KIFO CHA HAWARA (mkono wa jinni)
SEHEMU YA ISHILINI NA TANO
MTUNZI:
Mbogo EDGAR
NUMBER +255 743 632 247
ILIPOISHIA SEHEMU YA ISHILINI NA NNE: pili ni namna ambavyo Jessenia alivyokuwa ana nitendea ungesema ni mtu ambae tunafahamiana kwa muda mrefu sana, japo ndio siku ya kwanza kukaa pamoja, maana hata sikuile pale uwanjani, nilipishana nae tu, nasio kuongea nae kama ilivyokuwa leo, niliwaza hayo mpaka nilipopitiwa na usingizi, na kulala fofo, mpaka mida ya saa saba za mchana, niliposhtuliwa na mlio wa simu yangu, nikaichukuwa pembeni ya mto, na kuitazama kwenye kioo, kutazama jina la mpigaji, alikuwa ni simu toka ofisini dar es salaam kwa mkurugenzi wa MSC, yani bwana Winfred, hapo nikakumbuka kuwa nilisha sahau kuhusu kazi iliyonileta huku Pemba na kutopea kwenye matamanio ya kingono………
Hata hivyo nikaipokea haraka ile simu na kuiweka sikioni, “hallow mzee shikamoo” nilisalimia huku napanga majibu ya maswali ambayo bado nilikuwa sijaulizwa, “Eric ni week sasa hujatuma ujatuma taarifa yoyote, unafanya kazi kweli wewe?” niliulizwa na mkurugenzi Winfred kwa sauri ya ukali kweli kweli, hapo nikasema nikitetemeka tu nimeumia, ngoja kwanza nitulize akili, “boss hii kazi inahitaji utulivu, nikama nilivyo kueleza mpaka sasa bado hatuja hakikisha kama muuwaji ni mtu wa kawaida au jini, hivyo kuna vitu inabidi nivifanyie kazi kubaini muuji ni binadamu au jini” nilijibu kwa sauti tulivu isiyo na wasi wasi wowote, kisha nikasikilizia mkurugenzi ataongea nini, “na mpaka sasa wewe una amini muuwaji atakuwa ni nani?” aliuliza mkurugenzi, “mzee kiukweli kwangu mimi ni hamsini kwa hamsini, kuna wakati nataka kuamini kuwa muuwaji sio jini, kwamba kuna mtu anafanya hivyo tena sio mmoja, ila ninapofikiria kuhusu aina ya vifo vinavyotokea na jinsi watu wanavyo kutwa wamekauka na kubadilika rangi hapo ndipo napoondoa wazo la kuwa muuwaji ni binadamu” nilimjibu mkurugenzi, ila ukweli majibu yangu hayakuwa sahihi, “ok! Eric, sasa utakuwa unatoa report kila siku jioni, pia tazama kwenye account yako mshahara wao tayari, toa taarifa mara moja pale utakapo kwama na kuhitaji msaada wetu” alisema mkurugenzi na kukata simu.
Hapo nilishusha pumzi ndefu na kuachia kicheko cha chini chini, halafu nikainuka toka kitandani na kujiandaa kwenda kuoga, ukweli nikwamba, mpaka sasa nilikuwa naamini kwa asilimia sabini, na tano kuwa muuwaji ni binadamu, lakini nilikosa mambo mawili ya kunisaidia kumtambua muuwaji au kuthibitisha kama muuwaji ni binadamu, moja ni kwanini kila anaekufa anakauka damu, na pili kwanini huyo muuwaji wakike huwa anatoweka mara tu anapo fanya mauwaji.******
Naam saa kumi na nusu ndio muda ambao nilifika uwanjani pale chake chake, kwa kutumia usafiri wa umma, sikupenda kumsumbua Mwasenga kuhusu usafiri, nilisema nitamtafuta jioni wakati wa kurudi, muda mwingi nilikuwa nawaza kuhusu Jessenia, niliwaza kama jana ndio ulikuwa mwanzo wa urafiki wakudumu na Jessenia au urafiki wetu haukuwa endelevu, nilitamani kumuona tena Jessenia, mwanamke mwenye kunukia marashi mazuri na tabasamu angavu.
Pale uwanjani nilikuta watu wachache sana, ambao ndio kwanza walikuwa wanajiandaa na mazoezi, nikajiunga nao na kuana mazoezi, huku kila muda ulivyozidi kwenda ndivyo watu walivyoongezeka, nakumbuka siku ile sikumuona kabisa Maimuna, ambae alikuwa na kawaida ya kunitazama wakati nafanya mazoezi, lakini leo mpaka namaliza mazoezi saa kumi na mbili na nusu sikumuona Maimuna, sikujiuliza kwanini wala sikutaka kulifikiria swala hilo, kwasababu sikuwa na wazo na mtoto huyu, ambae nilihisi kuwa mwishowe angeniletea kashfsha ya kutembea na mwanafunzi au pengine ninge kuwa na bahati mbaya zaidi ya kupigwa jini.
Kama ilivyo kawaida mazoezi yalikoma baada ya adhana kusikika na mimi nika kusanya kila kilicho changu na kuweka kwenye begi, nikatoa truck kwenye begi na kuivaa juu ya bukta, nikavaa tishet kisha nikatoa simu kwenye begi, halafu huku nabofya namba ya Mwasenga nikabeba begi langu dogo, ambalo ndani kama kawaida huwa naweka kile kijipotable changu, cha AGP, (Automatic Gun Pistol) vibali vya kuimiliki pamoja na kitambulisho cha kazi, wallet yenye kiasi cha fedha na nguo mbili za kuzugia, kisha nikasepa zangu kuifuata barabara ya Markiti na kama ilivyo kawaida niliongozana na watu wachache waliokuwa wanatoka hospital wanaenda msikitini, huku simu ipo sikioni nasikilizia mwasenga apokee ili nimuombe aje kunichukuwa, sikuwa na wasi wasi na hilo, maana hii ndiyo mida yake ya kuleta walinzi Wawi messi, simu iliita bila kupokelewa mpaka ilipokatika, “dah! nimebugi” nilijisemea huku nawaza umbali wa kutoka chake mpaka machomane, wakati huo nilikuwa na katiza usawa wa msikiti, ambapo watu ndio walikuwa wanaendelea kuchukuwa udhu, na wengine walikuwa wanaingia msikitini, na baada ya kuuvuka msikiti sikuweza tena kuona watu wengine, nikabakia peke yangu na kama ujuwavyo tabia za visiwa vilivyopo Mashariki ya Africa, giza huwa linawahi kuchomoza na pia linawahi kuzama, hivyo kijigiza chepesi tayari kilikuwa kimesha anza kutanda, nashukuru sasa sikuwa na hofu kama ile ya mwanzo, kikubwa niliwaza kuhusu umbali ninaotakiwa kutembea kwa miguu.
Nikiwa naendelea kutembea kusogelea barabara kuu itokayo mkoani (kusini pemba kwenda kaskazini, yani huko wete) nikapiga tena simu kwa Mwasenga, nayo ikaanza tena kuita, yani iliita sana, mpaka wakati inakaribia kukatika, ndio ukapokelewa, “kaka vipi” alisema Mwasenga, wakati huo nilikuwa natokeza barabarani, “afadhari umepokea bro, maana nilishaanza kuwazia mwendo wa Macho mane” nilisema kwa sauti iliyojaa matumaini, “Ticha kumbe leo ulienda mazoezi, mi nilijuwa umepumzika bwana” alisema Mwasenga ambae sikuona kama kuna dalili ya yeye kuwa nagari, maana kulikuwa na sauti za watu waliokuwa wanaongea ongea, sambamba na sauti ya music wa chini, “nimeibuka zoezi, sema sikukujulisha mapema” nilimuambia Mwasenga huku naendelea kutembea kufuata uelekeo wa Macho Manne, “poa Ticha, lakini leo sipo na gari, kuna dereva mwingine ameenda kufuata walinzi, akifika nitamuambia akufuate” aliniambia Mwasenga, kisha tukakata simu na kuendelea kutembea taratibu.
Naam nilitembea kwa dakika kama tano hivi, sasa nilishapita njia panda ya Tibirinzi na kuvuka chuo cha uogelaji, na wakati na anza kuingia kwenye eneo la vichaka na kuiacha chake, nikikaribia njia ya kuingilia msingini mara nikasikia ngurumo ya gari ambalo lilikuwa linatokea upande wa Macho Mane, ukweli ilikuwa ni ajabu sana, maana ngurumo hiyo niliitambua kuwa haikuwa ya gari la mwasenga, na kweli hata liliposogea na kuonekana kwenye upeo wa macho yangu niliweza kuliona kuwa lilikuwa ni chai Maharagwe, lililoandikwa Wete Mkoani, kwa maana linatoka wete kuelekea mkoani.
Kwakutambua kuwa gari lile halikuwa na faida kwangu sikuhangaika nalo sana, maana lingekuwa linenda wete ninge abiria ili gari la Mwasenga nikakutane nalo Macho Mane, lakini sasa lilikuwa linaelekea mkoani, hata hivyo nikaliona limesimama usawa wa kijinjia cha kuingilia msingini, ilionyesha kuna abiria alikuwa anashuka, ni kweli lilishusha mtu na gari likaondoka na kunipa nafasi ya kumuona mtu alieshuka, mtu ambae alilipua mapigo yangu ya moyo na kunifanya nitamani kutimua mbio, alikuwa ni mwanamke mrefu kiasi ambae licha ya baibui jeusi alilolivaa kuwa pana, lakini katika mwanga hafifu wa saa moja kasoro niliweza kuona jinsi umbo matata la mwanamke huyu lilivyo kaa vyema kwa maumbile ya kike, maana niliweza kuona jinsi makalio yake makubwa na hips zenye upanda wa wastani yalivyo jichora kwenye vazi hilo ambalo ni vazi la kwanza katika kuhifadhi maungio ya binadamu hasa wa kike, maziwa yake makubwa kiasi yaliyo tuna kifuani kwa mwanamke huyu ambae kiukweli sikuweza kuona uso wake ambao ulizibwa kwa kitambaa ambacho huitwa niqab, huyu ndie mwanamke ambae anafanana kwa kwa asilimia kubwa na yule mwanamke ambae nilipata maelezo yake katika tukio la Madungu guest na kule Maskini hajengi kwa Vuai, na pia anafanana na mwanamke ambae nilimuona akiwa amepakizwa kwenye pikipiki na huyo huyo Vuai, nilitamani kukimbia lakini alikuwa mita chache sana, hata ningesema nikimbie isinge saidia, niliamini angenyoosha mkono na kunikamata bila hata kusogeza hatua, hivyo nikaamua kutumia maombi kama ilivyokuwa siku ile kule sokoni, maombi ambayo kiukweli sikuwahi kuyafanya, hapo kabla, “lakini nime mkosea nini mpaka nimuogope?” ndivyo nilivyo jiuliza kimoyo moyo, huku nikikemea pepo kimoyo moyo, huku nikiwa natembea taratibu kusogelea usawa wake, na kila nilipozidi kusogea nilianza kusikia harufu ya manukato kama yale ambayo hutumiaga Jessenia, muda wote nikiwa na waza hayo yule mwanamke alikuwa bado amesimama ananitazama ungesema ananisubiri mimi, iliiniogopesha kwa kweli, hapo nikaamua niweke tayari nguvu za mzungu, hivyo nilifungua zip taratibu, huku naendelea kusogea mbele, “asalam alaykum” nilisalimia mara tu nilipofika karibu yake, huku kimoyo moyo nakemea, nikipanga kuwa nitapo mpita nitembee kidogo halafu nianze kukimbia, wakati huo mkono wangu upo karibu kabisa na mdomo wa begi, tayari kwa lolote, endapo lingetokea huwezi kujuwa pengine ingenisaidia, “waalaykum salam Eric, za toka jana?” alijibu yule mwanamke, huku anatoa niqab yake na kunifanya nishushe pumzi ndefu, “hooooo! Kumbe ni wewe” nilisema huku nikijitahidi kuficha wasi wasi wangu, ni baada ya kuona kuwa hisia zangu zilikuwa tofauti na ukweli.
Huyu alikuwa ni Jessenia mwenyewe ambae uso wake ulijawa na tabasamu pana la furaha, “ni mimi huyo, au ulidhania jini alisema Jessenia, huku anacheka, na mimi nikacheka kwa nguvu, “kwanini unasema hivyo Jesse, nilijikuta napenda kumuita Jesse baada ya Seni kama wengine wanavyo muita, “yaani nilicheka sana alivyonisimulia Aisha siku ile, vipi lakini leo hujachukuliwa na gari” aliuliza Jessenia, sasa na mimi nikiwa nimesimama karibu yake, “gari linakuja, kuna sehemu lilienda” nilimjibu, huku tukitazama upande wa Macho Mane, ambako gari lingetokea, “hoooo! hivyo basi nisindikize kidogo, wakati unasubiri gari au nitakuchelewesha” alisema Jessenia kwa sauti fulani ya kudeka, “hata nikichelewa sidhani kama ni tatizo, maana sina umuhimu wakuwahi, kuliko usalama wako” nilisema kwa sauti ambayo haikuwa na shaka lolote kwamba nimeridhia kumsindikiza, sijui kwanini Jessenia alifurahi sana kusikia hivyo, maana aliachia tabasamu pana la furaha, “haya twende basi” alisema Jessenia, huku anaongoza barabara ya kuelekea msingini.
Sijui kwanini sikujiuliza hata sekunde moja, nikakubali mara moja kumsindikiza, pasipo kuwaza kuwa naweza kupishana na hilo gari, “vipi jana ulikaa mpaka saa ngapi pale staring?” aliniuliza Jessenia, wakati tunatembea taratibu kuelekea mtaa wa msingini, yeye akiwa mbele yangu, “nadhani ilikuwa kama saa saba hivi kama sio saa nane kasoro” nilimjibu kwa sauti tulivu, huku natazama eneo lake la nyuma kutathmini kiwango cha mgongo wake, “jana nilikereka kweli kweli, yaani Ussi amenitoa mapema pale Wawi na kisha yeye akarudi tena” alisema Jesseni kwa sauti ya kulalamika, huku akipunguza mwendo kama vile ananisubiri mimi na kuanza kutembea ubavuni mwangu, nilitaka kuhisi kuwa alishtukia nilichokuwa nakifanya, yaani kumtathmini makalio yake, “kaka lazima akuchunge dada yake” nilijibu kwa utani, “khaaa! Wanakera bwana, yani wote wananitazama mimi tu, mjomba ananitazama mimi shangazi mimi, hata yeye Ussi ananitazama mimi wakati yeye mwenyewe kutwa kuchwa yupo kumbi za starehe” alisema Jessenia kwa sauti ile ile ya kulalama, na hapo nikama nilikumbuka jambo ambalo nilitamani kupata majibu yake, hata hivyo nilihitaji akili nyingi kutoa swali hilo ilinipate jibu lisilo na shaka, “kwa hiyo unaishi na mjomba wako, vipi kuhusu mama au baba wao hawakutazami wewe?” nilimuuliza kwa sauti tulivu, “mh! si bora ningekuwa nao basi, mama alifariki zamani sana, ila baba yangu hakuna anaemfahamu” alisema Jessenia, huku anaushika mkono wangu na kuumanisha viganja vyetu, au naweza kusema alifunguisha ndoa, maana tulishikana kwa mtindo wa vidole kuingiliana ungesema tulikuwa na urafiki wa muda mrefu au ni wapenzi kabisa, ilisisimua moyo, japo lilikuwa ni jambo la kushangaza sana kwangu, jana nilijuwa tunashikana na kukumbatiana kwaajili ya starehe, sasa leo imekuwaje, na ukizingatia kwa utamaduni wa kisiwa hiki cha marashi ya karafuu mwanamke kushikana mikono na mwanaume namna hii ni hatua moja kubwa sana katika mahusino, pia isitoshe nilishawahi kusikia habari za kwamba, mschana huyu hakupenda mazoea kama haya na wanaume zaidi kusalimiana nao na kuongea mambo ya kawaida, tena kwa vijana wa ambao anawafahamu kwa ukaribu, zaidi ya hapo hakuna mzoea.
Ukweli maneno ya Jessenia yalinishanga kidogo, kwamba mama yake alikufa siku nyingi zilizopita na baba yake hakukuwa na mtu aliemfahamu, “ina maana mama yake Jessenia ndie hakuwa anaishi hapa pemba, kwamba ujauzito aliupatia huko mbali?” nilijiuliza kimoyo moyo kabla sijauliza swali la wazi, “hooooo! Kwahiyo baba yako alikuwa mwarabu sio?” nilimuuliza kama mtego, japo sikudhania kama majibu yake yalikuwa na maana yoyote kwangu au kwake, “ndivyo wanavyosema” alijibu Jessenia na wakati huo tulikuwa tunakatikaza kwenye majengo makubwa ya kifahari yenye kuzungukwa na kuta ndefu na madhubuti za kupendeza, “mh! inamaana hujawahi hata kuiona picha ya mama yako?” nilimuuliza Jessenia, huku namtazama usoni, nikamuona kama amenyongea kidogo, “angalau ningewahi kuiona hata picha yake, yani natamani sana kuiona sura ya mama yangu, hawana picha yoyote ya mama” alisema Jessenia na hapo alinishangaza kidogo, inakuwaje ndugu zake wakakosa picha yake hata moja, lakini sikutaka kumuuliza chochote kuhusu hilo, wakati huo tulikuwa tunaingia kwenye eneo lile lenye kibanda cha udongo na mihogo mingi, “pole sana Jesse, naamini ukiolewa na kutengeneza familia yako upweke utaisha” nilimuambia kwa sauti tulivu iliyo sheheni liwazo, nikamuona anatabasamu huku ananitazama, “mh! mume atoke wapi labda…” ni kama kuna kitu alitaka kuniambia lakini akaishia kuguna kidogo, na wakati huo mvumo wa simu yangu ukaanza kusikika, kwamba ilikuwa inaita toka ndani ya begi, kwa maana nilikuwa nimesha irudisha begini, nikaachia mkono wa Jessenia na kutoa simu kwenye begi, ambalo lilikuwa bado lipo wazi, nilipoitazama mpigaji ilikuwa ni namba ngeni, nikajiuliza kama niipokee au laa, maana nilihisi pengine ni simu toka dar, ambayo inahusu maswala ya kikazi, “mbona hutaki kuipokea au mkeo?” aliuliza Jessenia, huku anatabasamu, japo alitabasamu ila niliona kwenye sauti yake alikuwa na dalili ya kuchukizwa na kitendo cha mimi kuto kupokea simu ile, “mke? unazungumzia mke wa bibi na bwana au mke kwa maana ya jina la mtu fulani?” niliuliza huku nikijifanya kushangaa lile swali lake, huku nikionyesha kujiamini, wakati huo tulikuwa tumesimama, karibu na njia ya kuingilia kwenye kile kijumba cha udongo, “mke kama mke?” alisema Jessenia, huku akiachia kicheko, ambacho sasa hakikuwa na dalili za kuchukia, nadhani baada ya kuniona najiamini juu ya simu ile ambayo hata kama ningekuwa na mke sikuona sababu ya yeye kuchukizwa nayo, “mke atoke wapi bwana” nilisema huku napokea ile simu, “hallow..” kabla sijamaliza kuitikia ile simu nikasikia sauti kavu iliyojaa hasira, “oya bro, nipo chake hapa mbona sikuoni” ilikuwa ni sauti ngeni kabisa iliyo unguruma kwenye simu, nikatambua kuwa tayari huyo dereva alieachiwa gari na mwasenga atakuwa ameshafika chake na kunikosa, “hooooo! Sorry! Umenipita hapa njia panda ya msingini” nilisema hivyo, huku namtazama Jessenia na kumuaga kwa ishara, “poa poa” alisema yule mpigaji wa simu kisha akakata, “sasa Jesse, tutaonana kesho” nilimuambia Jessenia, huku naanza kurudi kinyuma nyuma, “sawa lakini ungepaona kwanza kwetu, ni nyumba hiyo hapo mbele yako” alisema Jessenia huku anaonyesha ile nyumba kubwa ya kifahari iliyopakana na lile eneo la kibanda cha udongo, “ok! siwezi kupasahau alama ni hili eneo” nilisema huku naonyeshea lile eneo kubwa lenye kibanda cha udongo, na wakati naonyeshea hivyo ndivyo nilipo shtuka kwa kugundua kuwa mita chache pembeni yetu, yani kwenye kichaka pembeni ya ile njia ya kuingia kwenye kile kibanda cha udongo, kulikuwa na mtu amesimama kwenye mafukutu ya mashina ya mihogo anatusikiliza tunacho ongea, na mtu huyu hakuwa mwingine alikuwa ni mzee Zidadu Makame, yaani mzee Mangeu………. INAENDELEA
KIFO CHA HAWARA (mkono wa jinni)
SEHEMU YA ISHIRINI NA SITA
MTUNZI:
Mbogo EDGAR
ILIPOISHIA SEHEMU YA ISHIRINI NA TANO: alisema Jessenia huku anaonyesha ile nyumba kubwa ya kifahari iliyopakana na lile eneo la kibanda cha udongo, “ok! siwezi kupasahau alama ni hili eneo” nilisema huku naonyeshea lile eneo kubwa lenye kibanda cha udongo, na wakati naonyeshea hivyo ndivyo nilipo shtuka kwa kugundua kuwa mita chache pembeni yetu, yani kwenye kichaka pembeni ya ile njia ya kuingia kwenye kile kibanda cha udongo, kulikuwa na mtu amesimama kwenye mafukutu ya mashina ya mihogo anatusikiliza tunacho ongea, na mtu huyu hakuwa mwingine alikuwa ni mzee Zidadu Makame, yaani mzee Mangeu……….Endelea…..
yule ambae ana alama nyingi na kubwa za makovu usoni mwake, sikutaka ajuwe kama nimemuona, hivyo nilikwepesha macho yangu pasipo kuonyesha mshtuko wowote, “basi sawa tutaonana kesho” alisema Jessenia kisha, kila mmoja wetu akageuka na kuondoka zake, niliondoka pale kwa kukimbia nikiwa na malengo mawili, moja likiwa ni kufika sambamba na gari pale njia panda, ambapo palikuwa na umbali wa mita kama sitini au sabini toka pale nilipokuwepo, pili ikiwa nikuondoka eneo lile kwa haraka, kukwepa mtego wa babu Mangeu ambao sikujuwa lengo lake.
Nilikimbia kama hatua kumi hivi, nikageuka nyuma ilikuona kama kuna chochote kilichotokea, yaani kama mzee Mangeu anifuata au laa, lakini baada yake nikamuona Jessenia aliekuwa anatembea kusogelea nyumba ile aliyosema ni kwao akigeuka na kunitazama, halafu alipoona nimegeuka akapunga mkono, namimi nikapunga mkono pia na kuendelea kukimbia, na hatua kadhaa mbele nikageuka tena, hapo nikamuona Jessenia anasukuma geti la pale nyumbani kwao nakuingia ndani, nakabla sijageuka kutazama mbele, yaani nakoelekea nikashtuka kumuona mzee Mangeu anaibuka toka kichakani na kuibukia barabarani kisha akatazama upande ambao mimi nipo, halafu akanyoosha mkono mmoja juu, ni kama alikuwa ananiita au ananisimamisha huku na yeye anaanza kutembea kuja upende ule, ukweli hapo niliongeza mwendo na kuzidi kukimbia kuelekea upande wa barabarani, ambako sasa niliweza kusikia ngurumo ya land rover defender likija kwa speed kutokea upande wa mjini.
Nilikimbia kwa speed, sikutaka kutazama tena nyuma, nilishaingia kwenye eneo lenye vichaka, mara baada ya kuivuka nyumba ya mwisho nikaongeza speed ungesema nakimbizwa na mnyama mkali, hakika ningekutana na mtu yoyote angedhania kuwa mimi ni mwizi niliekoswa koswa huko nitokako, nilibadili ukimbiaji mara baada ya kukaribia barabarani na kuweza kuliona gari likiwa mita chache toka njia panda linasogea kwa mwendo wa taratibu, nadhani dereva alikuwa anajaribu kuona kuwa nitakuwa nimesimama wapi.
Unajuwa kitu ambacho nilikifanya hata wewe lazima ungecheka kama sio kusikitikia, maana niliibuka barabarani kama vile sikuwa mbali wala sikuwa nimetoka kukimbia speed ya kilomita themanini kwa saa, gari lilisimama na mimi nikaingia na kutulia kidogo nikijaribu kushusha pumzi taratibu ili huyu jamaa yaani dereva ambae kiukweli alikuwa mgeni kwangu asijuwe kilicho nitokea, dereva ambae alikuwa amekunja uso kwa hasira akaondoa gari kwa speed ungesema anawahisha mgonjwa, ukimya ulitawala ndani ya gari huku nikiendelea kushusha pumzi, mpaka nilipoona afadhari kidogo, “mambo vipi kaka” nilimsalimia yule dereva ambae kwenye bega lake hakuwa na alama yoyote ya cheo, yaani alikuwa ni Private kwa cheo hicho cha chini kabisa, “poa” alijibu yule dereva ambae sura yake ilikuwa ngeni kabisa machoni pangu kwa sauti kavu, kama mtu mwenye kuchukia, hapo sikuona sababu ya kumsemesha, nikapiga ukimya na safari ikaendelea mpaka pale messi ambapo aliingiza gari na kuliweka kwenye maegesho, ambayo yalikuwa na magari kama manne hivi, ukiachilia gari aina ya Toyota V8 la bwana Ussi ambalo nilikuwa nalifahamu, mengine yote sikuwa nawafahamu wamiliki wake.
Dereva akazima gari nakushuka bila kuniambia chochote, kisha yeye huyoo akaufuata mlango na kuingia ndani ya ukumbi, akiniacha mimi ndani ya gari nikiamini kuwa kuna kitu anaenda kutazama kisha anakuja kunipeleka kambini nikaoge nije kula, lakini nikashangaa mpaka saa mbili kasoro inanikutia pale, “au amesahau kama ameniacha ndani ya gari?” nilijiuliza huku nashuka na begi langu mgongoni nikaelekea ndani ambako nilikuta watu ni wengi kiasi, si unajuwa week end, ukiachilia taarab ya jana leo kulikuwa na disco la kawaida, nikaangaza angaza macho kushoto na kulia nikitazama mtu alievalia nguo za jeshi, lengo likiwa ni kumtazama dereva, nikabahatika kumuona akiwa amesimama karibu kabisa na DJ, anapiga story na DJ huyo pasipo kuonyesha dalili ya kwamba anakumbuka kuna mtu alimuacha kwenye gari.
Kuna kitu lazima tuelewane kidogo, hii sehemu inamilikuwa na jeshi la ulinzi, hivyo basi, japo wateja wengi walikuwa ni raia lakini isingekuwa ajabu kumuona askari akiwa amevaa sale za kazi ndani ya ukumbi huu, maana kuanzia msimamizi wa ukumbi huu pia jamaa aliekuwa pale counter, na DJ wote walikuwa ni wanajeshi, japo walikuwa wamevalia mavazi ya kiraia, raia waliofanyia kazi hapa walikuwa ni wahudumu wawili wa kike ambao nao ni waschana kutoka bara.
Nilipoona hivyo nikamfuata mpaka pale, ambapo nilimkuta anaendelea na story zake anaongea huku anacheka kwa uchangamfu na DJ, walikuwa wanazungumzia mambo ya kambi ya mafunzo, niwazi huyu dereva alikuwa ametoka kwenye mafunzo fulani, “mambo vipi kaka?” nilimsalimia DJ, ambae ni kama alisha nizowea, “hoooo! ticha fresh, naona leo umechelewa kutoka mazoezi” aliongea DJ, wakati huo nikamuona yule dereva akibadilika sura na kununa kidogo, “ndiyo bwana kuna changamoto kidogo ilitokea” sasa ndio naelekea vitongoji” nilimjibu kisha nikamtazama yule dereva, “samahani bro, naona ulinisahau, nilikuwa nakusibri unipeleke kule…” kabla sijamaliza kuongea yule dereva akawahi, “sina mafuta ya kuendea vitongoji zaidi subiri mpaka muda wa kupeleka watu kambini” alisema yule dereva akiwa katika uso mkavu kweli kweli.
Dah! hapo nikashusha pumzi ndefu ya kuchoka, maana sikuwa na mamlaka ya kumlazimisha yule jamaa anipeleke nikaoge, ukiachilia kuwa mimi ni raia, ambae sikuwa mfanyakazi wa serikari, na kwamba nipo chini ya askari yoyote alieitwa askari, pasipo kujali kama ni mwenye cheo kidogo, pia katika mkataba wetu swala la usafiri, halikuwepo, hivyo sikuwa na namna “ok! poa poa” nilisema hivyo na kuondoka zangu pale kwa DJ, nikiwaacha wanaendelea na story zao, nilitembea kwa haraka kuufuata mlango wa ukumbi, huku nachakata akili yangu namna ya kufika kule AKC, (Ali Khamis Camp), bahati nzuri akili yangu wakati mwingine ipo haraka sana katika kutafuta ufumbuzi, wazo la kwanza lilikuwa ni kumpigia Malambo afisa utawala, lakini nikaona kuwa wazo lile lingine kuwa jema, kutokana na kwamba hawa watu na hii camp yao huwa hawana kuongea kirafiki, hasa mtu anapoonekana kufanya kiburi cha makusudi, lazima yule dereva angechukuliwa hatua za kinidhamu, sikuona kama ingekuwa vyema, hivyo nikaona ni vyema kama nitatumia wazo la pili, ambalo ni kumpigia simu mwasenga anipafanyie mpango wa usafiri.
Nikasimama usawa wa meza moja hivi ambayo sikuwa nimewatazama waliokaa, na kufungua zip ya begi kwa lengo la kutoa simu, “ticha vipi, naona leo umechelewa kutoka mazoezini” nilishtuliwa na sauti fulani toka kwenye ile meza ya jirani, sauti ambayo licha ya kuitambua lakini nikageuka ili kumtazama mwenye sauti hiyo ili kuhakikisha kama kweli ni yeye, nilishtuka kidogo baada ya kumtazama mtu alieniongelesha, “ndiyo bwana usafiri ulikuwa changamoto kidogo” alikuwa ni kijana Ussi, aliekuwa pamoja mwanamke mmoja ambae sikuwahi kumuona nae hapo kabla, walikuwa wanaendelea kupata vinywaji kama kawaida ya Ussi ya kutandaza vinywaji juu ya meza, “dah! utarudi tena kweli, au ndiyo moja kwa moja?” aliuliza Ussi, ambae alikuwa anaongea kwa uchangamfu, japo nilihisi utofauti katika uongeaji wake, ni kama alikuwa anajilazimisha kuchangamka mbele yangu, sikutaka kujuwa nini kimemsibu, “sidhani kama nitarudi, maana muda umeenda sana” nilimjibu Ussi, huku anikiwa natoa simu na kuibofya namba ya Mwasenga, ambayo iliita kidogo halafu ikakatwa, nikaitazama ilikujuwa kwanini ilikatika, lakini kabla sijafanya hivyo nikashtuka nikiguswa begani, nikageuka haraka ili kumuona alienigusa, “Ticha vipi, umeamua kula kabisa ndiyo uende camp?” alikuwa ni Mwasenga, ambae alikuwa na chupa ya bia mkono wake wa kushoto, “sikuwa na wazo hilo, ila yule jamaa yako naona safari yake imeishia hapa, yaani hapa nilikuwa nakupigia unisaidie namna ya kufika camp” nilimueleza Mwasenga huku narudisha simu mfukoni, “kwahiyo amekuacha hapa hapa?” aliuliza kwa mshangao Mwasenga, ambae alikuwa anakijiharufu cha pombe, huku anamtazama yule dereva kule upande wa kwenye kizimba cha DJ, akionyesha wazi kuwa anataka kumfuata yule dereva mwenzie, “achana nae bro, naona jamaa hayupo sawa, kama vipi nipate usafiri nifike camp” nilimueleza Mwasenga, ambae alionyesha kukasirishwa na kitendo cha yule mwenzie kuniacha pale Wawi Messi, “ana mambo ya kijinga huyu jamaa, unadhani afande Malambo akijuwa hujapelekwa camp atasemaje” alisema Mwasenga kwa sauti iliyojaa hasira.
Hapo ukapita ukimya mfupi, huku mimi nasubiria atafanya nini ili niweze kufika camp, “ok! kuna funguo ya spacio hapa si unaweza kuendesha gari?” aliniuliza Mwasenga huku anatoa funguo ya gari mfukoni mwake na kunikabidhi, “sasa bro, mimi naona ungenipeleka tu, maana siwezi tena kurudi huku” nilimueleza Mwasenga huku nikikataa kupokea funguo, “haina noma we nenda nalo tu, nitalichukuwa kesho, we lichek tu lile la mwisho kabisa” alisema Mwasenga na hapo nikaona ni wazo zuri, hivyo nikapokea funguo na kuagana na Mwasenga tayari kwa kuondoka, mara nikamuona askari ambae ana hudumiaga chakula anakuja upande wetu, mwanzo sikudhania kama anakuja kwangu, nikaanza kuondoka nikiwa naamini kuwa yule askari anamfuata Mwasenga, “Ticha nakufuata wewe” alisema yule askari na mimi nikasimama, wakati huo nikamuona Mwasenga anaondoka kuelekea kwenye meza yake, lakini hakufika mbali nikamuona yule askari dereva anatoka kule kwa DJ na kumfuata Mwasenga kule kwenye meza yake, tena alionyesha kuwa na haraka na wasi wasi, “hoo! Bro, nilidhania unakuja kujiachia na vinywaji” nilisema huku nacheka kidogo, “hapana nilikuja kukuuliza kama utakuja kula, maana tunataka kufunga kule messi” alisema yule jamaa, na ukweli ni kwamba nilipanga nikanunue chakula chochote hapo macho manne kisha niende zangu Ali Khamis Camp, “ukweli sitoweza kurudi kula, maana ndio kwanza naenda kuoga” nilijibu, na wakati huo nikamuon yule dereva anaongea kwa umakini mkubwa na Mwasenga, “basi poa kesho kaka” alisema yule mhudumu na tukaagana, kisha nikaondoka zangu kuelekea nje na nilipofika nje nikanyoosha moja kwa moja kwenye gari la mwisho kabisa, ambalo lilikuwa ni Toyota spacio jekundu.
Naam nilifikia gari na kufungua mlango, kisha nikaingia ndani na ile nawasha gari tu, nikamuona yule dereva anakuja mbio mbio, akionyesha anataka kuongea na mimi…. ENDELEA NAYO
KIFO CHA HAWARA (mkono wa jinni)
SEHEMU YA ISHIRINI NA SABA
MTUNZI:
Mbogo EDGAR
NUMBER +255 743 632 247
ILIPOISHIA SEHEMU YA ISHIRINI NA SITA: na wakati huo nikamuon yule dereva anaongea kwa umakini mkubwa na Mwasenga, “basi poa kesho kaka” alisema yule mhudumu na tukaagana, kisha nikaondoka zangu kuelekea nje na nilipofika nje nikanyoosha moja kwa moja kwenye gari la mwisho kabisa, ambalo lilikuwa ni Toyota spacio jekundu.
Naam nilifikia gari na kufungua mlango, kisha nikaingia ndani na ile nawasha gari tu, nikamuona yule dereva anakuja mbio mbio, akionyesha anataka kuongea na mimi…. ENDELEA……
Na hata sura yake ilionyesha uchangamfu tofauti na mwanzo, hivyo nikashusha kioo na kumsubiria, “Ticha vipi ndio unaenda camp?” aliuliza yule dereva kwa sauti iliyojaa uchangamfu, mara baada ya kunifikia, sikuona sababu yakumkunjia, kutokana na yale aliyo nifanyia, “ndio bro, bwana Mwasenga amenipa usafiri” nilimjibu kwa sauti iliyochangamka kidogo, “dah! samahani sana Ticha, ujuwe Mwasenga hakunifafanulia, ukizingatia mimi sikuwepo hapa camp” alisema yule dereva kwa sauti ya kama anaomba msamaha kwa kile alicho kifanya, “usijali kaka” nilimjibu huku nikionyesha uchangamfu mkubwa, kama vile sikuwa nimechukizwa na kitendo cha yeye kuninyima usafiri, “poa poa Ticha ila samahani sana, jamaa hakunieleza vizuri” alisisitiza yule dereva, kisha tukaagana na mimi nikaondoa gari kuifuata barabara kuu iendayo vitongoji na mimi nikaelekea upande wa Macho Mane, ambako niliishia eneo la madukani nikaweka gari pembeni na kushuka kwenda kununua samaki na chapati bila kusahau, sharubati (juice) ya mabungo, kisha nikarudi kwenye gari na kuondoka zangu kuelekea Ali Kahamis Camp.
Saa mbili na nusu nilikuwa tayari nimeshaoga nimejituliza mule chumbani naendelea kula huku naanza kutafakari kilicho tokea siku ya leo kule msingini kwa kina Jessenia, moja ukaribu wangu na Jessenia, ambao umezuka ghafla na kukomaa kwa haraka, pili tukio la kufuatwa na mzee Mangeu, “huyu mzee ni kweli anaweza kuwa mchawi na anafuga majini?” nilijiuliza huku naendelea kula samaki chapati na juice, vitu ambavyo vilitengenezwa kwa ufundi mkubwa, na kuwekwa viungo vizuri vya kuvutia, na kuongeza hamu ya kula, “lakini mbona sijamkosea kitu chochote yule mzee?” niliwaza hilo, huku nikikumbuka jinsi alivyo jibanza akitusubiria mimi na Jessenia tuagane, “au yeye ndie anaefuga majini na amegundua kuwa ninapeleleza hii kesi?” nilijiuliza hivyo mara baada ya kukumbuka siku ile alipokuwa anatusikiliza nilipokuwa naongea na wakina suleimani kule msibani kwa Vuai” niliwaza hivyo huku maswali mengine yakizidi kuongezeka kichwani mwangu, “kwanini alijificha pale kichani, je alikuwa amenitegea mtego wa kunifanyi jambo la kilozi, au alikuwa anatusikiliza tunacho ongea mimi na Jessenia, nakama nikusikiliza tunacho ili yeye kimsaidie nini, “kwanini yule mzee alijijaribu kunifuata, nikweli alikuwa ana jambo lolote na mimi au alitaka kunikausha damu?” niliwaza bila kupata jibu, lakini mwisho nikaona itakuwa vyema nikipata habari za kina kuhusu yule mzee Zidadu Makame ambae vijana wanamuita Mangeu, “nitamtumia Jessenia kupata habari za yule mzee” niliwaza hivyo nikiamini naweza kupata habari yoyote nzuri itakayosaidia katika kazi yangu ya huku Pemba.
Naam siku iliyofwata ilikuwa ni jumapili, siku ambayo nilichelewa kuamka pia, mida ya saa tatu za asubuhi ni baada ya kumashwa na milio wa simu toka kwa Mwasenga, “Ticha vipi leo utaenda mazoezi?” aliniuliza Mwasenga ambae anilimueleza kuwa nitaenda mazoezi mida ya jioni, japo moyoni mwangu nilikuwa nawaza sana kuhusu usalama wangu na babu Mangeu, maana zile dalili za jana hazikuwa nzuri kwangu, “ila pia mchana nitaenda mess kupata chakula cha mchana, nilikuwa na siku tatu sijala ugari” nilimueleza Mwasenga na yeye alisema tutakutana messi nyakati za mchana.
Ilikuwa hivyo, nilifika mess mida ya mchana, nikitumia gari nililopewa na Mwasenga, nikiwa na vifaa vyangu vya mazoezi na vile vya kujilinda, kikiwepo kisu na AGP kwenye begi langu, saa nane kamili nilikuwa ukumbini nimesha maliza kula tunaongea mawili matatu na Mwasenga, ambae alikuwa anapata bia mbili tatu, na mimi nilikuwa na chupa moja ya maji, sikutaka kunywa bia wala wine, kutokana na kwamba nilikuwa na mpango wa kwenda mazoezi hapo baadae, “sasa we tumia gari mpaka jioni, utanipatia mida ya chakula cha jioni utakapokuwa unapelekwa camp na defender” alisema Mwasenga, ambae kiukweli ni kama alikuwa amenirahisishia sana, maana nisinge hangaika kuhusu usafiri.
Nilikaa pale kwa muda mrefu nikiongea na Mwasenga, japo muda mwingi nilikuwa nawaza kuhusu Jessenia, hasa kuhusu jana wakati naondoka, maana alionekana kunitazama sana wakati ule, kuna kitu ambacho sikuweza kukitambua wakati ule kutokana na wasi wasi niliokuwa nao juu ya Mangeu, ila wakati huu niliweza kukumbuka na kuvuta hisia zangu, maana ile kugeuka geuka kunitazama mpaka anaingia kwao, nikama vile alitamani tuendelee kuwa pamoja, pia jambo lingine ni hisitoria ya maisha yake, hasa kitendo cha mjomba wake kutokuwa na kumbu kumbu zozote za wazazi wake, yaani mama ambae ni dada wa mjomba wake, na baba yake ambae ni mwarabu (kwa mtazamo wangu) na pia nilikumbuka matukio ya kuvutia ikiwa tabia yake ya kunishika mkono, na hata kunitazama usoni na kunionea aibu, kujitabasamulisha na kunizoea kwa haraka, vitu ambavyo nilivitafsiri kama dalili za Jessenia kunipenda, na kwamba angeni kubalia mara moja endapo ningehitaji penzi lake, labda nikudokeze jambo, mpaka muda huo tayari nilikuwa nimesha tamani na kulihitaji penzi la mwanadada huyu mrembo wa nguvu, na hata zile shutuma na hisia kwamba Jessenia ni jini nilikuwa nimesha achana nazo.
Saa kumi na nusu ndio muda ambao niliegesha gari kwenye kwenye eneo la wazi pembeni ya kidogo ya uwanja huu wa mpira wa kikapu, ambapo tayari nilikuta wachezaji wengine wamesha kuja, nilijiandaa na kuingia uwanjani, kama ilivyo kawaida yao hawakuwa na mzoezi ya kupasha mwili, kabla ya kuanza kucheza hivyo tuliingia moja kwa moja na kutengeneza timu mbili, kisha tukaanza kucheza, leo pia sikumuona Maimuna akitazama mazoezi, lakini haikunishtua, maana muda wote nilikuwa nawaza kuhusu Jessenia na kama ningepata bahati ya kumuona, nisingekuwa na uwezo wa kwenda nyumbani kwao, hasa kutokana na wivu wa binamu yake, yaani Ussi, niliendelea na mazoezi huku mara kwa mara nikitazama nje kama ningemuona Jessenia, ambae jana alisema tutaonana kesho, lakini mpaka saa kumi na moja na nusu sikuwa nimemuona Jessenia.
Naam nakumbuka mida ya saa kumi na mbili kasoro nikiwa nimeshakata tama kabisa ya kumuona Jessenia, ndipo wakati naendelea kucheza mpira na kufunga gori moja zuri la dunk, najuwa inahitaji maelezo marefu ili kuelewesha, lakini kwakifupi ni kwamba, nilipokea mpira over head pass, nikiwa nje ya duara la D, yani umbari wa hatua kama ishirini toka kwenye gori, nikadunda mara moja na kuukamata mpra nikianza kuhesabu hatua tatu za layup, ambayo iliishia kwenye mduara mdogo wa funguo, yaani sehemu ambayo hutumika kutupia mitupo huru, (free shoot/penart), kisha nikainuka kurukia gori, na hapo nika utumbukiza mpira kwenye kikapu, kwa kuweka kabisa, nikigusa chuma cha kikapu, (rim), kila mmoja alishangaa kwa jinsi nilivyoruka umbari mrefu, na wakati huo huo ndio ambao nilisikia mtu anapiga makofi toka nje ya uwanja, sio peke yangu niliegeuka kutazama kule nje kwenye kibaraza cha jengo la KVZ, macho yangu yaka kutana uso kwa uso na Jessenia ambae alikuwa amesimama akinitazama, na hata macho yetu yalipokutana alitabasamu kidogo na kutazama pembeni kama ilivyo kawaida yake,”mwanangu wewe noma, dah! kama NBA” walisema wachezaji wenzangu, japo ni kawaida yangu kufanya mambo kama yale hasa kipindi ninapokuwa ninafanya mazoezi kwa muda mrefu, “dah! wakija stone town lazima tuwapige safari hii” alisema mwenzao mmoja, huku mwingine akitoa wazo lake, “hapa cha msingi tumuombe bwana Pross aanze tukochi” hilo lilikuwa wazo zuri, lakini kwa mfumo wao wa mazoezi sikufikir
ia kama itakuwa vizuri, “nikweli kabisa, tuanze utaratibu wa mazoezi kabla ya mechi ijayo na wete” alishauri mchezaji mwingine, huku tukiendelea kucheza, sikuacha kutazama nje mara kwa mara kuona kama Jessenia alikuwa anaona kile ninacho kifanya mchezoni, nae nikamuona akiwa ananitazama na mara kwa mara macho yetu yalikutana na yeye kutabasamu na kutazama chini kwa haraka ungesema pengine kuna kitu tulitoka kukifanya, hali ile ilinifanya nijihisi vizuri sana, niliona kama mazoezi yanachelewa kuisha, maana nilitamani kuondoka na Jessenia kwenye gari hili nililokuja nalo, pengine ningepata furasa ya kuwa karibu na mwanamke huyu, na pengine kuweza kufikisha ujumbe wangu kwake.
Lakini nilishtuka mida ambayo adhana ilisikika na sisi kusitisha mazoezi, ndipo nilipotazama pale alikuwepo Jessenia, lakini sikumuona tena, haya sasa ukaribu wa eric na yule mdada seni mwenye sifa za umbo za yule jini wetu unazidi, vipi kuhusu ussi vipi kuhuze mzee mangeu? …… ITAENDELEA MUWE NA USIKU