Kigoma, Uvinza: Wananchi waua Askari wa akiba 3 waliodaiwa kutaka kufanya unyang'anyi wa ng'ombe

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989
Tukio kubwa limeripotiwa kutokea mkoani Kigoma, Wilaya ya Uvinza ambapo Askari wanne wameuawa kwa sababu walitaka kuwanyanganya ng’ombe wafugaji wa jamii ya kisukuma kwenye msitu wa Kagera, Nkanda.

Askari hao wanadaiwa kumpiga risasi mchungaji baada ya kuwagomea wasichukue ng'ombe na wafugaji hao waliposikia kuuliwa kwa mchungaji walienda na zana za jadi wakaua askari watatu na Afisa Misitu mmoja.

Mpaka sasa wananchi zaidi ya 40 wamekamatwa na wengine wanaendelea kusakwa huku vyombo vingi vya habari vikizuiliwa kuripoti suala hilo.

Taarifa zaidi zinaeleza kuwa jamii hiyo ya wafugaji imeamua kujichukulia sheria mkononi baada ya kuchoshwa na matendo haya ya uonevu ambayo yamekuwa endelevu kwa muda mrefu.

UPDATE
Waliofariki ni Afisa msitu mmoja na Mgambo 2.

Inadaiwa kuwa mgambo hao walienda kutekeleza jukumu lao la kukagua eneo hilo la pori ambalo shughuli za kibinadamu zimezuiliwa, ndipo kundi kubwa la watu liliwavamia na kuwashambulia.

Kitendo hiki kilitokea baada ya Mgambo kuanza kuwaondoa mifugo waliowakuta, ambao kwa mujibu wa taratibu hawaruhusiwi kuwepo kwenye eneo hilo.

Watu 46 walikamatwa, na 28 kati yao waliotambuliwa kujihusisha na uvunjifu huo wa amani wamepelekwa mahakamani.
 
Serikali itume timu ya uchunguzi haraka vinginevyo Polisi watafanya mauaji kwa hao watu waliokamatwa ili kufunika ushahidi

Hawaaminiki hao wanatengeneza tatizo halafu wanashindwa kulitatua!
 
Tukio kubwa limeripotiwa kutokea mkoani Kigoma, Wilaya ya Uvinza ambapo polisi wanne wameuliwa Kwa sababu walitaka kuwanyanganya ng’ombe wafugaji wa jamii ya kisukuma kwenye msitu wa Kagera, Nkanda...
Unagusa ng'ombe za ngosha au masai ,wewe utakuwa unataka ni kwenda kwa sir God si bure
 
Wananchi Wanalijua Hilo Hivyo Wanawahi Kuwalaza Chini Wote
Ameuwawa Afisa Misitu, Na Askari Wa Akiba 3
Leo Wameongeza Idadi
Askari WA akiba ni mgambo!! Nani amewapa ruhusa kushika bunduki na kuua!?
 
Mwandishi unatuambia askari walitaka kufanya unyan'ganyi dhidi ya mfugaji lakini mwishoni mwa Uzi wako unatueleza kwamba Askari walikuwa wanataka tu kuwahamisha wafugaji.

Tukuaminije.

Je, una interest yoyote juu ya Hili ukijaribu kupindisha ukweli?
 
Askari WA akiba ni mgambo!! Nani amewapa ruhusa kushika bunduki na kuua!?
Thread Hii Ni Tukio La Pili Kutokea Huko Uvinza


La Kwanza Ameuwawa Afisa Misitu Mmoja Na Askari Mgambo 3


Leo Ndiyo Wananchi Wamewalaza Chini Askari Police Hao Wakiwa Na Mijegeje Yao
 
Back
Top Bottom