'Kigogo' ni mtu wa aina gani?

'Kigogo' ni mtu wa aina gani?

CHENGU MANURE

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2015
Posts
914
Reaction score
567
Hili suala la kuitana vigogo, kigogo chanzo chake kilikuwa ni nini na wapi, Na pia nini hasa tafsiri ya neno kigogo.

Kuna
Kigogo wa serikali.... kigogo wa tra akamatwa.

Kigogo wa CHADEMA... mfano kigogo wa CHADEMA auwawa Geita.

Kigogo wa madawa ya kulevya.

Mke/mtoto wa kigogo.

Kigogo wa kanisa flani.

Hii kitu ipo dunia nzima au ni Tanzania tu, nini kigezo cha mtu kuwa kigogo, na hawa vigogo wanafaida gani nchini.

Msamiati huu tata wenye kuwapa watu vichwa bila sababu bora ufutwe rasmi kama hauna tija.
 
Ulaya vigogo huwaita logs yaani "two logs have been accused for smuggling" yaani "vigogo wawili watuhumiwa kwa usafirishaji kinyume".
 
kigogo = mmiliki wa pesa nyingi ambazo hakuzipata kihalali.

Mfano wa vigogo
riz1

hii kitu inatakiwa ipotee ndani ya miaka mitano.
Ukimuamsha bill gate hata usiku wa manane atakuambia alivyokuwa tajiri. Hawa wakwtu huku ukiwashtua kidogo tu wanakufa kwa presha.

Ni wakati wa kuwa na matajiri royal
 
Kigogo = mmiliki wa pesa nyingi ambazo hakuzipata kihalali.

Mfano wa vigogo
Riz1

TanZania daima waliandika taarifa ya Alphonce mawazo(Mungu ailaze roho yake pema peponi) kuwa kigogo wa chadema auwawa geita....

Hii ipoje??
Mawazo alijipatia pesa vilivyo halali???
 
hili suala la kuitana vigogo, kigogo chanzo chake kilikuwa ni nini na wapi, Na pia nini hasa tafsiri ya neno kigogo.

kuna
kigogo wa serikali.... kigogo wa tra akamatwa ...
kigogo wa chadema... mfano kigogo wa chadema auwawa geita..
kigogo wa madawa ya kulevya...
mke/mtotot wa kigogo...
kigogo wa kanisa flani.....

etc. hii kitu ipo dunia nzima au ni tanzania tu, nini kigezo cha mtu kuwa kigogo, na hawa vigogo wanafaida gani nchini.

Msamiati huu tata wenye kuwapa watu vichwa bila sababu bora ufutwe rasmi kama hauna tija.

Aulizwe tid aka kigogo, mnyiama,
 
Kigogo maana yake ni ukongwe au ukubwa au umaarufu zaidi ya wengine mfano vigogo wa ligi kuu ya uingereza manchester,arsenal,chelsea
 
Hahahah!...hilo la Kenya,lugha sanifu hamwezani nalo...hahah.
Nyote mliochangia hapa mmefeli..
 
Hahahah!...hilo la Kenya,lugha sanifu hamwezani nalo...hahah.
Nyote mliochangia hapa mmefeli..

Manyang'au washavamia Uzi, hamkawii kusema na kiswahili ni cha kwenu enyi wazee wa kupenda sifa
 
Kigogo refers to mtu mwenye mambo makubwa, au nguvu kubwa
Aidha kiuchumi, kisiasa, kidini...
 
kwa mawazo yangu kigogo ni mtu hai/EXITS ambaye yuko mahala flan kwa cheo flani ila anatumia cheo hicho kwa manufaa yake na kujilimbukizia mali .Na almost huyu mtu lazima awe na jina kubwa mahala alipo KIGOGO NI TOFAUT KABISA NA FISADI ki maana.
 
Back
Top Bottom