Kifo cha kanumba chazua ushirikina

Kifo cha kanumba chazua ushirikina

Maseto

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
944
Reaction score
546
Wana Jf.habari. Niko hapa Deluksi hotel,karibu na kwenye msiba wa kanumba.watu wamemzingira ajuza mmoja mnene,mfupi akiwa amevaa gauni anayedaiwa ameanguka eneo hili kutokana na ungo wake aliokuwa anasafiria kufeli.anadaiwa kutoa maelezo ya kujichanganya.kuna wanaosema anadai alikuwa anatokea mbagala akienda kwenye msiba wa kanumba,na wengine wanasema alikuwa anatokea sumbawanga kuelekea naigeria akiwa na wenzake wapatao watano kwenye kikao cha wachawi.vijana wameacha msiba na kumzingira bibi huyo,wengine wanamvuta bila utaratibu kama vile mbweha wanavyonyanganyana mzoga.ni balaa hapa.magari yanapita kwa tabu mno.watu wanaimba turudishie kanumba wetu,wengine mwanga!mwanga!
 
o la bongo ni kuamini uchawi kila kitu, hata kama wataona mtu kauawa watasema sio bure kule ushirikina palE, ACHENI HIZO JAMAA KAUAWA BASI HAKUNA UCHAWI HAPO
 
basi bibi wa watu kama ana mental disorder wanammaliza
 
Humu ndani kumeamia soga za kijiweni pale mwembechai
 
Ni moja kati ya dhana muflis, tena ni ule ufilisikaji uliyotukuka!
 
duh mie nimesikia eti walikuwa wanaenda songe ndo akadondoka hapo maeneo ya lion sinza
 
Weka picha basi,na ingekuwa kweli basi zingekuja sredi nyingi za hii habari sema ni cooked story ndio maana hipo ya kwako tu.
 
wadau hyo story ni ya kweli sio cooked kama mnavyodhani,mie pia nilikuwa karibu na hilo eneo namsubiri mtu,akachelewa kidogo alipofika ndio akawa ananipa hyo story kuhusu huyo bibi japo mimi binafsi sikufika kushuhudia.
 
Nimesikia clouds mda c mrefu.huenda ikawa kweli..mh does it mean kanumba kachukuliwa???mmmm wapi gwajima?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom