Kigezo cha kwanza kwa mtu anayewania urais awe na shahada ya uchumi

King_Villa

JF-Expert Member
Feb 6, 2012
575
378
Habari zenu wakuu. Poleni na majukumu.

Hapa nilikuwa nimekaa tu natafakari mambo kadhaa ambapo niliangali tangu mwanzo wa awamu wa tatu mpaka hapa tulipo, huku nikichambua mambo kinagaubaga kwenye baadhi ya sera za viongozi wetu.

Nilijaribu kuangalia mafanikio na mapungufu ya awamu ambazo zilifanikiwa kujibu baadhi ya matatizo pamoja na misimamo na sera na vipaumbele kwa viongozi waliokuwepo kipindi hicho (priorities).

Katika awamu ya Rais Mkapa yeye alijikita sana katika kuondoa ujinga, alitengeneza mashule mengi ili kumuwezesha kila mtu kupata nafasi ya kwenda shule; kiukweli kwenye hili alifanikiwa maana elimu inaweza kututoa sehemu moja kwenda nyingine kiuchumi.

Maono yake yalikuwa mazuri maana Unapokuwa na elimu itakusaidia kufanya maamuzi sahihi hata kama hautakuwa na kazi wala kipato, lakini upungufu wa Sera hii utaonekana baadae utakapo kuwa umejaza wasomi wengi nchini ambao walipitishwa katika mitaala isiyowapa mihemko (motivation) ya kujikwamua kimaisha bila utegemezi wa serikali. Hii inaweza ikasaidiwa na mtu utakaye mkabidhi madaraka ni kiasi gani ataipokea sera hiyo.

Katika awamu ya Rais Kikwete aliweza kutengeneza nchi ivutie mataifa mengine kwenye uwekezaji, maanake aliweza kuitambulisha nchi kimataifa na fursa za ajira zilikuwa nyingi kutokana na uwepo wa makampuni mengi ya nje yanayojiendesha kwa faida. Kutokana na kuwepo kwa nguvu ya ununuaji (Purchasing power).

Upungufu wake ni kuwa serikali itakuwa na mapato hafifu kwasababu ili kampuni ijiendeshe kwa faida lazima utengeneze mazingira ya kampuni kulipa kodi kidogo au utengeneze mazingira ya kutoibana pesa ilimradi flow ya pesa iwe kubwa mitaani.

Pia serikali inapokuwa na mapato hafifu, big project kwa ajili ya nchi zitakuwa zinakwamishwa kutokana na ufinyu wa bajeti.

Awamu ya Rais Magufuli ameweza kujikita katika kuinua miundombinu ya nchi kama kigezo muhimu katika maendeleo ya nchi na ameweza pia kujikita katika kuboresha nidhamu ya kazi.

Upungufu wake mkubwa utaonekana baada ya watu kufanya kazi kwa weledi hakutakuwa na mianya ya kujipatia pesa isiyo halali hivyo utalazimika kupunguza matumizi ili uweze kujikimu na kile cha halali unachokipata pia kutakuwa na muanguko wa customers kwenye baadhi ya product ambazo haziitajiki kutumika na mtumiaji Mara kwa Mara. Kwahiyo, kampuni lazima itafute njia ya kujikimu kwa kile inachopata ikiwa ni pamoja na kupunguza wafanyakazi.

Pia kama kuna project zinafanyika kwenye kuinua infrastructure zinazotoka nje, mara nyingi kuna kuwa na flow kubwa ya pesa inayotoka kwenye mzunguko kwa ajili ya kulipia hizo big project hivyo kusababisha nchi kuingia kwenye mikopo.

Hizo ni awamu ambazo nilizishuhudia akili yangu ikiwa pevu.

My take:

Ningeomba kuwekwe sheria kuwa atakapochaguliwa Rais awe na at least Shahada ya Uchumi ili aweze ku-control baadhi ya mapungufu yatakayo jitokeza katika sera zake.

Kwanini nasema MCHUMI?

Binafsi nimepitia masomo ya uchumi na ninajua umuhimu wa kiongozi yoyote kuwa na elimu ya uchumi maanake unaipoitwa kiongozi, ujue waliokuchagua wanajua matatizo yao 100% ni maswala ya kiuchumi.

Mfano kufikia mwaka 2000, 75% ya Watanzania walikuwa wanategemea kilimo kwahiyo kuwainua wakulima na kuwatengenezea maisha mazuri kupitia kilimo lazima ujue market ya mazao yao.
Huwezi kuhusianisha mazao ya wakulima na utegemezi wa soko la ndani au la nje.
Hili haliwezekani kufanyika kama hauna elimu ya uchumi.

Mfano tutakapo zungumzia Darkmarket ni mpaka uwe na elimu ya uchumi ndio utaweza kulielezea hilo neno.

Economics is mostly needed for a any leader.

Ni hayo tu viongozi wangu .
 
Kama tu mbunge kuwa form four imeshindikana vipi shahada ya uchumi, rais ana washauri wa kila sekta sio lazima yeye abobee ktk uchumi. Hata sayansi ina faida yake unaona Magu alivyo jikita ktk mifumo ya kisasa hali Mzee wa Msoga alikuwa anahofia.
 
Umeandika sana.

Unadhani degree ya uchumi ina msaada gani kama mtu ameingia kwa maslahi yake na watu wachache?

Unadhani degree ya uchumi itasaidia nini iwapo mtu ni mdini,mkabila,mchama,mkanda,na mbinafsi?

Unadhani rais anaongoza nchi peke yake kiasi eti anapaswa kujua kila kitu kuhusu uchumi?

Rais anatakiwa awe na maono,mzalendo,mcha Mungu,asiyedhulumu haki za wengine,na mtu anayeshaurika.Kuna zaidi ya degrii za uchumi kupata rais bora.
 
kibaravumba,

Mcha Mungu si lazima.

Katiba hailazimishi kuwa na dini wala kumcha Mungu.

Hata Nyerere alisema akitokea ntu hana dini tutatafuta namna ya kumuapisha.

Wengi wanaojifanya wacha Mungu waongo tu.

Mkapa kanisa lake lilikuwa Palm Beach Hotel, sakramenti yake ilikuwa Scotch Whisky.

Alivyowania urais akawa hakosi Kanisa la Katoliki Immaculata la Upanga.

Alivyomaliza urais watu hawamuoni kanisani.
 
Wee jamaa bhana, kwa hiyo rais anachotakiwa kujua ni uchumi peke yake. vipi hii nchi haina watu wanaoweza kumshauri rais kuhusu maswala ya uchumi hadi awe mchumi mwenyewe..
 
Msingi mzima wa kutafuta viongozi wetu ni mbovu. Rais mzuri sio lazima awe na elimu ya juu. Ila ni lazima 1. Awe na hofu ya Mungu. Hofu nayoisema haihusiani na kuwa na dini au kuwa mpagani. Hofu ya Mungu ni kujua kwamba Mungu ndiye mkuu wetu sote na anataka kila mmoja wetu apate haki yake na kwamba alituumba tukiwa tofauti lakini anataka tusibaguane. 2. Ili Rais awe bora ni lazima awe ni mtu wa kuwaongoza wengine wafanye anayotaka. Matajiri wakubwa duniani hawana elimu kubwa sana lakini wana uwezo wa kuwaongoza watu wafanye wanachotaka. Kwa sababu hiyo ni lazima wanakuwa na washauri wazuri na wako tayari kukosolewa ili wafanye mambo kwa ubora zaidi. Matajiri wakubwa wanawatumia watu waliosoma na wenye uzoefu kuliko wao na wanafanikisha shughuli zao. Jambo la tatu na la mwisho ni kwamba Rais yeyote ambaye ni Rais bora hana ubaguzi wa kidini, kisiasa, kikabila, kiukoo wala kikanda. Swala la kuwa na shahada za uchumi au elimu kibwa is not an issue at all !!!
 
ingekuwa mada inayo husu picha ngekuelewa sanaaa....mada yako yahusu walosoma uchumiii...Toa MIFANO ya maraisi walosoma hiyo shahada ya uchumiii ...utaelewekaa

nawaza ...walosoma Gynecology ama Dentist ...ama Skin......hahhahahaha professinal hizo je?

...kila binadam ana karama...kikubwa ni namna unavyoitumiaaa..
 
Nimekubaliana na mawazo yenu wote, Naona logic yangu imekataliwa 100% .
Possibly something wrong within my thoughts.
Nashukuru 100% ya waliopinga mmepinga kwa hoja zenye ukweli.
Blessed J.F
 
Back
Top Bottom