kibogo
JF-Expert Member
- Apr 1, 2012
- 9,739
- 4,746
Mh. Kigwangala na Mbunge Mwenzako wa Bukene katika Ziara ya Mh. Rais mlipaza sauti juu ya watendaji wa Serikali Mkurugenzi na Mhandisi wa Maji wa Wilaya kuwa ni watendaji wabovu na mlitaka viongozi hao waondoke na hao watendaji. Kwa kukurupuka walitekeleza matakwa yenu.
- Mkurugenzi aliondolewa na kupewa kazi nyingine Mkoani
- Mhandisi pia aliondolewa kwa ahadi ya waziri husika kuwa anaondoka nae
Sasa napenda kuuliza Waziri wa maji alihaidi ndani ya wiki moja atakuwa ametekeleza yale mliyosema ni mapungufu ya huyo mhandisi, je yametekelezwa hadi sasa?
- Majibu mnayo kuwa hakuna kilichotekelezwa kama mlivyohaidiwa hadi sasa kwa maana hiyo mlichokiongea na kusababishia watumishi hao kuondolewa mlikuwa mnajua kabisa sio makosa ya watumishi hao bali ni makosa ya serikali, ilikuwaje mkaongea hayo.
- Kutokana na yaliyotokea mmechangia matumizi ya fedha yasiyo ya lazima kwa gharama za kuhamisha hawa watumishi na gharama za kuleta hao wengine.
- Ushauli wangu kwa wanasiasa tusiwe na hoja kama za akina Kigwangala ambazo hazina tija kwa maendeleo ila ni kufanya siasa nyepezi zilizopitwa na wakati pia kwa viongozi wa juu kuchukua hatua kwa kutumia maneno ya kwenye mikutano ya hadhala ni udhaifu kiutendaji.