Frank Wanjiru
Platinum Member
- Apr 12, 2012
- 25,616
- 46,676
Upepo mkali ulioambatana na mvua kubwa iliyonyesha kwa siku mbili mfululizo umesababisha mapaa ya nyumba 15 kuezuliwa huku baadhi ya nyumba zikibomoka katika Vijiji vya Kasana na Nyarugusu, Wilaya ya Kibondo Mkoani Kigoma.
Tukio hilo limetokea Oktoba 21 na 22, 2026, ambapo upepo huo pia umesababisha mti kuanguka juu ya nyaya za umeme na kuongeza athari kwa Wananchi wa maeneo hayo.
Kufuatia maafa hayo, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kibondo kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo imetembelea Vijiji vilivyoathirika kwa lengo la kuwapa pole na kuwafariji Wananchi waliokumbwa na maafa hayo.
Aidha, Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo imewataka Wananchi kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya majanga ya asili na kutoa taarifa kwa Mamlaka husika wanapokumbwa na majanga ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa.