Mtela Mwampamba
JF-Expert Member
- Dec 19, 2012
- 537
- 347
Katibu Mwenezi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wa wilaya ya Tandahimba, Hamza Salum amejivua uanachama wake na vyeo vyake vyote katika Chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) sambamba na kiongozi mwingine ambaye ni Katibu wa CHADEMA wa Wilaya hiyo ya Tandahimba Ndugu Jafari Hassan maarufu kama "mwarobaini" aliyehamia CCM pia amesema;
"Kubwa lililonifanya nije CCM ni kwamba nimeitumikia kampuni ya watu kwa muda mrefu sana bila mimi kupata faida yoyote.,tumeona yaliyowakuta wenzetu ambao nao wamekitumikia chama hiko mpaka kufa kwao na Chama kimeshindwa hata kuwazika achilia mbali kuwauguza"
Hamza amepokewa na mjumbe wa kamati kuu ya Chama Cha Mapinduzi alhaji Abdallah Bulembo ambaye yuko wilayani Tandahimba katika ziara yake ya mikoa ya kusini inayoendelea sasa katika Mkoa wa Mtwara.
Huu ni muendelezo wa viongozi wakubwa wa Chama hicho kujiuzulu na kujiunga na CCM kwa madai mbalimbali, mengi yakiwa ni matendo maovu na unafiki uliokithiri wa Viongozi wa juu wa Chama hicho.
Binafsi nawakaribisha viongozi hao wa Chadema ndani ya Chama Cha Mapinduzi kwani mimi binafsi niliyaona hayo ambayo wanayaona sasa mapema mno. Haiwezekani Chama kinachoongozwa kwa misingi ya fitina na uzandiki kikaweza kubaki na viongozi ama wanachama ambao hawaamini katika misingi hiyo.
Binafsi, namshukuru Mungu kwa kuendelea kuwaonyesha njia watanzania na kuyafichua yale yaliyokuwa yakifanywa kwa siri na chuki zilizokuwa mioyoni mwao kiasi sasa wameziweka dhahiri na kuwabainishia watanzania walio wengi rangi halisi ya Viongozi hao wa Chadema.
Kidumu Chama Cha Mapinduzi.