Kigoma: CHADEMA wamtangaza Elius Michael kuwania ubunge wa jimbo la Buyungu

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,496
3,461
Katibu Mkuu wa Chadema, Vicent Mashinji amemtangaza Elius Michael kuwania ubunge wa jimbo la Buyungu. Jimbo hilo liko wazi baada ya aliyekuwa Mbunge wake, Kasuku Bilago (CHADEMA) kufariki.

Katibu Mkuu-Chadema Dk Vicent Mashinji ameinyoshea kidole Tume ya Taifa ya Uchaguzi na kusema hawana imani nayo kutokana na viongozi wapya waliochaguliwa hivi karibun ambao ni Jaji Mkuu mstaafu Thomas Mihayo na aliyekua Katibu Muenezi wa Itikadi CCM Omary Mapuli

"Uvurugwaji wa chaguzi huleta mkanganyiko katika nchi. Na hatuwezi kuacha kushiriki uchaguzi kwasababu hatuna imani na tume ya uchaguzi, lazima tupate viongozi kulingana na matakwa ya wananchi", amesema Dk. Vicent Mashinji, Katibu Mkuu CHADEMA
 
Huenda tukapata movie ya aina yake, tume mpya, waziri wa kitengo mpya, katibu mkuu wa chama dola mpya.
 
Back
Top Bottom