Kigogo UVCCM ahamia CHADEMA

CDM ni kawaida yenu kumpokea kila mwana CCM anayekuja kwenu! swali langu ni je huwa mnawafanyia character assessiment? kumbukeni hata Shibuda alihamia hivyohivyo!

Na Shitambala wa Mbeya, CCM walimfanyia assessment?
 
viona mbali wanajua nani atachukua nchi 2015 lakini nakukumbusha CDM sio sehemu ambayo utapata cheo sababu umekimbia ccm,..hayo mambo wanayo ccm walipompa wassira cheo..
Vyema mkuu! Wanajeshi wapiganaji wanatakiwa wawe wengi kuliko viongozi CDM. Mwaka 2016 January tutaimba hivi:

_Majeshi yalisonga mbele vifaru vikiunguruma mizinga ikikohoa, joka kulitafuta.
CCM yalikiona kijinga cha moto (CDM); Kilichomtoa nyoka pangoni mwake!
Naye Nepi alikiona Kijinga cha moto(CDM); Kilichomtoa nyoka pangoni mwake!
Naye Chikwete alichiona chijinga cha moto; kilichomutoa nyoka pangoni mwake!
Naye sita, wasira, maembe, lowasa, chenga chenga walichiona chijinga cha moto;Kilichomtoa nyoka pangoni mwake!
Nyoka pangoni mwake;x3
 
Nenda ukapiganie demokrasia ndani ya CDM, muulize ZITO kawa Naibu Katibu Mkuu hewa maamuzi yote ni kanda ya Kaskazini. Hata ikatokea Kafulila amepoteza ubunge, watamleta mhindi agombee ili kulipa fadhila kwa Sabodo

Very interesting!!! How old are you?

Tiba
 
Viva CHADEMA, endeleeni kuhubiri elimu ya demokrasia kwa wananchi, mtavuna samaki wengi sana. Mpaka papa mtawavuna kabla ya 2015.
 
Mamluki huyo. Katumwa kuja kuchungulia kunani Chadema

Huyu ni juu yake sasa kwani huku tunawataka wapiganaji na siyo mamluki

Mbinu za magamba tuna kitambo sana mifukoni,hapa ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo nakwambia hadanganyiki mtu.

Na naona huyu Ndg kaja wakati mwafaka!
Ndani ya chama tupo kwenye harakati ya kukoleza lile usemi tuliopumzisha usemao "TWANGA KOTE KOTE MPK KIELEWEKE"

Viva Chadema!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Mjumbe wa mkutano mkuu wa umoja wa vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mahanya Edward (35 yrs) amekihama chama hicho na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).Edward alikabidhi kadi yake ya CCM kwa Katibu wa CHADEMA jimbo la Kigoma Kusini Shaban Madele.
Edward ametaja sababu ya kujiunga na CHADEMA kuwa ni kutokana na chama hicho kuwa na msimamo thabiti wa kuwapelekea wananchi maendeleo na ndicho chama ambacho kwa sasa wananchi wanakitaka.Pia alitaja sababu nyingine kuwa ni CCM kupoteza mwelekeo na kukumbatia vitendo vya rushwa.

Source:Nipashe uk. 8

what's the catch?
 
Viva CHADEMA, endeleeni kuhubiri elimu ya demokrasia kwa wananchi, mtavuna samaki wengi sana. Mpaka papa mtawavuna kabla ya 2015.

Mkuu ila papa hasiwe White hair wala najitoa kwasababu ya siasa uchwara za CCM....
 
huyu anapigia mahesabu uchaguzi mdogo wa ubunge. Nadhani anafikiria kwamba hatimaye kafulila atapoteza kiti cha ubunge kutokana na kufukuzwa na nccr-mageuzi. Hivyo ameshaangalia upepo na kugundua kuwa chadema kiweza kupatia hiyo nafasi.

Wise thinking!!!! Hata mimi niliuliza ghafla sio kwa Kafulila huko. Mmmh CDM waangalieni sana watu kama hawa ambao wanajua nafasi CCM ni finyu bora walete vurugu CDM
 
Back
Top Bottom