaka.

Siku akiondoka timu ianze kutembeza bakuli?

Uwanja wa mazoezi kajenga, je unaitwa Simba kwanini uwe na jina lake na sio la club.

Washabiki wa Simba acheni kuwa wapumbavu timu inatumiwa kisiasa, timu inatangaza biashara za mtu asiye na hisa kihalali?

Simba mjitafakari, Kigwangalla anazo hoja za msingi.
Bodaboda alipata vle?
 
Kweli akili ni mali inakuaje Mo aseme anatumia B3 kwa mwaka kuihudumia timu na mashabiki wanashangilia tu bila hata kuuliza je wadhamini wa simba wanatoa kiasi je viingilio kwa mwaka ni kiasi chukua mapato ya simba toa matumizi tuone deficit yake ni ngapi otherwise atwambie matumizi ya simba ni zaidi ya b5 yule ni mfanyabiashara hawezi kutoa kiasi hicho bila faida Kigwa ana hoja hata mkimpuuza
 
Hata ka biashara ka kuuza karanga hauna. Nani atakuelewa
 
Hamis yupo sahihi
Hamisi hili tatizo kaliona baada ya kunyimwa alichoomba? Huyu Kigwa ana roho mbaya sana na ana chuki ya muda mrefu, sitosahau alichomfanyia J.J. Mwaka kipindi akiwa Afya, yeye kaisaidia nini Simba? Si kwamba namtetea Mo ila Kigwa anafanya kila kitu kulipiza kisasi kupitia kwa wanachama na wapenzi wa Simba wa wasiomjua Kigwa watamuunga mkono
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom