Kigogo wa Magamba amdunda mkewe

Fidel80

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2008
Messages
21,965
Points
1,225

Fidel80

JF-Expert Member
Joined May 3, 2008
21,965 1,225
Kigogo huyo wa chama cha magamba wilayani Sumbawanga amemshushia kipigo kizito mke wake wa ndoa aitwaye Tuli Mwakibinda chanzo cha kipigo ni sms iliyo ingia kwa Tuli wkt wakiwa wamejipumnzisha sebuleni. Kigogo huyo ambae ni maarufu sana mjini Sumbawanga aliomba simu ya mkewe asome sms iliyo ingia usiku Tuli alikataa jambo lililo muuzi kigogo huyo wa magamba na kuanza kujifunzia kung fu kwa mkewe kana kwamba anajiandaa kwenda kupambana na wafuasi wa CHADEMA. Baada ya kipigo kizito Tuli alikimbizwa hospitali ya Serikali Sumbawanga jitiada za madaktari kuokoa roho ya Tuli ziligonga mwamba na kufariki tar.06/09/2011 asubuhi akiwa anapatiwa matibabu kutokana na kipigo cha mmewe.
Tuli alikuwa ni nesi katika hospitali ya Sumbawanga.

Mpaka sasa hivi kigogo huyo wa chama cha magamba yupo mikononi mwa vyombo vya usalama wao wanadai kaua bila kukusudia. Je kile kipigo alicho kuwa anamshushia alitegemea nini? Lengo lake lilikuwa kumwaribu sura ya mapokezi lakini bahati mbaya akawa ana ruka mpaka za masoti na kumuumiza tumbo Tuli.
Pumnzika kwa amani Tuli
Mwanga wa milele umwangazie.
Amina
 

IGWE

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2011
Messages
9,006
Points
2,000

IGWE

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2011
9,006 2,000
Hapo ndipo ninapoamini kweli binadam tumetofautiana sana kimtazo,...mm naamini nikichokana na mwanamke/au mtu yeyote basi dawa ni kupotezeana,..yaani hata kama tuna kitu cha aina gani kinachotuunganisha,......kupigana mm sio kabisaaa,....anyway r.i.p my sister Tuli Mwakibinda,....twakuganile fijo loli Kyala akuganile naloli...leka utusye kulutengano lya kyala
 

Fidel80

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2008
Messages
21,965
Points
1,225

Fidel80

JF-Expert Member
Joined May 3, 2008
21,965 1,225
Mtaje huyo bruce lee
Hapo ndo ninaposhangaa mimi, mwathiri hajatajwa jina, katajwa mwathirika!!
Wanaume wengine bwana! ndio yale yale ya mambo ya SIMU!
Kigogo wa CCM mbaroni kwa tuhuma za mauaji Send to a friend
Tuesday, 06 September 2011 20:26
0diggsdigg

Mussa Mwangoka, Sumbawanga
JESHI la Polisi Mkoa wa Rukwa linamshikilia kiongozi mmoja mwandamizi wa CCM mkoani hapa, kwa tuhuma za mauaji ya mkewe kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ni wivu wa mapenzi.

Kifo cha mwanamke huyo kinadaiwa kwamba kilitokana na kipigo kutoka kwa mumewe baada ya kumsababishia majeraha hivyo kuvuja damu nyingi na kufariki dunia baada ya kufikishwa hospitalini.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Rukwa, Isuto Mantage alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba kiongozi huyo wa anashikiliwa na polisi na afikishwa mahakamani wakati wowote.

Alisema tukio hilo lilitokea jana asubuhi majira ya saa tatu katika Kitongoji cha Kantalamba.

Kwa mujibu wa majirani, ugomvi wa wanandoa hao ulianza pale kiongozi huyo alipobaini kuwa mkewe yupo kwenye moja ya baa mjini hapa. Walisema baada ya kubaini hilo aliamua kumfuata na kumtaka warejee nyumbani.

Wakiwa nyumbani, inadaiwa kwamba mzozo ulianza baada ya mumewe kudai kwamba mkewe anatembea na wanaume mwingine. Baada ya mvutano wa muda mrefu, inadaiwa kuwa mwanamume huyo alianza kumpiga ngumi, mateke na kumbana shingo.

Majirani waliposikia sauti walifika, lakini walimkuta mwanamke huyo ameishiwa nguvu na ameanguka chini.

Majirani hao wakizungumza kwa sharti la kutotajwa jina gazetini walisema ilionekana kana kwamba mwanamke huyo alipigwa na kitu kizito kichwani. Walimbeba na kumpeleka hospitali jirani ya Dk Atman na walipompima walibaini kuwa ana majeraha ya damu kuvujia ndani ya ubongo.

Akiwa kwenye hospitali hiyo ya Dk Atman inaelezwa kuwa hali yake ilizidi kuwa mbaya hivyo wakachukua uamuzi wa kumpeleka Hospitali ya Mkoa wakati huo akiwa amepoteza fahamu. Alilazwa katika wodi ya wagonjwa mahututi ambako alifariki alipokuwa akipatiwa matibabu.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa, Dk Sadun Kabuma alisema walipomchunguza kwa makini walibaini kuwa damu inavuja ndani ya ubongo.

"Inawezekana alikuwa akikibamiza kichwa cha mwanamke huyo ukutani kwa nguvu hali iliyosababisha kuvuja kwa damu nyingi kwenye ubongo wake...... hata maiti anaendelea kuvuja damu puani," alisema Dk Kabuma.

Source:Kigogo wa CCM mbaroni kwa tuhuma za mauaji
 

bht

JF-Expert Member
Joined
May 14, 2009
Messages
10,338
Points
1,250

bht

JF-Expert Member
Joined May 14, 2009
10,338 1,250
khaa mnanikumbusha Dr. Majamba wa UDSM aliapa kamwe hatamiliki simu ya kiganjani anahofia ndoa yake...
 

NGULI

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2008
Messages
4,811
Points
1,225

NGULI

JF-Expert Member
Joined Mar 31, 2008
4,811 1,225
Kiongozi anapimwa kwa uvumilivu na Hekima. Huyo Tyson hana sifa ya uongozi kabisa. RIP Tuli
 

nimie

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2011
Messages
525
Points
195

nimie

JF-Expert Member
Joined Sep 9, 2011
525 195
Hivi m'ke akikushinda kabisa nafikiri bora kumpeleka kwao kuliko kumpiga, pumbafu huyo jamaa wa magamba alijua atarekebisha polisi. He can do so, but ndo kaua!!!
 

Forum statistics

Threads 1,379,853
Members 525,596
Posts 33,758,641
Top