Kifo ni somo kubwa kwetu sisi tulio hai

zandrano

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
7,150
7,728
Apumzike mzee wetu Rais Mstaafu awamu ya 2.

Kifo ni somo kubwa sana kwetu sisi tulio hai kuwa ipo siku nasisi tutakufa, hakuna atakaye ishi milele.

Haswa kwa viongozi wote mliopewa dhamana katika nafasi mbalimbali timizeni wajibu wenu kwa haki.

Tuishi kwa kupendana, tusioneane. R.I.P Mzee Ruksa.
 
Ninawapa pole sana wanafamilia wote, pia, na Taifa zima la Tanzania. huyu alikuwa Rais wetu, Mungu alimtumia maeneo mengi kuijenga nchi yetu.

Naungana nawe, kifo ni somo kubwa kwetu sisi tulio hai, ni mtihani mkubwa sana, wapo wanaofeli na wapo wanaofaulu. kufeli au kufaulu kunategemea wapi utaelekea baada ya kifo. Where are you going to spend your eternity? kuna maeneo mawili tu, aidha UZIMA WA MILELE au MOTO WA MILELE. this is real na inaogofya. maamuzi yako unayoyachukua hapa duniani, ndiyo yatakayokupeleka utakapostahili, Mungu hadhihakiwi na Mungu ni wa haki atampa kila mtu anachostahili, bila kujalisha ulikuwa nani hapa duniani.

Marko 8:36 Yesu aliwafundisha kwamba, Kwani itamfaidia nini mtu kuupata ulimwengu wote, akapata hasara ya nafsi yake katika moto wa milele, au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake (ili isiangamie baada ya kifo)? hii ndio theme ya huo mstari. pia,

Ufunuo 14:13 imeandikwa, Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sana. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao.

Yohana 14:6 Yesu alithibitisha kwamba, Mimi ndimi njia kweli na uzima, mtu haji kwa Baba ila kwa njia ya mimi.
Yesu alifanyika kafara la dhambi zetu alimwaga damu yake kwa ajili ya ondoleo la dhambi, ukitubu leo atakusamehe dhambi zako zote, utahesabiwa haki na hata ukifa aidha kwa ajali au ugonjwa (ambako hakupigi hodi, hatujui siku wala saa) utapata thawabu ya kuepuka moto wa milele, utaenda uzima wa milele. nakuasa, okoka leo, mpe Yesu maisha yako ili kufa kwako kuwe na faida.

ni hatari kufa bila Mungu. nanyi nyote wenye masumbufu ya dunia, Yesu alikufa kwa ajili yenu, kaa chini, tafakari, kwanini watu wanasema ukiokoka utakombolewa, chukua hatua, jaribu, ukiona wokovu haujakusaidia basi, ila umeshajaribu, isijekuwa hata kujaribu hutaki kumbe huko ndiko kwenye ukombozi wako. Mungu awasaidie.
 
"Death is not the greatest loss in life
The greatest loss is what dies inside while you still alive ". Ma nigga pac
the greatest loss is when you lose your soul to eternal hell, hiyo ndiyo mauti ya pili. itakufaa nini ukiupata ulimwengu wote, pata pesa zote, pata wanawake wote au wanaume wote kama wewe ni mwanamke, pata vyeo vyote, uwe rais wa kila nchi, uwe mfalme nakadhalika, ila utakapokufa unaenda moja kwa moja motoni? wakati Mungu ameweka njia ya wokovu, kwa Yesu Kristo Bwana wetu? wewe unayenisikiliza, jua leo kuwa uhai ulio nao ni opportunity Mungu amekupatia ili pengine utatubu na kubadili njia zako, pengine uponye nafsi yako.

KUMBUKA: vitu vingi tunavichukulia kisahisi tu tukiwa navyo, just vey simple yaani.
1. Huwezi kuona thamani ya chakuka, hadi siku ulale njaa kabisa huna chakula na watoto wanalia njaa.
2. Huwezi kuona thamani ya watoto hadi uwapoteze kwa kifo, walinde.
3. Huwezi kuona thamani ya uhai wako hadi pale utakapougua, ushindwe hata kusogeza mkono na una kila material thing hapa duniani wewe ni tajiri ila uzima unakiondoka.

Mungu amekupa uhai, ni kitu cha thamani, ila hajakupa bure, hataki upotee, anategemea uache njia zako mbaya, umgeukie yeye kwa kumkiri Yesu Kristo awe Bwana na Mwokozi wako ili pengone upone moto wa milele, Mungu hafurahii kifo cha mwenye dhambi.
 
Kufa hakujaanza leo! Kosa kubwa kubwa lililofanyika ni kutuleta duniani pasipo kutuuliza, then unaishi alafu unakufa, baadaye unaambiwa habari za moto wa milele!
 
Kufa hakujaanza leo! Kosa kubwa kubwa lililofanyika ni kutuleta duniani pasipo kutuuliza, then unaishi alafu unakufa, baadaye unaambiwa habari za moto wa milele!
umeongea kwa jeuri sana, huwezi kujibizana na Mungu aliyeamua kukuleta, alikuwa na lengo zuri tu na wewe kwamba umwabudu, uwe mtakatifu usiye na mawaa. nafasi hiyo bado ipo hata sana, umeshazaliwa na huna lolote la kumfanya Mungu, kilichobaki ni kuukubali tu ukweli kwamba yeye anakupenda, na alikuumba kwa mapenzi yake, na bado anakupenda, anatamani uwe mtakatifu ili hata huo moto usikukute. moto upo kwa ajili ya waasi na wewe walau bado u hai una nafasi ya kuwa mtakatifu kwa kumpokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yako, na uishi maisha matakatifu mikononi mwakw Mungu hapo utakuwa tayari umeuepuka. kama hutafanya hivyo, huna namna, nafasi hii usiipoteze.
 
kumbuka 1Wathesalonike 4: 13 -18 inasema kuhusu unyakuo, hawa wote wanaokufa,kama wamekufa katika Bwana (walimpa Yesu maisha yao), kabla hata wale ambao watafikwa na unyakuo wakiwa hai, waliokufa katika Bwana watafutuka then wataungana na watakatifu waliopo duniani, wote watapaa kumlaki Bwana mawinguni. hiki ni kitendo cha kufumba na kufumbua. mtihani sasa ni kwa wale ambao hawakufa katika wokovu, bwana wao atakuwa ni shetani aliyetengenezewa moto na hiyo ndiyo itakuwa ijara yao.

IMEANDIKWA: Lakini ndugu, hatutaki msijue habari zao waliolala mauti, msije mkahuzunika kama na wengine wasio na matumaini. Maana, ikiwa twaamini ya kwamba Yesu alikufa akafufuka, vivyo hivyo na hao waliolala katika Yesu Mungu atawaleta pamoja naye. kwa kuwa twawaambieni haya kwa neno la Bwana, kwamba sisi tulio hai tutakaosalia hata wakati wa kuja kwake Bwana, hakika hatutawatangulia wao waliokwisha kulala mauti. kwasababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza. Kisha sisi tulio hai tuliosalia tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele. Basi, farijianeni kwa maneno hayo.

KESHENI BASI KWA MAANA HAMJUI SIKU WALA SAA. hujui utakufa kwa ugonjwa, kwa ajali, kwa kupaliwa tu na soda, kwa ngumi, kwa majambazi au kwa kitu gani, ila kabla Yesu hajaja kuna halahala ukafa siku yeyote. msidanganyike na mafundisho yanayosema utaombewa ukiwa umekufa Mungu akusamehe dhambi hukohuko, never, Biblia inasema baada ya kifo ni hukumu, hakuna kutubu au kusamehewa tena. usifanye betting na maisha. ishi kiuhakika.
 
Amina mtumishi, barikiwa na Bwana Yesu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom