Kigoma yaanza kufunguka

Watu mna maneno!
 
Binafsi maendeleo ya miundombinu nayaona manispaa ya kigoma tu, huko kwingine (wilayani) bado sana.
 
Hivi Maruzuku Khamisi, aliacha warithi wa kuendesha biashara yake ya usafiri?
Maruzuku Khamis alikuwa kati ya matajiri kanda ya ziwa, akishindana na mwarabu mmoja aliyeitwa Shariff Mohamed na kaka zake.
 
Naam tutakuwa na mapepo kabisa
 
Utakuwa unatoka ujiji bilashaka
 
Fedha inayotolewa ni kidogo sana,serikali hainaga utaratibu wa kutoa pesa yote kwa pamoja kwa miradi mikubwa badala yake huwa inatolewa kila mwaka hadi project inaisha labda iwe mkopo ndio pesa inaweza kuwa yote ipo
Hayo ya tender waulize Tanroads na wizara
 
Pongezi hapana, hayo yote tuliyastahili lakini maksudi viongozi wakatufanyia mtima nyongo
Japo mama alikuwa na wajibu wake wa kukupikia na kuhakikisha kuwa umekula lakini tulifundishwa kusema asante kwa chakula. Kupongeza na kushukuru ni tabia njema na haidhuru hata kama ulistahili kufanyiwa... Je, ni mara ngapi umejisikia vizuri ulivyopongezwa kwa jambo ambalo lilikuwa ni waljibu wako kulitenda, kwa mfano kufaulu masomo darasani..
 
Kilichoandikwa ni Ukweli serikali kuanzia ya Kikwete ilianza kuonyesha kigoma ni sehemu ya Tanzania.Nililala Siku mbili kigoma na nikagundua kigoma kuna chakula kingi na bei chini kushinda Mbeya nilipopazoea bidhaa nusu bei Kigoma ni Robo bei. Tatizo ukienda kigoma kuna beria ni nyingi sana
 
Tanzania yote ina haki ya kuwa na maendeleo.

Nilimuelewa JPM alipoweka mkazo wa kuhamia Dodoma. Anatenganisha serikali na wafanyabiashara.

Pia anaiweka serikali mahali inapoweza kufikiwa na kila mtanzania.
 
Kila sehemu unakutana na askari wa uhamiaji, unaulizwa kitambulisho mpaka kero
 
Barabara ya Simbo Ilagala mpaka Kalema Rukwa ni ya muhimu sana kwa uchumi wa watu wa kusini lakini haizungumziwi popote na wabunge wote wawili wa eneo hili nikama hawapo.
 
Kanyonza Vs kibonge. Barabara ya nyakanazi ina zaidi ya miaka kumi haiishagi na mkandarasi Nyanzaroad yuko site anakumbatiwa tu.
2014 gari ikifika nyakanazi from KGM gari zima vumbi tupu..
Watu wanadhambi kweli hadi Leo haijaisha!
 
Barabara ya Simbo Ilagala mpaka Kalema Rukwa ni ya muhimu sana kwa uchumi wa watu wa kusini lakini haizungumziwi popote na wabunge wote wawili wa eneo hili nikama hawapo.
Siku hizi Kalema ni Katavi sio Rukwa tena kama zamani
 
Visasi vyaweza kuwepo iwapo kuna watu wanaona kazi unayofanya ni ya hovyo!!inatia hasira.ndo maana Mungu aliamua kumfukuza Shetani na malaika zake kwa kosa LA kuanza kuona kazi na sheria za Mungu ni za hovyo! Watu wa hovyo ni mbora wasiwepo
"---watu wa hovyo". Ni akina nani hawa!
Nani ana mamlaka ya kuhukumu na kuwaweka pembeni hawa 'watu wa hovyo'; mwenye madaraka (vyombo vya dola, au wananchi wenye uwezo wa kuamua nani awe kiongozi wao?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…