Kigali City "The Singapore of Africa"


Sasa kwanini wacongo wenyewe wasitumie madini yao yawaletee maendeleo yao tangu enzi za kina Lumumba, Mobutu, Kabila Snr/Jr.
 
Usafi wa kila Jumamosi ya mwisho mwezi tumeiga Rwanda. Kwamfano Dar, serikali ikaamua barabara zote ziwe za kiwango cha lami, kuondoa gereji, biashara zote na wamachinga wote sehemu amabazo sio za biashara na barabarani, wahusika wakishirikiana na Tanesko, Jiji na TANROAD wakapanda maua na miti rafiki pembezoni mwa barabara, Usafi ukafanyika kila siku. Dar itapendeza.
 
Sasa kwanini wacongo wenyewe wasitumie madini yao yawaletee maendeleo yao tangu enzi za kina Lumumba,Mobutu,Kabila Snr/Jr.

Wakati wa mobutu aliyatumia hayo madini kukuza uchumi wa zaire kwa mfano 1 zaire (shilling) ilikuwa sawa na 1usd kwenye miaka ya 70-80

Pia naye hakujisahau alipooa nchi ilimzawadia madini kama vile almasi nk kama dhwadi kwa bwana harusi.


Sent using Jamii Forums mobile app
 

Aisee hapo umedanganya mzee baba,nimekuwekea data za Usd againist Zaire currency kwa kipindi cha 1970-1980:On average ilikua

Min ni 1usd:211.280

Max ni 1usd:275.356



Hio ratio ya 1:1 haijawahi kutokea mzee baba.
 
Hivi hawa jamaa ni wabantu?
 

Shida yetu ni siasa nyingi mkuu,tukianza huo utaratibu wa usafi kila J’mosi kua ni lazima na usipofuata sheria hio hatua kali zitachukuliwa then wataanza kuibuka wanasiasa huku UVCCM itasema hivi then kesho Bavicha wataibuka kusema vile, keshokutwa watu wa haki za binadamu wataitisha press ili mradi iwe vurugu vurugu tu.
 
Usafi ukifanywa na mmlaka zinazohusika na ukawekwa utaratibu mzuri na unaoeleweka wa adhabu tutafanikiwa sana. Kiasi kwamba raia hawatasubiri kila J'mosi ya mwisho wa mwezi. Tatizo kuna mikwara ya kisiasa mingi, na sifa kwa watawala kana kwamba wao ndio wanafanya usafi.

Moshi na Iringa ni safi wakati wote, watu wameelewa na hakuna shida. Kila mfanya biashara yupo responsible na eneo lake la biashara. Huwezi kuta mchoma mahindi au mkaanga mihogo anaacha uchafu akimaliza biashara kwa siku, anachukua fagio na kusafisha kiasi kwamba huwezi gundua kwamba hilo eneo lilikuwa bize na biashara.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…