Chadema yavamia Mkoa wa Kigoma kama nyuki, Mbowe ateketeza Jimbo la Buyungu kwa Chopa

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,798
218,442
Taarifa ikufikie popote ulipo kwamba, yule Mwamba wa siasa za Tanzania na Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe, leo anapiga mikutano mitatu mfululizo kwenye Jimbo la Buyungu katika ili Operesheni 255 iliyozinduliwa Jana Mwanga Center.

FB_IMG_1684412089333.jpg
FB_IMG_1684412082683.jpg
FB_IMG_1684412077155.jpg


Ratiba Kamili hii hapa :

1.Kata ya Nyabibule , Uwanja wa shule ya msingi Rimashi

2.Kata ya Gwarama , Uwanja wa mpira Gwarama

3.Kata ya Kakonko , Uwanja wa Mpira Kakonko .

Ikumbukwe kwamba Chadema ndio Chama pekee kinachoweza kufanya mikutano ya hadhara kwa sasa nchini Tanzania

Usiondoke JF kwa ajili ya Uhondo mwingi sana unaoambatana na operesheni hii .
========
UPDATES

Akina Thomaso karibuni

View attachment 2626642View attachment 2626643View attachment 2626644


Sent from my SM-J500H using JamiiForums mobile app
View attachment 2626645
 
Taarifa ikufikie popote ulipo kwamba , yule Mwamba wa siasa za Tanzania na Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe , leo anapiga mikutano mitatu mfululizo kwenye Jimbo la Buyungu katika ili Operesheni 255 iliyozinduliwa Jana Mwanga Center .

View attachment 2626457View attachment 2626458View attachment 2626459

Ratiba Kamili hii hapa :

1.Kata ya Nyabibule , Uwanja wa shule ya msingi Rimashi

2.Kata ya Gwarama , Uwanja wa mpira Gwarama

3.Kata ya Kakonko , Uwanja wa Mpira Kakonko .

Ikumbukwe kwamba Chadema ndio Chama pekee kinachoweza kufanya mikutano ya hadhara kwa sasa nchini Tanzania

Usiondoke JF kwa ajili ya Uhondo mwingi sana unaoambatana na operesheni hii .

Sent from my SM-J500H using JamiiForums mobile app
Hongereni makamanda wetu tupo pamoja!
 
Matumizi mabaya ya fedha za walipa kodi
Ruzuku ni fedha ya walipa kodi.

Ni kama mchanganisho wa mishikaki mayai.
 
Demokrasia mnaipenda lakini ajabu hamtaki pawepo na uwanja sawa kwa wachezaji, njia zinazotumika kuleta usawa unaita matumizi mabaya ya fedha!.

Sijui kule kwenye ripoti ya CAG utaitaje..
Usifadhaike mkuu. Nimeua ndege wawili na Jiwe moja.
 
CHADEMA OPERESHENI 255

Freeman Mbowe, alisisitiza kuwa "Tanzania inahitaji katiba mpya."

Moja ya mambo yanayotajwa kusukuma madai ya katiba ni kuzorota kwa huduma za jamii, wananchi kunyimwa haki, wanawake kukandamizwa na sheria kuwepo kwa zinazoumiza wananchi, hasa kwenye kodi na ushuru wa biashara.

1684415937390.png

Picha : Wanachama wa CHADEMA katika moja ya mikutano yao nchini Tanzania.

Katibu Mkuu wa Baraza la Wanawake la chama hicho, Catherine Ruge, ambaye kabla ya mkutano huo alilitembelea soko maarufu kwa wanawake wajasiriamali, Nazareth la mjini Kigoma, alisema ni dhahiri kuwa wanawake hao wajasirimali hawataweza kujikwamua ikiwa katiba ya sasa itaendelea kuwapo.

Kwa upande wake, mwenyekiti wa Baraza la Vijana la chama hicho kwa mkoa wa Kigoma, Boniphace Chuzura, alisema "serikali ya CCM imeshindwa kushughulikia matatizo ya kaya masikini kupitia mradi wake TASAF kwa kuwatumikisha kutengeneza barabara za mitaa", kazi ambayo yeye alisema inapaswa kufanywa na Mamlaka ya Barabara (TARURA) ....

Soma zaidi : Source : CHADEMA yazinduwa 'Operesheni 255' kudai katiba mpya – DW – 17.05.2023
 
Back
Top Bottom