KIFO CHA HAWARA (mkono wa jini)
SEHEMU YA KWANZA
MTUNZI: MBOGO EDGAR
NUMBER: +255 743 632 247
MWANZO : Ilikuwa ni majira ya saa saba mchana siku ya juma mosi, kilomita mbili toka kati kati ya mji maarufu sana Kisiwani Pemba Chake Chake, ni wakati ambao zilikuwa zime tawala habari za uchaguzi mkuu wa raisi wabunge na wawakilishi wa mwaka 2005, kipindi ambacho kwa kawaida zilijaa hofu kwa wananchi wa kisiwa hiki, kutokana matukio ya chaguzi zilizopita hasa mwaka 2000 sasa basi, kwenye nyumba moja ya kulala wageni iliyopoa kwa utulivu wake (tofauti tulivyozoea Tanzania bara) inayofahamika kwa jina la Madungu Guest house, iliyopo maeneo ya Madungu pembezoni mwa barabara kuu iendayo kusini pemba itokayo Chake Cheke kwenda mkoa wa kusini Pemba kupitia Mtambile mpaka Mji wa Mkoani (Ndiyo jina la mji huo) barabara ambayo ilionekana kupambwa kwa bendera za vyamba mbali mbali vya siasa, madugu guest ikiwa jirani kabisa na makao makuu ya jeshi la polisi la mkoa wa Chake Chake.
Naam tukiwa hapo Madungu Guest house aliingia kijana mmoja mwenye asili ya uchotara wa mswahili na mwarabu, japo asilimia kubwa alikuwa ni mwarabu, alievalia kitanashati japo kwa wakazi wa Tanzania bara wangesema alivalia simple, ila kwa huku ungesema amevaa kiungwana, maana ukiachia kofia yake ya duara (baraghashia) nyeupe yenye kudaliziwa kwa nyuzi za hariri, pia alivalia shati lake blue lenye draft nyeupe na nyekundu pasipo kuchomekea, na suruali yake nyeusi huku chini akivalia viatu vya wazi, sijui kama ndio maandiko sahihi kwamba ni sendoz, lakini ndivyo tunavyo itaga.
Kijana yule mwenye muonekano wa hali nzuri ya kimaisha, huku kidevu chake kikitawaliwa na ndevu nyeusi za kung’aa, ambazo zilionyesha uarabu wake alielekea moja kwa moja mpaka mapokezi na kuongea na kijana mmoja wa kiume aliekuwepo pale mapokezi, ambae mara moja alimpatia funguo na kumtajia chumba namba kumi na moja, kwamba ndio chumba alicho takiwa kijana yule mwarabu akaingie, na huku wakiwa kama walisha wahi kuonana kabla ya hapo, yaani ilionekana kuwa yule kijana alishatangulia mwanzo kuja kufanya mipango ya chumba kwenye ile nyumba ya kulala wageni, “sasa nikuambie kitu, we nenda kamchukue mlango wa nyuma” alisema yule kijana mwarabu, hapo kama walio elewana toka mwanzo, yule kijana akaenda kule kwenye mlango wa nyuma.
Naam ile anaukaribia tu mlango akasikia harufu nzuri ya manukato, hapo yule kijana muhudumu wa vyumba mwenye asili ya watu toka bara, ambao huku kisiwani hupewe jina la mnyamwezi, akajikuta akisisimkwa na mwili wake, maana alijuwa fika kuwa harufu ile inatoka kwa mschana aliesimama nje ya nyumba ile na aliejiandaa kwa kuja kupewa dudu, labda kuna kitu nikudokezee, ni kwamba mschana wa kiarabu au anaefua tamaduni hiyo huwa ana maandalizi makubwa sana pale anapoenda kwenye tendo la ndoa, wanasema ni moja ya ibada, na anatakiwa kumfanya mwanaume avutike na kuhamasika wakati anampatia dudu, hivyo hujifukiza marashi mbali mbali na kujinyunyuzia utuli wa kila aina,ukifikia wakati baadhi ya wanaume hujikuta anasimamaisha mnazi hata pale anapo kutana na mschana huyu ndani ya dala dala au kupishana nae njiani.
Ndiyo ilivyo kuwa kwa kijana huyu muhudumu wa hii guest house, mara tu alipofungua mlango ule mdogo wenye gate la chuma na kumkuta mschana mmoja mwenye umbo na kimo cha kupendeza, maana kwa haraka haraka ungesema ni mschana toka bara, kwasababu miili mingi ya waschana wenyeji wa visiwa hivi vilivyopo mashariki mwa Afrika walikuwa ni wenye maumbo ya kiingereza, yaani wembamba kama waarabu na wengi hawa shep ile namba nane, tofauti na huyu ambae usawa wa macho yake alionekana kuwa ni mweupe kabisa, tena kama mwarabu, lakini umbo lake ni zaidi ya mschana wa bara mwenyewe, maana alikuwa mschana mrefu kiasi mwenye kifua cha wastani, wembamba wake hasa maeneo ya tumboni ungesema kuwa ni mvivu wa kula, japo alikuwa amevalia nguo ndefu nyeusi, yaani baibui lenye hariri za rangi ya dhahabu kwenye pindo zake na kifuani, lakini usinge shindwa kuona jinsi alivyo jaaliwa makalio na mapaja yaani hips pana zenye kuvutia kila mwanaume mwenye macho yenye kimbele mbele kama ya
Daudi1 huku akifunika nywele zake kwa ushungi mweusi, pia aliziba uso wake kwa kitambaa fulani cheusi kama wapiganaji wa kijapan wenye asili ya Ninja, kwa wale wa uarabuni wanaita niqab, harufu nzuri ya manukato ilitawala eneo lile, “assalam alaykum” ilikuwa ni sauti nyororo na nzuri iliyojaa aibu kilo mia toka kwa mschana huyu mzuri ambae alionekana mwenye wasi wasi mwingi kana kwamba ile ndio ilikuwa mara yake ya kwanza kuingia sehemu kama ile, ambayo kikawaida mtu akiingia anajuwa kinachofuata ni kitu gani, ya kwamba ni kupeana dudu tu na si jambo jingine, ukichukulia pengine ni mwenyeji wa maeneo haya haya na sio msafiri, “waalaykum salaam shemeji karibu ndani” alisema kijana muhudumu, kijana muhdumu wa guest ambae alivutiwa na muonekano wa mschana huyu, hata alipo jaribu kumtazama usoni mwanamke huyu hakika ilikuwa ni vigumu sana maana mschana huyu alikwepesha macho kwa aibu na kutazama chini na yule mschana akaingia ndani akimfuata nyuma kijana yule mwenye asili ya kutoka Tanzania bara,
Naam talishi wa nyumba ya wageni bwana Hassan Mohamed, ambae ni mwenyeji wa mkoa wa Tabora, Pemba alikuja kutafuta maisha, alimchukuwa yule mschana na kumpeleka kwenye chumba namba kumi na mmoja ambako aligonga mlango ukafunguliwa na yule kijana chotara, ambae jina lake alijulikana kama Abdulqadir Amer, (unaweza ita Ame) na yule mschana akaingia haraka ndani ungesema aliona mtu ambae anaweza kuwafumania, “hooo! punguza wasi wasi basi, si hivi umeshaingia na hajakujuwa mtu” alisema Abdulqadiri, kwa lafudhi ya kipemba, huku akimshika mkono mpenzi wake huyo kama vile anamzuia asikimbie sana, kisha akamuingiza ndani ya chumba kile namba kumi na moja, huku bwana Hassan mnyamwezi wa tabora pale Itigi anataka kuondoka zake ili kuwapisha wapenzi hawa wafanye ya kwako, “sasa Hans hee! hebu niagizishie sahani mbili za chips mishikaki mi nne juice ya ukwaju na bakuli moja la urojo” alisema Abdulqadir huku anampatia noti ya shilingi elfu kumi bwana Hassan au Hans kama walivyo kuwa wanamuita, “chenji ni ya kwako” alisisitiza Abdul, kisha akaingia ndani na kufunga mlango kwa ndani, hapo Hassan hakuweza kuondoka mara moja, alisimama kidogo pale mlangoni, ni kama kuna jambo alikuwa analisubiri huku akitikisa kichwa kwa masikitiko ya wivu, “dah! dogo anafaidi huyu, hebu ona ule mzigo umejazia wowowo kama amesusiwa, halafu sijui amelitoa wapi lile demu, utadhani ametoka bara” aliwaza Hassan akiwa ameganda kwenye mlango wa chumba kile namba kumi na moja, ambao ulikuwa umesha fungwa, “ngoja kwanza nioge basi, mbona unaharaka weye” ilisikika ile sauti tamu ya kike yenye lafudhi ya kipemba, “si uvue basi ukaoge sasa unaenda oga na nguo zako” alisema Abdurqadir kwa saut ya kubembeleza, “naenda vulia msalani, naona haya mie” alisema tena yule mwanamke, sauti yake ikiambatana na kicheko ambacho kilionyesha wazi kuwa amejawa na aibu, ungeweza kusema kuwa mschana huyu ndio alikuwa anaingia kwa mara ya kwanza na mwanaume katika mazingira kama haya, “haya bwana mshindi weye nenda kaoge” alisikika Abdul, kijana mwenye jina kubwa sana hapa mjini Cheke chake, kutokana na biashara yake ya manukato na mapambo ya wanawake kama vile mikufu na hear ring (heleni) pia viatu na nguo za ndani, “na lile dirisha lifungwe bwana wasije kuchungulia” alisikika tena yule mwanamke ambae mimi na wewe hatuja mfahamu ni nani kutokana na kufunika sura yake, “usijali nitafunga we nenda kaoge tu” alisema Abdulqadir Ame.
Hapo Hassan hakuona sababu ya kuendelea kukaa mahali pale, akatoka zake na kuelekea alikotumwa ambako ni kamwendo kidogo, ni umbali wa mita mia tano toka nyumba ya kulala wageni, hakuwa na wasi wasi ya kuwa endapo atakuja mteja mwingine kule ofisini kwake na kumkosa, maana Nyumba ile ya wageni yenye vyumba kumi na saba haikuwa na wateja wengi kama zilivyo nyumba nyingi za kulala wageni za Tanzania bara, maana huku Pemba kuna wakati bwana Hassan hukaa hata week hajaona mteja hata mmoja, labda kipindi cha sikukuu au msimu wa watalii na kipindi cha uchaguzi, maana watu wengi wa kisiasa huja na kuchukuwa vyumba pale Madungu guest house na ndio maana bwana Hassan hutamani kama kila mwaka kungekuwa na uchaguzi pasipo kujali vurugu na usumbufu unaotokeaga.
Nusu saa baadae tayari Hassan alikuwa ameshapata Chips, urojo juice ya ukwaju, na vitu vyote alivyo agiziwa bwana Abdulqadir, na sasa alikuwa njiani anarudi kule ofisini kwake huku muda wote akiwaza jinsi Abdul atakavyo kuwa anafaidi kitumbua cha yule mwanamke, japo hakumuona kwa sura, lakini umbo la yule mwanamke lilitosha kabisa kuonyesha kuwa alikuwa ni mzuri na mtamu kiasi gani, ni kama alichizika kijana huyu ambae licha ya kuwepo huku Pemba kwa miaka saba lakini ukweli waschana wazuri wa kipemba ambao idadi yao kubwa wenye asili ya kichotara wa kiarabu aliishia kuwaona kwa macho tu na kuwaita shemeji, maana hakukuwa kazi ndogo kumpata mwanamke wa kipemba na ukamshawishi akupe kitumbua bila kutangaza ndoa, na sifa kubwa lazima uwe mtu wa dini na ushiriki ibada pamoja na swala tano, hapo bwana Hassan ambae unaweza kusema kuwa ni jina lake pekee ndilo linalo mtambulisha kuwa ni muislam akaanza kubahatisha kwa waschana toka bara ambao wengi wao ni wa kutoka Tanga, wanaokuja kufanya kazi kwenye bar maarufu ambayo kwa kipindi hicho ilikuwa moja pekee inayo milikiwa na Jeshi la ulinzi, inafahamika kama staring Mess, hapo ndipo bwana Hassan alipokuwa anapunguzia mzigo wake, sasa Hassan alikuwa anatembea barabarani huku anatathmini kila mwanamke anae pishana nae kama angemuona wa kumzidi yule alieingia hotelini na Kijana Abdulqadir, “haaa! huyu hawezi kutia mguu pale, ile mashine bwana” aliwaza Hassan akiwa anapishana na waschana mbali mbali na kuwa tazama makalio huku ana mfuko uliojaa mazaga zaga mkononi mwake.
Lakini wakati Abdul anatembea huku anawaza juu ya yule mschana na kuwatazama wengine sehemu za makalio mara akamuona mschana mwingine kama yule yule aliemuacha na mteja wake kule nyumba ya kulala wageni akija mbele yake, mwenye kimo na umbo kama lile tena amevaa vile vile na kujiziba niqab usoni, haikuwa ajabu kwa watu wa huku maana ni moja ya stara kwa wanawake, Hassan alimtazama vizuri yule mwanamke ambae alionekana akitembea kwa mwendo wa haraka sana huku akiwa mwenye wasi wasi mwingi akielekea mjini Chake Chake, yaani kule alikokuwa anatokea Hassan, hata alipopisha nae na kupiga hatua kadhaa akageuka na kutazama makalio ya mwanamke huyu, ni kweli na yeye alikuwa amefungasha, “siku hizi wapemba nao wamo” alijisemea Hassan, huku anatazama mbele anakoelekea, “na baada ya kutembea mita kama kumi mbele akageuka tena nyuma kwa lengo la kumtazama tena yule mschana, akihitaji kutazama tena makalio ya mschana yule mwenye kufanana na demu wa mteja wake aliemuacha kule guest house chumba namba kumi na moja.
Lakini ile anageuka na kumtazama yule mwanamke nae ndio wakati alikuwa anageuka na kama vile alikuwa anamtazama yeye, na macho yao yalipokutana yule mschana akatazama mbele haraka huku anaendelea kutembea kwa mwendo wa haraka sana, Hassan alitabasamu kwa ujinga wake wa kutazama makalio ya waschana, unajuwa haikuwa ajabu sana kwa mwanamke wa kisiwa hiki kuvaa kama vile kwasababu ni moja ya utaratibu walio ulithi toka kwa wakoloni wao ambao ni waarabu, pia hata dini yao inawashauri kuhifadhi miili yao, “duh! sijui demu amekolea mbona aligeuka kuni tazama?” aliwaza Hassan kisha akageuka tena na kumtazama yule mschana.
Naam Hapo Hassan akashikwa na mshangao mkubwa sana, maana hakumuona tena yule mschana, ina maana alishatoweka………… INAENDELEA.....
KIFO CHA HAWARA (mkono wa jini)
SEHEMU YA PILI
MTUNZI : MBOGO EDGAR
NAMBA: +255 743 632 247
ILIPOISHIA SEHEMU YA KWANZA : na macho yao yalipokutana yule mschana akatazama mbele haraka huku anaendelea kutembea kwa mwendo wa haraka sana, Hassan alitabasamu kwa ujinga wake wa kutazama makalio ya waschana, unajuwa haikuwa ajabu sana kwa mwanamke wa kisiwa hiki kuvaa kama vile kwasababu ni moja ya utaratibu walio ulithi toka kwa wakoloni wao ambao ni waarabu, pia hata dini yao inawashauri kuhifadhi miili yao, “duh! sijui demu amekolea mbona aligeuka kuni tazama?” aliwaza Hassan kisha akageuka tena na kumtazama yule mschana.
Naam Hapo Hassan akashikwa na mshangao mkubwa sana, maana hakumuona tena yule mschana, ina maana alishatoweka …ENDELEA NAYO SASA.....
Hassan akageuka kabisa na kutazama pengine alihisi ametazama kwa haraka ndio maana hajamuona yule mschana, lakini aliona watu wengine tu! ila mwanamke anae fanana na yule mschana hakuonekana kabisa, “mh! au jini nini?” aliwaza Hassan na kupuuza mawazo yake ya kutazama makalio ya waschana na kuelekea ofisini kwake.***
Naam Hassan alipofika pale ofisini kwake moja kwa moja akaufuata mlango wa chumba namba kumi na moja akatega sikio kusikiliza kinachoendelea ndani ya chumba hicho, lakini hakusikia chochote sio mlio wa kitanda wala miguno ya kimapenzi, hakajuwa kuwa waliopo ndani wameamua kujipumzisha baada ya kupeana dudu mzunguko wa kwanza, hapo akaamua kugonga mlango kidogo lakini hakupewa jibu lolote toka ndani zaidi ya harufu ya manukato, Hassan akagonga tena mlango akirudia mara kadhaa huku akiongeza nguvu ya ugongaji bila kupata jibu lolote, ndipo Hassan akahisi kuwa kijana Abdul atakuwa juu ya kitumbua lakini nje ya kitanda, hivyo akaona awape nafasi ya kufaidi na wakishamaliza lazima Abdul atamfuata mapokezi kuchukuwa mzigo wake.***
Lakini kwa mujibu wa bwana Hassan, yalipita masaa matatu bila kuona Abdulqadiri akija kuchukuwa mzigo wake, ndipo bwana Hassan Mohamed alipoamua kwenda kugonga tena mlango wa chumba namba kumi na moja ambapo hakukuwa na jibu wala dalili ya jibu toka ndani ya chumba hicho, Hassani katika maelezo yake akasema kuwa alipoona hivyo akajuwa kuwa pengine wateja wake wapo katika kupeana dudu, ukweli ni kwamba bwana Hassan licha ya kuwa ni tarishi wa muda mrefu pale hotelini, lakini alikuwa na kautaratibu fulani wakati mwingine ka kupiga chabo, akaona hiyo ndiyo njia itakayofaa kuangalia kile wanachokifanya wateja wake kwa muda mrefu namna hii, kwanza kabla ya kufanya hivyo akaanza kwa kutega sikio mlangoni kwa mara ya pili na kusikiliza ndani, ikawa kama mwanzo hakusikia chochote, hakukuwa na dalili ya uwepo wa watu ndani, “mh! ina maana alishaondoka kimya kimya, au?” alijiuliza Hassan, kabla hajapata wazo la kuzunguka nyuma ya nyumba hii ya kulala wageni ili akachungulie dirishani kuhakikisha kama wateja wake bado wapo ndani.
Sekunde chache baadae tayari bwana Hassan alikuwa amesha zunguka jengo la hotel hii iliyopo Madungu pembeni ya mji Chake Chake, kitu cha kwanza Hassan aliona kuna jiwe kubwa sana chini ya dirisha lile ambalo lilikuwa wazi, hakushangaa sana maana hakukumbuka kama mara ya mwisho alipokuwa anachungulia wateja wake kiasi cha siku nne zilizopita kama alilitoa au hakulitoa, hivyo akasimama juu ya jiwe pale kwenye dirisha la chumba namba kumi na mmoja ambalo dirisha na panzia lake lilikuwa wazi, hivyo ikawa kazi nyepesi kwa Hassan kuweza kuchungulia ndani ya chumba hicho pasipo kujiuliza kwanini dirisha lilikuwa wazi kiasi hicho, wakati aliwasikia wawili hawa wakikumbushana kulifunga kabla ya kuanza kupeana dudu.
Naam ile Hassan alipochungulia ndani ya chumba kile alishtuka na kujikuta akianguka kwa uwoga kubwa uliompata, “mamaaaaa!!” alipiga kelele Hassan huku anainuka na kujaribu kukimbia, lakini akajibwaga chini kwa miguu yake kukosa nguvu, maana alishtushwa na kuogopeshwa na hali aliyo iona mule ndani, ukweli ni kwamba japo Hassan aliweza kuona mwili wa mtu mweusi kama mkaa ukiwa umelala sakafuni, mwili wa mtu ambae ulikuwa na dalili nyingi sana za kuwa ni Abdulqadiri, nikutokana na zile ndevu na nguo alizovaa, lakini kwa sasa alikuwa amebadilika na kuwa mweusi kama alie banikwa kwenye moto mkali, usinge weza kuamini kuwa ndie yule kijana Abdulqadir ambae ni chotara wa kiarabu kabisa.
Hassan aliinuka haraka pale chini na kuanza kutimua mbio kuelekea barabarani huku anapiga kelele kama mtu aliechanganyikiwa, “Jini!! jamani jiniiii!” hivyo ndivyo alivyo sema bwana Hassan, akiamini kuwa Abdulqadir alikuwa ameuwawa kwa kunyonywa damu na jini, japo toka amefika hapa pemba hakuwahi kuona wala kutokewa na jini, tena aliamini kuwa jini mwenyewe ni yule mwanamke, ambao amesha wahi kusikia habari zao mara nyingi sana hapa kisiwani, ukizingatia, hakuonyesha dalili ya kuwepo mule ndani.***
Hassan alipofika barabarani alisimama kwa sekunde kadhaa, huku akipiga kelele za “jini jini” huku watu wakimshangaa, maana alikuwa anaendelea kupiga kelele kama Mtu anae weweseka, “jini !! jamani Jini” kwa wasio mfahamu kilichotokea wakajuwa kuwa Hassan ni chizi freshi, lakini ukweli lilikuwa ni tukio la kushangaza kwa Hassan alieamini kuwa Abdulqadir ameuliwa na jinni.
Baada ya dakika chache za kuweweseka ndipo Hassan akapata wazo la kwenda kituo cha cha polisi, na kituo cha polisi ambacho kilikuwa karibu yake ni kile cha polisi mkoa wa Chake Chake, yaani Madungu Polisi, ambacho kilikuwa mita chache toka pale hotelini, ambako alitoa taarifa ya kifo cha kijana yule ambae sio mgeni machoni na masikioni kwa wakazi wa Chake Chake, maana Adbdulqadir alikuwa ni mfanya biashara na muagizaji wa vifaa vya wakina mama toka nchi za falme za kiarab.
Naam polisi walifika eneo la tukio na kukuta mwili wa kijana Abdulqadir na kuanza uchunguzi wa kina, ambapo kwa msaada wa madoctor, waligundua kuwa kijana Abdulqadir amekufa baada ya kukaukiwa na damu, japo kulikuwa na utata mkubwa sana madoctor kushangazwa na ukaukaji ule wa damu kwa mtu ambae ameingia mwenyewe pale hotelin na kuja kukaukiwa damu na kufa mara moja, hapo kila mmoja alifananisha kifo hicho na vifo vingine kadhaa vilivyo wahi kutokea miaka ya nyuma, vifo vya aina hiyo hiyo vilivyo husishwa na jini wa kike anaehusika na vifo hivyo.***
“Lakini kuna mtu mmoja pekee anaefahamika kwa jina la Jonh Joseph, hakuridhika na maamuzi au imani ya wananchi na jeshi la polisi hapa kisiwani pemba kuwa kuna jinni anafanya mauwaji hayo, hivyo amekuja ofisini kwetu na kuomba tufanye uchunguzi wakina ili kubaini ukweli juu ya mauwaji hayo, na wewe ndie uliechaguliwa kwenda kisiwani pemba kufanya uchunguzi huo” alisema bwana, Winfred Mbogo, mkurugenzi wa kampuni binafsi ya upelelezi na uchunguzi, ya MSC (Mbogo Spy COM), alipokuwa anamaliza kunisomea simulizi nzito ya kusisimua na kutisha nikiwa nimekaa mbele yake ndani ya ofisi yake, tukutenganishwa na meza kubwa yenye vikolombwezo vya kila aina vilivyo ashiria kuwa hii ni ofisi, iliyopo mbezi mwisho jijini dar es salaam, “lakini mkurugenzi inawezekana vipi mimi nikaenda kumchunguza jinni?” licha ya kwamba hii ilikuwa ndiyo kazi yangu ya kwanza toka nirudi nchini toka masomoni na nilikuwa natamani kupata kazi japo moja nionyeshe uwezo wangu, lakini kwa jukumu hilo nilikuwa mbishi kidogo, ni kutokana na sababu ambazo nitakueleza mbele, japo ubishi huo haukuweza kuzaa matunda, maana amri ilikuwa ni moja tu kwenda kisiwani pemba kuchunguza kifo cha Abdulqadir, lakini kichwani mwangu nikipanga kuwa nitenda kuzuga ili muda upite kisha nirudi na kusema kuwa sijafanikiwa.****
Wapo waliopenda kuniita mvuvi wa nchi kavu, hasa wale niliokuwa nasoma nao shule ya msingi, secondary hata chuo kikuu cha dar es salaam nilikokuwa nasomea usalama wa nchi na mahusiano ya kimtaifa, nilipewa jina hilo kutokana na jinsi nilivyo weza kuingia kwenye mahusiano na baadhi ya waschana ambao walionekana kuwa ni wakipekee, labda kutokana na hali zao za kimaisha kuwa za juu sana au tabia zao za upole na kutokuhitaji mwanaume wa kupeana dudu pasipo malengo yoyote ya baadae, japo nina sifa ya kuitwa mpenda mademu au mzinzi kama wakina John Bonge wa NIZIBE MBOMO, au Edgar Haule wa kwenye MAMA MWENYE NYUMBA mimi naitwa Eric Frank, lakini huwa napenda kujiita mkono wa jini, yaani nisieshindwa kitu, jina nililojipati mwenyewe nikiwa kwenye moja kati ya vyuo vya kipelelezi nilivyo wahi kupitia, ikiwa ni sehemu ya kujinadi na kujisifu, japo sikuwahi kupata kazi ya kuchunguza yenye muonekano kama huu.
Yap, nimeona nikusimulie mkasa huu ambao ulitokea miaka kumi na nne iliyopita, yaani toka mwaka huu wa 2019, kipindi hicho nikiwa na miaka 25 tu! nina mwaka wa tatu toka nimejiunga na kampuni binafsi ya upelelezi wa siri hapa nchini, yenye makao makuu yake Mbezi Mwisho jijini Dar es salaam, huku rafiki zangu wengi wakijuwa kuwa nafanya kazi kwenye kampuni ya kuchapisha vitabu ya MSP COM, nikiwa kama fundi na mtaalamu wa kutengeneza compter, yaani hardwere na softwere, nikweli nilikuwa na uwezo mzuri katika vifaa na programe za computer, Kwa sababu katika mafunzo ya upelelezi na mapigano ya kujiami kwa mikono na silaha za jadi na zile za moto niliyo ya chukuwa kwa miaka mitatu toka mwaka 2002 mpaka mwaka 2005, katika nchi za Japan Cuba China na Israel, pia nilikuwa najifunza sana kuhusu internet tecnolog.
Japo ni muda mrefu umepita toka nipewe na kulifanya jukumu hili, lakini sidhani kama itakuwa vibaya nikikusimulia mkasa huu ambao ukiachilia kuwa ndio jukumu langu la kwanza kulifanya, baada ya kutoka mfunzoni, pia ni moja ya mikasa kati ya mikasa ambayo ilinisisimua sana na kunipa wakati mgumu, yaani kumchunguza jini.***
Ilikuwa ni tarehe kumi na moja ya mwezi wa tano ya mwaka 2005, ni kabla ya miezi mitano kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa raisi wa serikali ya muungano na raisi wa zanzibar, wabunge wa wakilishi na madiwani, Mida ya saa kumi na mbili za asubuhi ndio mida ambayo Meli kubwa ya MV mapinduzi ilipotia nanga kwenye bandari ya mkoani kusini Pemba, tukiwa tuna hitimisha safari iliyo nichukuwa takribani masaa kumi na saba toka bandari ya dar es salaam, ukweli muda wote wa safari nilikuwa sina amani moyoni mwangu, japo mimi kimuonekano ni mpole na hilo nalifahamu toka nikiwa mdogo, lakini safari hii upole wangu ulizidi mara dufu kutokana na kuhofia hii safari, na kitu kilicho nifanya nikose amani juu ya hii safari ni mambo matatu, moja lilikuwa ni kutokana na kipindi ninachoenda ambacho ni cha uchaguzi, maana nilikuwa naifahamu vizuri mikasa ya uchaguzi jinsi inavyo kuwa, hasa nikiangalia uchaguzi wa nyuma yake wa mwaka elfu mbili, ambao ulikuwa na habari nyingi za vurugu, na mwaka huu wa 2005 ulikuwa ni mwaka wa uchaguzi, na mbaya zaidi ni kwamba kulienea uvumi wa kuwa kuna watu wa kutoka Tanzania bara wameingia kule visiwani kuongeza nguvu ya chama fulani cha kisiasa katika upigaji wa kura, hivyo basi kila mtu mwenye asili ya kutoka bara kwa jina la utani (chogo), alishukiwa kuwa ni mmoja wa wanachama waliokuja kuvuruga uchaguzi,
Pili nilikuwa nahofia sana kuhusu habari za majini (jini), ukweli nilishawahi kusikia habari nyingi sana za mitaani kuwa Pemba kuna majini mengi sana, na kwamba unaweza kumuona mtu na ukaongea nae vizuri kabisa kumbe ni jini, na kwamba wakati mwingine majini hao wanaweza kukuchukia na kukudhuru bila sababu yoyote, au wanaweza kukupenda na kukung’ang’ania uwe mpenzi wake huku wakikupatia masharti magumu sana katika mapenzi yenu, na endapo utashindwa au kukataa kutimiza masharti yao basi cha moto utakiona, na ukichukulia mimi kama mimi sio kwamba najisifu, ila ukweli kutokana na jinsi nilivyo na muonekano wangu umesha wasumbua sana waschana wengi sana toka nikiwa shule, hasa kipindi tukiwa kwenye michezo ya shule za sekondari UMISHUNTA, nikiwa mchezaji wa Baskert ball, waschana wengi sana walipenda kuwa na mimi na kunitumia vijizawadi kama vile post card na mialiko ya matembezi ya pamoja, hivyo nilipata wasi wasi hawa majini lazima wange nipenda tu, lakini hiyo sio kesi sana, kesi ipo hivi.
Niliwahi kusikia kuwa kuna majini ya kiume ambayo hubaka binadamu wa kiume, yaani hapo ndipo nilipoiona dunia kuwa ndogo.na kulaani kazi hii ya upelelezi ambayo mwanzo niliiona kuwa inanifaa kutokana na kipato kikubwa, na sasa ndio najuwa maana ya ule mshahara wa milion moja na laki nane kwa mimi mfanyakazi wa miaka mitatu, wakati mfanyakazi wa kawaida alikuwa analipwa kiasi cha shilingi elfu tisini na nane mpaka laki moja na elfu tano ikiwa ni kima cha kati cha mishara, pia niliwahi kusikia kuwa unaweza kukuta kifuu au kitu chochote ukakipiga teke nacho kika kuuliza kwanini unanipiga, na hata ukikimbia ungekikuta mbele bado kinge kuuliza au kupatwa na matatizo makubwa, ukweli nilizidi kukosa amani.
Tatu, Kazi yenyewe ambayo nilikuwa naenda kuifanya ilikuwa unahusishwa na imani za kishirikina na majini, ilikuwa kazi yangu ya kwanza , zaidi ya hapo upelelezi nilikuwa na ufahamu ule wa kwenye vitabu pekee yaani chuoni, hakika iliniogopesha sana, maana niliamini kuwa kama ni kweli watu hao wameuliwa na jinni basi hilo jini tayari limeshajuwa kuwa kuna mtu anaingia pemba kwaajili ya kuchunguza mauwaji liliyo yafanya, na kibaya zaidi hakuna muhalifu ambae anamuacha salama mpelelezi anae mfuatilia, hiyo ndiyo moja ya kitu nilicho jifunza.***
Niliendelea kuwaza hata niliposhuka toka kwenye meli ya mv Mapinduzi kwenye bandari ya mkoani pemba ya kusini, ambapo niliweza kuona mandhari ya pemba jinsi ilivyo, kilicho ni shangaza na kuni vutia ni uvaaji wa wakazi wa kisiwa hiki ambao ni kama utamaduni kwa wanawake walivalia magauni marefu ya kupendeza huku idadi kubwa wakiwa ni waschana ambao wenye asili ya kichotara wa kiarabu, sema hawakuwa na maumbo makubwa kama walivyo kuwa wanawake wa Tanzania bara, yaani hips na makalio makubwa, vijana wa sasa wanaita msambwanda, ila sura zao zilikuwa ni nzuri na zakuvutia, ila sikuwa na uhakika juu ya maumbo yao kwa sababu walivalia magauni marefu na kuficha nywele zao kwa mitandio huku wengi wao wakiwa wamevalia mababuibui meusi, Kwa upande wa wanaume wengi walikuwa wamevalia kawaida, suruali mashati ya bila kuchomekea na viatu vya wazi, yaani sendos.
Nilikatiza kwenye geti la kutokea pale bandarini na kufika eneo la stendi ya magari yaendayo sehemu mbali mbali ikiwa pamoja na Chake Chake, Mtambilie Konde Wete yaani Pemba ya kaskazini, nikaungana na wasafiri wenzangu kuingia kwenye magari haya, ambayo huku tunaita dala dala, ambayo ukiachia mabasi madogo kama vile Toyota coster na Toyota hiace, pia kulikuwa na gari aina ya suzuk Center, ambazo zilitengenezwa bord yake kwa mbao, nalo kutumika kama gari la abiria, zamani tulikuwa tunaita chai maharage.
Nilifanikiwa kupata nafasi kwenye Toyota hiace, na safari ya kwenda Chake Chake ikaanza, ukweli sikuwa na raha hata kidogo, nilijikuta naichukia Pemba bila hata sababu, hata nilipokuwa naitazama barabara nyembamba yenye kona nyingi sana kali na za ghafla, huku nikishuhudia karafuu zikiwa zimeanikwa pembeni ya barabara, ghafla nikajikuta nikiichukia ile harufu ya karafuu, huku ule wimbo wa marashi ya pemba ukinijia kichwani na kujikuta na wenyewe nauchukia vibaya sana, nikiona kama unanisanifu, stori yetu ndio imeanza namna hiyo itakujia kila siku hapa hapa JamiiForums ukihitajia kumsapoti mtunz kwa chochote basi namba yake ipo hapo juu ... MUWE NA USIKU MWEMA