Mjumbe wa mkutano mkuu wa umoja wa vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mahanya Edward (35 yrs) amekihama chama hicho na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Edward alikabidhi kadi yake ya CCM kwa Katibu wa CHADEMA jimbo la Kigoma Kusini Shaban Madele. Edward ametaja sababu ya kujiunga na CHADEMA kuwa ni kutokana na chama hicho kuwa na msimamo thabiti wa kuwapelekea wananchi maendeleo na ndicho chama ambacho kwa sasa wananchi wanakitaka.
Pia alitaja sababu nyingine kuwa ni CCM kupoteza mwelekeo na kukumbatia vitendo vya rushwa.
Source: Nipashe uk. 8