KIFO CHA HAWARA (mkono wa jini)
SEHEMU YA HAMSINI
MTUNZI:
Mbogo EDGAR
ILIPOISHIA SEHEMU YA AROBAINI NA TISA : hata lile lengo la kushirikiana nae nililiona halifai, japo nilisha panga kushirikiana nae bila yeye kujuwa mimi ni nani, na nina fanya nini, βmzee mimi naitwa Eric Frank, ni mwalimu wa taaluma, lakini nimekuja hapa kwaajili ya kuomba msaada na ushauri pengine maono juu ya kitabu ambacho ninakiandika kuhusu maisha ya binadamu, na viumbe vinavyoitwa majiniβ nilimueleza insp Aroub, huku nikijaribu kusoma uso wake kwamba atalipokea ombi langu au laaβ¦.β¦.ENDELEAβ¦.
Ukweli insp haroub alishtuka kidogo, baada ya kusikia hoja yangu na kunitazama kwa mshangao, nilihisi mambo mawili, moja ni kwamba pengine jambo alilotoka kuongea na mzee Mohamed linahusiana na kifo cha jana cha yule mfuasi wa Ussi, au anafahamu jambo kuhusu mchezo unao chezwa na muuwaji anae singizia jini, βkijana unadhani umekuja sehemu sahihi kuomba huo msaada?, mimi kazi yangu ni polisi, sasa nahusiana vipi na majini?β aliuliza insp Aroub, huku ananitazama kwa macho fulani yaliyo jaribu kuchangamka toka kwenye mshangao, huku macho yake yakiwa kama yananikagua hivi, wakati huo yule polisi koplo alikuwa anaondoka zake na kutuacha sisi wawili pale langoni.
Hapo nikaona kuna uwezekano wa kukosa kile nilichokitaka, hivyo nikatakiwa kujiongeza, kwanza nilianza kwa kucheka kidogo, βmzee nyie polisi mnakumbana na mengi, pia alieniambia nije nikuone sidhani kama alikosea, niwazi anautambua uwezo wako mkubwa wakupambana na kesi zinazo husu vitu kama hiviβ nilimueleza bwana Aroub, huku nikijichekesha kidogo, hapo insp alitulia kidogo kama vile anawaza jambo, kisha akainua uso wake na kunitazama huku anatabasamu, βbwanaaaa nani vile?β aliuliza insp Arob, kama vile amekubari kunisikiliza, na mimi nikamjibu kwa haraka, βEric, naitwa Eric Frankβ nilimjibu na kutega sikio kusubiri kusikia anachotaka kusema, βok! Hebu nifuate, na ninakupa dakika tano tu, maana kuna report nahitaji kuikamilisha haraka sana itumwe dar es salaamβ alisema insp Aroub, huku anaogoza kuelekea upande wa maegesho ya magari.
Naam!!! baada ya kutembea hatua kadhaa, insp akaanzisha maongezi, βhaya bwana Eric, hebu niambie, unatokea kampuni gani na unaulizia majini kwa maana ipi?β aliuliza insp Aroub, huku tukitembea taratibu kuelekea upande ule ule wa maegesho ya magari usawa wa lile Toyota spacio tulilokuja nalo.
Ukweli sikutaka tulisogelee, kwa sababu sikutaka Jessenia asikie ninachoongea na insp huyu mtu mzima, ambae lengo langu ni kushirikiana nae bila yeye kujuwa kuwa na mimi mpelelezi, βlabda nianze kujitambulisha tena, naitwa Eric, toka Mbogo Publishers iliyopo dar es salaamβ nilisema hivyo huku natoa kitambulisho fake, ambacho tunatumia dar es salaam, maana kampuni yetu ya upelelezi ni ya siri, japo inatambuliwa na serikali akakichukuwa na kukitazama, alitumia muda mfupi sana kukitazama, βmnajihusisha na nini?β aliuliza insp Aroub huku ananirudishia kitambulisho changu, βtuna jihusisha na uuzaji wa vifaa vya maofisini na uchapishaji wa makala na vitabu, pia mimi nina degree ya mipangilio za Tarakishi (computer softwere/program) na sasa nipo hapa Pemba, nime ajiliwa kwa muda kufundisha computer hapo shule ya sekondali ya Fider Castor, mwalimu wa computerβ hapo Arobu akanitazama kama vile ananifananisha na maneno ninayosema, βhoooo! kumbe upo vizuri eeh, sasa wewe umesomea computer zipi, yale makubwa au zile ndogo?β aliuliza mzee huyu, ambae niligundua kuwa uelewa wake juu ya computer ni mdogo sana, βmzee unapozungumzia computer, ziwe tarakilishi za mezani na zile mpakato au za mnara, zote zina mifumo ya kufanana tofauti maumbile na matoleo, pia uwezo kupokea mipangilio (program), uhifadhi pia na uzalishajiβ nilifafanua na hapo nikamuona tena Aroub ananitazama kwa namna ile ile ya kunikagua, βok! sasa kwanini msomi kama wewe unaanza kuulizia habari za majini?β insp Aroub aliniuliza swali ambalo nilikuwa nalitamani sana, kwanza tulicheka kwa pamoja, kabla sijamfafanulia, βni kwamba mzee wakati nikiwa namaliza kidato cha sita, nilikuwa nimeshaanza kuandika kitabu changu kinachoitwa Maisha unapande wa giza, nikijaribu kuandika kuhusu viumbe ambavyo kuna baadhi ya watu wanatoa ushuhuda kuwa wamekutana navyo, na baadhi wanaisi, kuwa ni mambo ya kufukilika, asa kuhusu viumbe vinavyoitwa jinniβ nilimueleza insp Arob, ambae sasa alionekana kuanza kuniamini, maana alikubaliana na mimi kwa kichwa, huku ananitazama tena, βok! sasa kwangu unataka nini maana mimi sio mganga wala mtabiri?β aliuliza insp Aroub, huku tuna ingia kwenye eneo la maegesho na bahati nzuri ni kwamba tulililenga gari moja la polisi ambalo lilionekana halija tembea muda mrefu kidogo, ni kutokana na nyasi chache kwenye matairi yake, βni kwamba mzee, ujuwe hii project niliisimamisha kwa muda mrefu sana, maana nilikosa dondoo muhimu kuhusu viumbe hivyo, lakini nilipofika hapa pemba nikasikia matukio mawili yanayohusishwa na jini, moja lilitokea week kama mbili zilizopita, na moja nimesikia leo asubuhi, nilipoulizia namna ya kupata hizi habari nikaambiwa nikuone wewe kwa sababu wewe ndie unae chunguza kuhusu vifo hivyoβ nilimaliza ufafanuzi na kumuachia Aroub aamue kama kuninyima ushirikiano au kunieleza anacho kijuwa ambacho ndio kitu cha kwanza nilicho kitaka kwa mzee huyu ili niweze kumsoma anachoelewa juu ya matukio haya ya kupangwa na mtu wa kawaida, au kama anafahamu juu ya kinacho endelea.
Insp Aroub, alitulia kidogo kama anawaza jambo fulani, kisha akainua uso wake, βkijana kwanza hongera sana kwa hiyo makala ambayo umeibuni, maana itatoa elimu nzuri sana kwa kizazi cha sasa, ila nikuambie kitu kimoja, ungekuwa umenijulisha ujio wako ungekuwa umefanya jambo zuri sana, maana kwa sasa nitakueleza kwa kifupi, ila ukipata nafasi utakuja tena kupata mengine zaidi, ila kwa sasa wacha nikueleze kwa kfupiβ alisema insp Aroub, akionyesha wazi kuniunga mkono katika kuandaa hiyo makala fake.
Mzee Aroub akaendelea kunieleza huku akisimulia mambo mengi niliyosimuliwa, yaani ambayo nilisha yasikia na kuyafanyia uchunguzi, βukweli kijana haya mambo ni mapana sana, aliekueleza kwamba uje kwangu hakukosea, maana ni mwaka wa tano sasa na chunguza kesi hii ambayo bado sijaipatia ufumbuzi, kuna kiumbe kinachosadikiwa kuwa ni jini, kina fanya mauwaji mara kwa mara tena kwa wanaume tu, mwanzo tulidhania vijana wawili wanafunzi walikufa kwa kuumwa na nyoka, lakini vipimo vilikataa kabisa, hata tulipopeleka sampuli dar es salaam, nao walikosa majibu ya chanzo cha vifo vile, lakini kwa upande wa wazee na wenye elimu ya majini wakasema kuwa vifo kama hivyo hutokea sana kwa watu wanao uliwa na majini ya bahariβ alieleza insp Aroub, huku nikijitahidi kumchunguza kama anaficha jambo au anasema anacho kijuwa, βlakini hapa karibu mashuhuda wanasema kuwa marehemu kama wawili hivi waliokutwa na janga hilo la jini, walionekana wakiongozana na mwanamke anae shabihiana, kwa maana maelezo yana mlenga mwanamke mmoja mrefu mwenye umbo la kuvutia, anaevaa baibui na niqab nyie watu wa bara munaita ninja, muda mfupi kabla hawaja uwawaβ alisema insp Aroub, na hapo nikamuwahi, βlakini mzee, unadhani huyo mwanamke ndie jini mweyewe?β nilimuuliza insp, ambae alishusha pumzi ndefu, kama vile alichotaka kunieleza hata yeye hajakiafiki, βndivyo tunavyo amini, maana hatuna viwezeshi kama tungekuwa na vifaa kama ulaya, nadhani tungeweza kulinasa hata tukio la jana usiku, ambapo huyu kijana ameuwawa hadharani kabisaβ alisema mzee Aroub, na hapo nilitamani kuamini kuwa haegemei upande wowote, lakini hapo hapo nikakumbuka kuwa muda mfupi uliopita alikuwa na mzee Juma Mohamed, mtu ambae nashuku kuwa anahusika juu ya kila kitu kinachoendelea, βsamahani mzee, hivi huyo jamaa alie uwawa naweza kukutana na ndugu zake, pengine anaweza kupatikana mmoja ambae alimuona akiwa na mwanamke au hilo jiniβ nilimuuliza insp kama mtego, maana nilijuwa fika kuwa lazima mzee Juma alikuja kumuona insp kuhusu kifo cha kijana wa Ussi.
Hapo insp Aroub nikawa kama nime mkumbusha jambo, βhuyo kijana ni mgeni hapa Pemba, aliajiriwa na mtoto wa mzee mmoja hivi kama ulimuona niliongozana nae wakati ule ulitaka kumsukuma, ndiyo nilimuita nimueleze hilo jambo, na yeye ndio kwanza anasikia hizo taarifa, hivyo anaenda kufanya utaratibu kama ni kuachia hospital izike au laa, maana amesema kuwapata ndugu zake itakuwa ngumuβ alisema insp Aroub, na hapo nikagundua kuwa, insp hakuwa anaelewa chochote juu ya mchezo unao endelea, βhooo! yule mzee niliwahi kumuona mara moja, kwenye msiba wa Vuai hapo msinginiβ nilimuambia insp Aroub nikijaribu kumleta kwenye ushawishi wa kujiweka wazi kama ni mshirika au la, maana kushiriki sio lazima awe muuwaji, ila akijuwa na kuficha nako ni kuhusika pia, βyah! na yeye anaishi pale msingini, na hao ni vijana wake wa pale mtaani umri wa Vuai ni kama wa kijana wake Ussiβ alisema insp Arobu, na hapo nikamchomekea swali tangulizi kabla sijaenda kwenye swali husika, βsamahani mzee kwa usumbufu ila naona maswali yanazidi kunijia kichwani, hivi unadhani huyo jini anauwa kwa sababu gani, maana katika dodosa yangu, ni kwamba jini huwa hauwi bila sababu, na kama angekuwa jini korofi basi mimi na wewe pia tunge kuwa hatariniβ nilimuuliza mzee Aroub, ikiwa ni njia ya kutambua kama anafahamu ukweli au la, βmh! ukweli ilo ndilo linalotushangaza hata sisi, maana tumewahi kusikia visa vingi vya majini, kama vile popo bawa, jini Chongo, na mengine, huwa yanatokea kwa sababu fulani na kuuwawa watu linalowahitaji kama huyu anavyo fanya, lakini mpaka sasa hatuja pata sababu au kitu ambacho kilitokea na kumnkasirishaβ alisema insp Aroub, ambae bado niliona kuwa hakua na muelekeo wa kuwa anatambua ukweli wa jambo hili, hapo nikacheka kidogo, kiasi cha yeye kunitazama kwa macho ya kuuliza, lakini kabla hajauliza lolote nikamuwahi, βsamahani mzee unajuwa hili jambo kwa sisi ambao hatuja kumbana na jini huwa tunaona kama hadithi za mbogo edgar, ila mlijaribu kuweka mtego wowote au kuwashuku watu fulani fulania kuhusika na matukio haya?β nilimuuliza mzee Aroub ambae alitabasamu kidogoβ¦β¦β¦ ENDELEA.
KIFO CHA HAWARA (mkono wa jini)
SEHEMU YA HAMSINI NA MOJA
MTUNZI:
Mbogo EDGAR
ILIPOISHIA SEHEMU YA HAMSINI : alisema insp Aroub, ambae bado niliona kuwa hakua na muelekeo wa kuwa anatambua ukweli wa jambo hili, hapo nikacheka kidogo, kiasi cha yeye kunitazama kwa macho ya kuuliza, lakini kabla hajauliza lolote nikamuwahi, βsamahani mzee unajuwa hili jambo kwa sisi ambao hatuja kumbana na jini huwa tunaona kama hadithi za mbogo edgar, ila mlijaribu kuweka mtego wowote au kuwashuku watu fulani fulania kuhusika na matukio haya?β nilimuuliza mzee Aroub ambae alitabasamu kidogoβ¦β¦β¦ ENDELEAβ¦β¦
Ni kama vile aliniona ninazungumza kitu ambacho yeye alisha kifanya, βunajuwa nilikuwa na mawazo kama ya kwako, kwamba kuna mtu anafanya matukio haya halafu anasingizia jini, lakini hatukufanikiwa kupata mshukiwa, na juzi kwenye tukio la kifo cha Vuai, nilipigiwa na watu wa jirani wa Vuai, kuwa ile nyumba ina security, kama tunaweza kuzikagua na kuona jinsi tukio lilivyo kuwa, na kwamba tuangalie kama kweli muuwaji ni jini au binadamu anae uwa kwa mtindo wa kipekee unao fanana na mauwaji ya jini, lakini bahati mbaya tulikuta mfumo wote wa camera ulikuwa mbovuβ alijibu insp Aroub, na hapo nilimshangaa kimoyo moyo, βkwanini unasema mfumo ulikuwa mbovuβ nilimuuliza insp Aroub kwa sauti tulivu, sikutaka aone mshangao wangu, βyah! tuliona kwa macho Vifaa vilikuwa vimeharibika haikuhitaji kuangalia mara mbili ili kuonaβ alisema insp, na hapo nilishindwa kuvumilia, βsamahani mzee ilikuwa ni mibovu au iliharibiwaβ swali langu lilimfanya insp Aroub anitazame kwa macho ya kunikagua, lakini safari hii hakukaa kimya, βkijana wewe ni mwalimu au mpelelezi?β aliuliza insp Aroub, ambae kiukweli, alinishtua na kunifanya nihisi kuwa ninaenda kuumbuka muda mfupu ujao.
Hapo nikajichekesha kibwege, huku nawaza ni mjibu nini ili kumuondoa kwenye hisia zake, lakini wakati nawaza nimjibu nini, insp Aroub akaniwahi βmaana una maswali ya kipelelezi, ambayo hata mimi sikuwahi kuyafikiria hapo kabla, ila sishangai sana, waandishi wengi wanakuwa kama wapeleleziβ alisema insp Aroub huku anacheka kidogo, βhooo! kumbe nafaa kuwa mpelelezi eeh?β nilimuuliza insp kwa kumzuga ili asigundue kama nilishtuka kwa swali lake, insp Alicheka kidogo, βyah! unamaswali mazuri, naimani kama ningekuwa na wewe toka hapo mwanzo ningefanikiwa kupata jibu sahihi, na pengine ningekuwa nimesha fanikiwa kumuona huyo jiniβ alisema mzee Aroub, ambae aliendelea kwa kusema kuwa, ukweli mazingira waliyo yakuta yalionyesha kuwa ile computer iliyobeba hard disc ilikuwa imevunjwa na kioo hakikuonyesha kitu, βsasa mzee tufanye marehemu alivunja mwenye security na kutoa hard disc, lakini sasa tujiulize alifanya hivyo kwasababu gani, si angeifungua na kutoa Hard disc, na kama kuna mtu alifanya hivyo ni nani, na kwanini, maana sidhani kama jini ana haja ya kuharibu mfumo wa camera za ulinzi ili kufanya jambo lakeβ nilimueleza insp Aroub, ambae sasa alikuwa amesha sahau kama anakazi kule ofisini maana tulikuwa tumesimama kwa zaidi ya dakika ishirini.
Insp Aroub alitulia kwa sekunde kadhaa, kama vile anawaza jambo kwa kina, kisha akavuta pumzi ndefu na kuishusha kwa nguvu, βyani hapa najiuliza ni kwanini wakati mwingine tusiwe tuna angalia vipaji kama hiki cha kwako na kuja kufanyia kazi ndani ya jeshi, maana unachokiongea ndicho nilichotakiwa kukichunguza mwanzo, hasa muda ule ambao tulikuwa tumetoka kuchukuwa mwili wa Vuaiβ alisema Aroub kama mtu anae jilaumu kwa kukosa kuliwaza hilo.
Kama ninge kuwa wewe msomaji, japo ninge mfumbulia fumbo ilo la camera, lakini ukweli lazima ningeingia kwenye matatizo, au kushukiwa katika nafasi ya kwanza, ila sikushindwa kutoa msaada, βila mimi naona jujachelewa, unaweza kupata jibu ambalo litatusaidia wote, wewe katika upelelezi wako, na mimi katika kukamilisha kitabu changuβ nilimueleza insp Aroub, kama vile natania, nikatulia kusubiri aniulize swali, βmh! sidhani kama naweza kupata chochote kwasasa, maana zimeshapita week mbili?β ujuwe kuna raha yake pale unapo kuwa na jibu, halafu unakaa kusubiri swali, βkwani unachotakiwa kujuwa ni kitu gani, mimi nadhani ni kufahamu kama camera zime haribika kabla au baada ya tukio, kama ni baada ya tukio nina uhakika kuwa huyo sio jini ni mtu kabisa ambae anafahamu madhara ya camera hizo endapo zitafika mikononi mwakoβ nilimueleza insp, ambae aliitikia kwa kichwa kukubaliana na mimi, βsasa nitaanzia wapi unadhaniβ swali hilo lilonyesha wazi kuwa mzee huyu alianza kuamini kuwa mawazo yangu yana mchango mkubwa sana kwenye kazi yake.
Hapo nikajifanya nawaza kidogo, kama natafuta jibu ambalo tayari nilikuwa nalo, nilitumia kama nusu dakika, kisha nikajifanya nimepata wazo, βhivi hakuna vijana wa karibu ambao walikuwa wanafahamiana na marehemu Vuai huko mtaani kwake?β nilimuuliza insp nae akacheka kidogo, βunaona basi hata hilo wazo sikuwa nalo, yupo kijana ambae muda wa tukio alimpisha Vuai aingie na mwanamke na ndie wa kwanza kugundua kuwa Vuai ameuwawa, nafanya mpango wa haraka sana kumpata kijana huyoβ alisema insp Aroub huku anajiandaa kuondoka pale tulipokuwepo, nilitamani kumuongezea wazo jingine la kumpata kijana mwingine wa Ussi, lakini nikasita kwa kuonekana ninafahamu mambo mengi kwa wakati mmoja.
Lakini nilimuona insp Aroub, kama vile amepata hamu ya kufanya kazi muda huo huo, βkijana naona tumeongea mengi, ila nahitaji kumpata yule kijana haraka sana, sitoweza kupeleka report dar es salaam pasipo kupata jibu la camera, hivyo chukuwa namba yangu ya simu, utanipigia kuona kama tunaweza kupata muda zaidi wa kupeana habari zitakazo patikanaβ alisema mzee Aroub, ambae sasa alionekana kuwa na haraka sana, akanitajia namba za simu, na mimi nikazihifadhi kwenye simu yangu, na mpaka namaliza kusave namba tayari Aroub alikuwa anatembea kwa mwendo wa haraka kuelekea kwenye jengo lao la polisi, nilitabasamu kidogo kwa kuona kuwa mzee huyu hakuwa anafahamu lolote juu ya kilichokuwa kinaendelea.
Nilitembea zangu taratibu kulifuata gari tulilokuja nalo, ambalo ndani yake alikuwepo Jessenia, ambae sasa niliweza kumuona ananitazama huku anatabasamu, tayari nilisha anza kuhisi njaa, maana hata nilipotazama muda kwenye simu yangu ilisha karibia saa tano za asubuhi, βwe Eric, yule insp Aroub unafahamiana nae, maana naona mnaongea kirefu haswaa?β aliuliza Jessenia mara baada ya mimi kuingia ndani ya gari, βniliagizwa kwake, ndio akawa ananieleza kuwa, mjomba wako alikuja hapa kuna mtu ameuwawa jana usiku, vipi umeisikia hiyo?β nilimuuliza Jessenia, ili nijuwe kama na yeye alikuwa anajuwa kuhusu mfanya kazi wa kaka yake kuuwawa jana usiku, wakati huo nawasha gari, βhapana sijasikia, wamesema ameuliwa na nani?β aliuliza Jesse kwa mshangao na uoga, βameuliwa na jiniβ nilimueleza Jessenia huku naondoa gari taratibu, βweeee! usiniambie, sasa mjomba yeye anahusiana nini?β aliuliza Jeseenia, wakati huo tunaingia barabara kuu nakushika uelekeo wa chake, βinsp ameniambia kuwa alie uwawa ni mmoja kati ya wafanyakazi wa Ussiβ nilimueleza Jessenia ambae alishtuka sana, βmamaaaaaa tayari mangeu amesha anza sasa, ndio maana mimi nakuambia tuondoke Eric tukaishi kwenu huko baraβ alisema Jessenia kama alie pagawa, na mimi nikajifanya namshangaa, huku namuwekea mkono begani kwake, βkwani sisi inatuhusu nini Jesse, we tulia mimi nimalize kazi zangu nakuja kujitambulisha kwenu kisha tunaondoka zetuβ nilimueleza jesse huku nampapasa begani, βyaani mimi nina wasi wasi na wewe na hivi mjomba ndio ameanza kukataa, yani nazidi kuchanganyikiwa kabisaaaβ alisema Jessenia, kwa sauti fulani ambayo licha ya kuwa katika unyonge wa kujidekeza lakini ilikuwa tamu sana, hilo usiliwaze Jesse, cha msingi ni wewe kukubali kuolewa na mimiβ nilimueleza hivyo huku natoa mkono wangu na kuongeza mwendo kuingia mjini chake chake, βJesse, hapa chake kuna sehemu ya kupata supuβ nilimuuliza Jessenia, βunasikia njaa eeh?β aliuliza Jessenia huku ananitazama βndiyo sijala toka janaβ nilimjibu kwa sauti ya msisitizo huku natazama kwenye eneo la mapaja yake, ambayo licha ya kuwa ndani ya gauni pana lakini niliweza kuona jinsi yalivyojaa na kutuna vyema, βkwani sasa tunaenda wapi si nyumbani kwako, kwanini usiende kula vitongoji?β aliuliza Jessenia na mimi kwa haraka haraka nikaona wazo lake halikuwa zuri, maana lazima nisinge kuta kitu ninacho hitaji kule vitongoji, βmh! sidhani kama itakuwa wazo zuri, maana kule wanamaliza mapema sanaβ nilimueleza Jessenia ambae tayari alikuwa amesha niondolea uvumilivu wa moyo na akili kwa rangi yake ya mdomo na wanja kwenye nyusi na kope zake za macho, na yeye akanielekeza mgahawa mmoja, uliopo njia ya markiti, kwa kuwa tulisha karibia chake chake, nilipunguza mwendo kidogo huku namtazama mschana huyu, ambae kiukweli siwezi kukuficha, mpaka hapo nilikuwa natamani kama ninge kuwa getoni nafanya kile ambacho nilimfanya jana, na leo nilipania kumfanyia vitu vingi ninavyo vijuwa, hakika sikutaka ajifunze kwa mwingine halafu anitukane wakiwa wanapeana dudu, maana kuna kisa kimoja nilipenda nikudokeze wakati natafuta maegesho hapa chake chake barabara ya marikiti maana ni finyu sana, je unajuwa ilikuwaje.β¦ ITAENDELEA..