Kigezo cha dini kinaninyima mwanamke

Kigezo cha dini kinaninyima mwanamke

joshydama

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2016
Posts
4,623
Reaction score
5,054
Ni sahihi kumkataa mwanaume au mwanamke kisa dini ni tofauti?

Ni kwamba kuna binti nampenda sana na namhitaji awe mke wangu. Ila ugumu unakuja pale tu kwenye kigezo cha dini.

Nimejaribu kumshawishi kuwa katika maisha ya mahusiano kitu cha msingi ni upendo wa dhati suala la dini ni nyongeza tu maana unaweza kumkataa mwenye upendo wa kweli na nia ukaolewa na mtu kisa tu mnatoka dini moja mwisho wa siku ukaishia kujuta maisha yako yote.

Ingawa yeye kwa upande wake anasema ananipenda tatizo lipo kwa wazazi na ndugu zake eti watamtenga.Kiukweli nashindwa nifanyeje kuhusu hilo suala.

Je niachane nae au niendelee kukomaaa nae vivyo hivyo huenda atabadilika au nimpige mimba ili iwe rahisi kumuoa.

Karibu kwa ushauri wenu wakuu.
 
The same to me! But tuliona dawa ni abebe mimba kwanza, akajifungua! Ikawa tumeshawamaliza nguvu!

NB:Njia hii ni hatari sana kama hujajipanga au kama bado mtoto wa mama!!

*Utamuacha baba, utamuacha mama.........!!
Ahsante Mkuu.

Nimejipanga ingawa huezi ukasema ujipange ukamilike kila idara mkuu.
 
Kuolewa siku hizi ni kama ajira, unataka kumpa na kuwapunguzia wazazi wake mzigo wa kulea na kumlinda na wanaume wachovyaji wasiotaka kuoa unawekewa vigezo!! Oa yeyote wa imani yako, siku huyo binti atakapopigwa mimba watakukumbuka.
 
Kuolewa siku hizi ni kama ajira, unataka kumpa na kuwapunguzia wazazi wake mzigo wa kulea na kumlinda na wanaume wachovyaji wasiotaka kuoa unawekewa vigezo!! Oa yeyote wa imani yako, siku huyo binti atakapopigwa mimba watakukumbuka.
Hicho kitu kinasumbua sana Mkuu.
 
Kuna sababu zingine uwa naona za kipuuzi sana, ktk kigezo cha dini hapo ugumu uja either Kati yenu mmoja mwislamu na mwingine mkristo, Lakini eti mnaachana kwa kigezo cha dini ikiwa wote wakristo hii aingii akilini.
Eti KKKT na TAG mfano lakini Mmmh mtakuwa amko serious.
 
kwema mkuu ... ile we unamajanga umeibiwa demu , umepeta mwingine dini haziendani aisee wewe pole sana
[emoji23] [emoji23]
Nouma sana Mkuu

Inabidi niende kwa babu kijijini akafanye mambo huenda gundu nalo linachangia.

Maana unaweza kuwa na gundu ila hautambui.
 
Back
Top Bottom