Kifo: Ni stahili yetu au adhabu?

Kifo: Ni stahili yetu au adhabu?

jerrytz

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2012
Posts
5,990
Reaction score
4,356
Wanajukwaa,
Leo nimeona nishirikiane nanyi katika hoja hii tata. Licha ya wanadamu kuonekana kuzoea kifo bado kifo kimekuwa fumbo kubwa tangu nyakati za zamani, wanafalsafa na wataalaamu wa kada za maisha wameeleza kifo kwa namna tofauti lakini wengi hawakufikia hitimisho.

Nimekuwa nikitafakari kuhusu kifo na nimejenga hoja katika maswali matatu.

1. Je mwanadamu anastahili kufa kwa sababu ya ubinanamu wake?

Nimekuwa nikisikia watu wakisema, baadhi yao kwa kunukuu vitabu vya kidini kwamba kila nafsi lazima ionje umauti. Nini msingi wa kauli hii? Je mwanadamu anakufa kwa sababu ya ubinamu wake au kifo ni sehemu ya kuwa mwanadamu?

2. Kifo kama daraja kuelekea kwenye maisha bora

Hapa ipo dhana/ nadharia ya maisha baada ya kifo, bila kuathiri unaamini nini kuhusu hili, unadhani kuna maisha bora zaidi baada ya kifo? Baadhi ya wakristo wanaamini kuwa tupo duniani ili kuishi maisha yenye haki ya kumpendeza muumbaji ili awapatie zawadi ya uzima wa milele yaani maisha yasiyo na mwisho baada ya kufa. Niseme hili hapa, ni kawaida ya mwanadamu kutamani kuendelea kuishi, hii ipo kwenye akili zetu, maisha yasiyo na mwisho. Kwa waislamu wao wanaamini uwepo wa pepo ambapo wale waliompendeza Mungu wataishi.

3. Kifo kama adhabu kwa mwanadamu

Wapo wanaoamini kutokana na imani zao kuwa mwanadamu anakufa kutimiza adhabu ya kosa lillilofanywa na Adam na Hawa (tamko la Mungu kwa Adam na Hawa katika kitabu cha mwanzo sura ya tatu).Hapa mambo mengi huibuka kama kwanini mfululizo wa adhabu hii uendelee kwa vizazi vyote?! Je ni haki kwa mwanandamu mwingine kufa kwa kosa la Adam na Hawa? ! Hakuna aliyechagua kuwa mwanadamu kwanini tuchaguliwe kufa? ! Hii imefanya wengi kuamini kuwa tunaishi ili tufe.

Hitimisho: Japo kifo kinabaki siri naamini kinaweza kujadilika na kupanua ufahamu wetu kuhusiana nacho.
 
Kama ni Mkristo... Ukisoma kitabu cha mwanzo kwenye biblia utapata majibu ya swali moja wapo au yote...
 
mwili unachoka kama unavoliona gari likikongoloka na hatimae kufikia mwisho....
 
Unasema tumekizoea kifo?
We umechanganyikiwa nn?!
Labda wewe ndiye umekizoea,hivi unaweza lala chumba cha maiti pale muhimbili au amama hospital?
acha utani dogo kifo hakizoeleki maana anayekimiliki kifo na kukiamrisha kutenda ata sura yake haijulikani.Na kama tungekua tunaishi nae hapa chini ya jua na anaonekana kwa macho bas angekua ni billionea!!!
 
Kijana naona leo kwenu ni full pilau,maana sikukuu umechanganyikiwa asbh mapeeeema!!
Yani unasema tumekizoea kifo?
thubutu!!!
 
Imani aside practically kama watu wangekuwa hawafi basi ingefika wakati ingebidi watu waache kuzaa pia lack of resources ingebidi watu waanze kwenda kwenye hiberation (kuwa inactive na kuacha kutumia resources) au tungeanza kupigana na kuchomana moto au kuwala wenzetu ili tupungue na kupata kushiba
 
Sasa tukichomana moto na kula wenzetu si watakufa! Ww vipi bana? Acha kujichanganya
 
Daah ......hivi tusingekuwepo ingekuwaje? Kwa nini mungu yupo? Asingekuwepo je ingekuwaje?

Huwa sipati majibu ya maswali haya.....ukomo wa kufikiri hugota hapo
 
kwenye maisha kuna safari tatu KUZALIWA,KUISHI,KUFA ili kuwa na uwiano mfano mtu anapokufa nafasi yake inachukuliwa na atakayezaliwa siku hivyo
 
Sasa tukichomana moto na kula wenzetu si watakufa! Ww vipi bana? Acha kujichanganya
Soma tena nilichoandika......

Hata kama tungekuwa hatufi (cell dead) ila lazima ingetokea jinsi ya kupunguza population either kwa kuacha kuongeza idadi, au kubadilisha form ya uwepo from bulky to simple matter (from a being to ashes au from a being to rouphages / manure)
 
Unasema tumekizoea kifo?
We umechanganyikiwa nn?!
Labda wewe ndiye umekizoea,hivi unaweza lala chumba cha maiti pale muhimbili au amama hospital?
acha utani dogo kifo hakizoeleki maana anayekimiliki kifo na kukiamrisha kutenda ata sura yake haijulikani.Na kama tungekua tunaishi nae hapa chini ya jua na anaonekana kwa macho bas angekua ni billionea!!!

Eat the meat throw away the bones. ....

"maana anayekimiliki kifo na kukiamrisha kutenda ata sura yake haijulikani."

Kwa kauli hii, nani anamiliki na kukiamrisha kifo? !
 
Daah ......hivi tusingekuwepo ingekuwaje? Kwa nini mungu yupo? Asingekuwepo je ingekuwaje?

Huwa sipati majibu ya maswali haya.....ukomo wa kufikiri hugota hapo

Kama ukomo wa kufikiri umegota hapo, hizi kauli zinatoka wapi?

Apumzike kwa amani?!

Tutakutana paradiso? !

Bwana ametoa, bwana ametwaa?
Binamu ni wajuzi wa kutengeneza mazingira yanayoendana na haiba zao. ...
 
Ukifa ndio mwisho wako,sanasana utaongeza idadi ya madini ardhini! Huwezi kuishi tena popote pale,kila kitu kuhusu wewe kitakuwa kimefungwa!
 
Back
Top Bottom