Kigoma Yazizima kumlaki Dr Slaa

Kigoma Yazizima kumlaki Dr Slaa

Hawana ujanja Mungi ni lazima daftari liboreshwe!

Molemo, kuna post yangu wanaitoa ma mods sijui kwa nini. napendekeza Dr slaa aandaliwe mapokezi makubwa Dar es salaam akiwa anatokea Kigoma, ili kumpongeza kwa ujasiri na ukomavu wa hali ya juu aliouonyesha dhidi wa manyang'au, wasaliti, wachumia tumbo na MaCCM wote
 
Dr.Slaa anaomba aridhi ipasuke aingie,ziara yake mdebwedo na kajishushia heshma yake sana,Ukanda mbaya!!!
 
Watu wameshawasili uwanjani hapa Community Centre mjini Kigoma kwa ajili ya ujio wa Gwiji wa Siasa Tanzania na Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr Wilbroad Slaa.

Wengine tayari wameshaanza kuchukua nafasi zao. Ngoma inachezwa hapa kama maandalizi ya kumpokea Katibu Mkuu Dkt. Slaa.

Manji wa ngoma hii anaitwa Mapigo Saba, ambaye anajinasibu kuwa ana miaka 61, anazidi kuwahanikiza watu waendelee kujongea hapa.

Anasema vijana makini, wazee makini na akina mama makini wako CHADEMA. Watu wanamsubiri kwa hamu mgeni wao!

Updates 1.....

Kila kitu kiko sawasawa hapa, mathalani kuna jenereta la dharura kama umeme utakatika.

Red brigade wako imara karibu kila kona ya uwanja huu kuhakikisha ulinzi uko sawasawa. Kuna stori inatafutwa na kuandaliwa nje ya uwanja hapa.

Wanahabari tumeshanyaka mpango mzima unaoandaliwa maana inavyoonekana huku ndani mipango yao hawataweza kufanikisha kwa sababu ya uimara wa ulinzi wa Red Brigade na usalama wa Chadema.

Kuna waandishi wa magazeti ya...wameshaandaliwa na tayari wamepelekwa hapo nje ambapo kuna kitu kinaandaliwa.

Update 2....

Watu wametulia kbs hapa Uwanjani, wakiendelea kumsubiri kwa hamu mgeni wao. Watu wanazidi kumiminika uwanjani.

MC anaendelea kuwasisitiza wananchi wengi walioko pembeni mwa uwanja waungane na wenzao wengi pia walioko mbele ya jukwaa.

MC anaomba wimbo wa ''SLAA ANAWEZA''. Anasema huo wimbo unakubalika sana Kigoma anasema kuna siku kwenye harusi moja, Bwana Harusi aliwashangaza waalikwa alipoomba wimbo huo kwa ajili ya kutokea ukumbini.

Anasema maudhui yake ni murua na leo mtu mwenyewe yuko hapa. Waliyempigia kura za kutosha mwaka 2010 kwa sababu wanamuamini na wanaamini katika chama chao, CHADEMA.

Updates 3....

Dkt. Slaa ameingia uwanjani tayari wananchi waliokuwa pembeni na nje ya uwanja, wanakimbilia karibu na jukwaa kumuona na kumsikiliza Katibu Mkuu huku uwanja ukilipuka kwa shangwe kuu.

Kikundi cha Mapigo Saba kinaitwa kwa ajili ya kuimba wimbo maalum kwa ajili ya mgeni rasmi.

Mkiti Mwalimu Adam anachukua mic kufungua mkutano. Katibu Mkuu ameshaketi jukwaani tayari. Anazungumza mawili matatu na Mkiti wa Kanda ya Magharibi, Mohamed Mambo. Tayari mkutano umefunguliwa watu wanashangilia hapa.

Mapigo saba anasema wana nyimbo 2 kwa ajili ya Dkt. Slaa. Anasema Chadema Kigoma kuna amani.

Mratibu wa ziara, Mwita Waitara Mwikabe anachukua nafasi yake kuendesha itifaki ya mkutano. Sasa wanatambulishwa madiwani wa CHADEMA hapa.

Diwani wa Uvinza anawafurahisha watu kwa kusema CHADEMA ni mpango Mungu, tunasonga mbele, hakuna kurudi nyuma. Watu wanashangilia hapa.

Sasa anapanda Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kigoma Ujiji anatoa taarifa namna CHADEMA kupitia Halmashauri yake inasimamia shughuli ya maendeleo.

Viongozi wa chama wanaendelea kujitambulisha. Leo kuna kikao cha Baraza la Mashauriano la mkoa, hivyo kuna viongozi wengi, baada ya Katibu wa Mkoa, Msafiri Wamalwa sasa kapanda Katibu wa Kanda ya Magharibi, Christopher Nyawanji.

Anatambulisha wasaidizi wake kwenye ofc ya kanda. Sasa Waitara anatoa taarifa fupi ya ziara tangu ianze Dec 4.

Updates 4.....

Sasa baada ya Mkiti wa Kanda, amepanda Katibu Mkuu Dr Slaa ambaye anashangiliwa mpaka inakuwa shida kusikilizana. Ameanza kwa kutoa dakika moja ya kukaa kimya, kwa sababu ya misiba iliyotokea kwa viongozi wawili wa CHADEMA Mkoa.

Updates 5....

Katibu Mkuu, Dkt. Slaa, ambaye amemaliza mkutano punde, amewaacha wananchi na hamu ya kuendelea kumsikiliza wakati akishusha nondo za mahesabu ya ruzuku na mapato mengine ya chama.

Sasa anaelekea kwenye kikao cha ndani, Baraza la Mashauriano la Mkoa.

Umati umetanda kila kona pembeni ya barabara wakimshangilia Dr Slaa na kusema CHADEMA ndiyo mkombozi wa Kigoma na Tanzania.Dr Slaa naye anashusha vioo vya gari na kupunga mikono kwa furaha kama heshima kwa wana Kigoma kwa mapokezi makubwa sana waliyompatia!!

Umati uliofurika kumsikiliza Dr Slaa mjini Kigoma leo:

attachment.php


Source:Afisa Habari Mkuu CHADEMA Tumaini Makene[/QUOTE]
Safi sana maana zito na maccm walifikiri kuwa kwa kuvuliva nyadhifa wafuasi wa chadema wangesusia mikutano aibu imewapata
 
Last edited by a moderator:
Molemo, kuna post yangu wanaitoa ma mods sijui kwa nini. napendekeza Dr slaa aandaliwe mapokezi makubwa Dar es salaam akiwa anatokea Kigoma, ili kumpongeza kwa ujasiri na ukomavu wa hali ya juu aliouonyesha dhidi wa manyang'au, wasaliti, wachumia tumbo na MaCCM wote

Ushauri mzuri sana Kamanda.

Dr Slaa ni Simba wa Vita Tanzania na ameivuruga vibaya sana CCM Kigoma.

Wale wavuta bangi waliotafutwa na Waasi kuvuruga ziara ya Dr Slaa Kigoma wamepotea kabisa kutokana na msimamo mkali wa wanaKigoma dhidi ya Waasi na Wasaliti.
 
Ushauri mzuri sana Kamanda.

Dr Slaa ni Simba wa Vita Tanzania na ameivuruga vibaya sana CCM Kigoma.

Wale wavuta bangi waliotafutwa na Waasi kuvuruga ziara ya Dr Slaa Kigoma wamepotea kabisa kutokana na msimamo mkali wa wanaKigoma dhidi ya Waasi na Wasaliti.

hakuna wa kumsimamisha Dr Slaa Tanzania hii, Zitto mwenyewe hilo analitambua kuwa kile ni kichwa
 
Ngoja tusubiri ziara ya zito huko ndo tutaona kati ya slaa na zito nani anavuta watu wengi hapo.

Kutoka mapovu ya "Slaa hatakiwi Kigoma" mpaka sasa mmekuja na single nyingine,kubalini tu kuwa mmeshindwa kuhujumu ziara ya Dr Slaa.Jipangeni upya!
 
Hao waha nao watakuwa mambumbu kama watakubaliana na propoganda za Slaa, wakati wanajua kama anaandaa uongozi kwa ajili ya wana kaskazini!

Acha ujinga wewe. Upumbavu wako usikufanye ukajiona una akili hadi kuwaita waha mbumbumbu. Chadema ilianza kustawi Kigoma kabla ya maeneo mengine, na hiki ndicho kinachowauma. Kama waha ni mbumbumbu vipi Zito mmuone wa maana na mwenye akili? Jitahidi kuepuka kuutangaza ujinga wako kwa jamii.
 
Hapo dr Slaa kachemsha huo ndio umati mkubwa wakumpokea kiongozi mkubwa kama yeye rais mtarajiwa???
 
Siku hizi neno 'umati' limepata tafsiri nyingine sio ile inayofahamika! Siasa bhana!
 
Kuna mtu anaitwa TASWIRA ni muongo haijapata kutokea toka kuanzishwa JF jamaa ana mabreaking news ya uongo uongo hadi anatia kinyaa!
 
Kuna msemo unasema wali wakushiba unauona kwenye sahani Magamba mmeona uyo ndio Dr slaa wa ukweli.
 
Jamani CDM Kigoma hamna chenu huo ndio umati mkubwa? Hizi siasa za maji taka za akina Molemo hizi zinaiua CDM kabisa!

Everything in chadema is fake, Dr Slaa is fake, his PHD is also fake, his wife is fake, his belief is fake, worse enough his party is even worse!
 
Kigomaa ahe kigoma mama we leka dutigite tunayofuraha ya kumwona Slaa, Chadema tunaikubali chadema tunaipenda
 
Tunamsubiri Singida aone Kama atapata watu na kwa taarifa amekacha kufanya Ziara Kiomboi! Nasikia anafanya wilaya zingine sio Iramba! Maana Mkumbo ni wa Huku na wanyiramba anawajua!
 
Chadema hakuna jipya! Kama uchaguzi ungefanyika Leo hata 5% ya kura za Urais asingepata!
 
Back
Top Bottom