Kigamboni kwapamba moto!

Kigamboni kwapamba moto!

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,007
Mchakato wa kutathmini na kulipa wamiliki wa viwanja vya Kigamboni(kuanzia baada ya Feri kwa upande hadi Kibada) umepamba moto. Kulingana na matangazo yaliyopo,kila mmiliki wa kiwanja kitakachoathiriwa anapaswa kujaza fomu maalum itolewayo na Serikali ya Mtaa husika mahali ambapo eneo litakalochukuliwa na Serikali lipo. Baadaye,zoezi la tathmini litafuata kabla ya malipo husika. Kwa wale wamiliki walio nje ya nchi,wanapaswa kuwakilishwa na watu wenye Nguvu za Kisheria (Power of Attorney) itambulikayo kisheria. Kila mhusika asikie na kutekeleza haya. VUTA-NKUVUTE aka Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
 
Last edited by a moderator:
Kama wanalipwa sasa sisi unatuhusu nini.Peleka FB kule
 
Kuwalipa ni jambo moja, lakini kuwalipa haki stahiki ni jambo lingine,

Wakiwahamisha hapo wanawapeleka wapi?
 
Utapeli mwingine huu,hivi wale wa mabomu walishalipwa?magamba wasanii...mmh!!haya yetu majicho!!
 
THANKS GOD MAMILIONI MENGINE YAJA. NILIKULA M50 ZA KIPAWA KWA NYUMBA YA M8 SASA KIGAMBONi SJUI M250 au M350, AH AH AH AKSANTE JK. MJIFUNZE KUWEKEZA KT RISK BUSINES ZINA RETURN KUBWA,
DAH DUNIANI KUZURI JAMANI
 
Wenye eneo wameanza mchakato wa kulimiliki...
 
Shukrani ubarikiwe VUTA-NKUVUTE, ungetuwekea na hilo tangazo lenyewe ingekuwa bora zaidi.
 
Last edited by a moderator:
Kwanini wanalazimisha kujenga mji wao mpya kwenye makazi ya watu mpaka kuingia gharama kubwa kulipa fidia ambazo ni lazima kutatokea na mzozo mkubwa.
Kama mnapenda mji mpya kwa nini msifeke msitu wa mwabepande ili muepushe usumbufu na hili swala gharama za kuamisha watu kama vile hawana hadhi ya kuishi eneo hilo ni tusi ninalolipinga tangu kuanza kwa mpango huu dhalimu mlioupa jina la 'mji mpya'


Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Kuwalipa ni jambo moja, lakini kuwalipa haki stahiki ni jambo lingine,

Wakiwahamisha hapo wanawapeleka wapi?

Kwa nini mtu anakubali kuamishwa kwenye ardhi yake kupisha binadamu wenzake waishi hapo???


Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Mchakato wa kutathmini na kulipa wamiliki wa viwanja vya Kigamboni(kuanzia baada ya Feri kwa upande hadi Kibada) umepamba moto. Kulingana na matangazo yaliyopo,kila mmiliki wa kiwanja kitakachoathiriwa anapaswa kujaza fomu maalum itolewayo na Serikali ya Mtaa husika mahali ambapo eneo litakalochukuliwa na Serikali lipo. Baadaye,zoezi la tathmini litafuata kabla ya malipo husika. Kwa wale wamiliki walio nje ya nchi,wanapaswa kuwakilishwa na watu wenye Nguvu za Kisheria (Power of Attorney) itambulikayo kisheria. Kila mhusika asikie na kutekeleza haya. VUTA-NKUVUTE aka Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam


Mhe.Ndugulile upo? ebu weka taarifa hii sawa!.
 
haya majina yanayoishabikia hii post, ukiyatizama vizuri yanaonekana yanatoka kwenye paylist ya nape pale lumumba
 
Mkuu mimi nikadhani tayari wananchi wameisha chukua sheria mkononi baada ya kuona Kigamboni kwapamba Moto! kumbe ni mchakato wa watu kulipwa
 
"Kinana" weka mbali na tembo....ccm ni wazee wakung'oa wananchi kucha na meno.ndugu wananchi tuiogope ccm ni janga la taifa.ccm no majangili ya tembo yakiongozwa na muhamiaji haramu mwenye uraia fake kinana
 
Tangu enzi zile za kuzama pantoni Kigamboni mpaka sasa Kigamboni ilikuwa ni ya wananchi na katika mazungumzo ya muda mrefu serikali imekuwa ikisema itawajengea wananchi wa Kigamboni daraja na wananchi walishangilia. Mradi wa daraja umechukua muda mrefu kuanza kujengwa kumbe walikuwa wanaweka strategy ya namna ya kuwaondoa wananchi. Kumbe daraja ni kwa ajili ya wenye ela zao ambao watakuja kuchukua maeneo yao na si kwa ajili ya wananchi waliopo (ni madon wanaotegemea kuja kujenga Kigamboni
 
"Kinana" weka mbali na tembo....ccm ni wazee wakung'oa wananchi kucha na meno.ndugu wananchi tuiogope ccm ni janga la taifa.ccm no majangili ya tembo yakiongozwa na muhamiaji haramu mwenye uraia fake kinana
 
Kwa nini mtu anakubali kuamishwa kwenye ardhi yake kupisha binadamu wenzake waishi hapo???
Development economics tells real estate development, may act on high cost to meet a benefit which over come cost!! though its among of the economic benefit theory fallacies!!
Kwa sababu hapo pana fikika, pana huduma na miundo-mbinu, mandhari nzuri ( kuliko mabwe) nk, hivyo unaweza kulipa zaidi na kuwatoa watu hapo.
Hakuna option ya kukataa kuhama!!! ila pricing and valuation is a main option!! sina hakika watu wa hapo wanajiweka wapi, ushauri kuna haja ya kuita independent valuer!! serikali/project valuer akija akute report ya thamani ya eneo, na mjadala iwe hizo technical reports not otherwise
SP
 
Back
Top Bottom