Kifo cha ferdinand ilikuwa sherehe ufilipino

kistwangara

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
656
195
NAKUSAHURI USOME KWA MAKINI SANA UJUMBE HUU UNA MAANA KUBWA SANA....

SIKU FERDINAND MARCOS ALIPOKUFA ILIKUWA SHEREHE YA KIHISTORIA NCHINI UFILIPINO.

Na Luqman Mloto.
Enzi nikisoma shule ya msingi, naikumbuka Kiezya Shule ya Msingi, asubuhi kwenye mchakamchaka tuliimba: “Idi Amin akifa, mimi siwezi kulia, nitamtupa Kagera, awe chakula cha mamba.” Wimbo ulikuwa na hamasa ya kuwatambua na kuwachukia maadui wa taifa letu. Tulikua tukilelewa kihisia kuhusu namna ambavyo Jenerali Idi Amin Dada alivyolitikisa taifa letu alipokuwa Rais wa Uganda. Amin aliivamia Tanzania kupitia Kagera. Alitangaza angeiteka mpaka Dar es Salaam ili kuiweka Tanzania kwenye himaya yake. Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere akawa hana uchaguzi zaidi ya kuliingiza taifa vitani, akatwambia:

“Tumebakiza kazi moja tu, nayo ni kumpiga. Uwezo wa kumpiga tunao, sababu za kumpiga tunazo na nia ya kumpiga tunayo.” Majeshi yetu yakaitikia kwa kauli moja yenye utii kwa Amiri Jeshi Mkuu: “Apigwe Nduli Amin, Apigweeee. Apigwe Nduli Amin, apigwee.” Pamoja na Tanzania kumpiga Amin, kumuondoa madarakani na kusimikwa kwa utawala mpya kwa baraka za nchi yetu, lakini haikusahaulika kuwa aliacha makovu kwa taifa letu kiuchumi na kimaisha kwa jumla. Wapiganaji wetu wengine walipoteza maisha na kujeruhiwa kwa kupata ulemavu wa kudumu. Ni hisia hizo zilizosababisha Watanzania wasiwe na upendo wala huruma kwa Amin. Tuliimba wenyewe kuwa Amin akifa tulikuwa na ofa nzuri kwa ajili yake, tungeuchukua mwili wake na kwenda kuutupa Mto Kagera ili mamba wakali wa mto huo, waufanye kitoweo murua. Amin alipopinduliwa alitorokea Libya kisha akaenda kuishi Saudi Arabia baada ya mfalme wa nchi hiyo kumpa hifadhi na mafao ya kutojihusisha na siasa. Alifariki dunia Agosti 16, 2003, Rais wa Uganda, Yoweri Museni alikataa asizikwe nchini humo. Akazikwa Jeddah, Saudi Arabia kama mtu wa kawaida.

SHEREHE ZA KIFO CHA MARCOS
Ferdinand Marcos alikuwa Rais wa Ufilipino. Aliingia madarakani Desemba 30, 1965, baada ya kuongoza taifa hilo kwa muhula mmoja wa miaka minne, mwaka 1965, aliweka rekodi ya kuwa kiongozi wa kwanza wa taifa hilo kuchaguliwa kwa muhula wa pili. Marcos hakuridhika kuchaguliwa kwake mara ya pili, alijiona yeye ndiye ‘Mungu wa Ufilipino’ kwamba anapaswa kutawala mpaka mwisho wa uhai wake. Ilipofika mwaka 1971, ikiwa imebaki miaka miwili amalize muhula wake wa pili na kukabidhi nchi kwa kiongozi mpya ambaye angechaguliwa, alianza mchakato wa kuivuruga Katiba. Alianzisha mchakato wa mabadiliko ya Katiba ili awe na ruhusa ya kikatiba ya kubaki madarakani atakavyo. Wananchi nao hawakukubali, walimpinga kila kona ya taifa hilo. Marcos alipoona Wafilipino wanamgomea, akaamua kuitawala nchi hiyo kijeshi.

Marcos alitumia kipengele cha dharura cha Katiba ya Ufilipino ya mwaka 1935 inayompa mamlaka Rais wa nchi hiyo, kutumia jeshi kama anaona kuna dalili za uasi. Tamko la Serikali ya Ufilipino namba 1081 la Septemba 23, 1972, liliitangaza Ufilipino kuwa nchi inayotaliwa kwa Sheria ya Kijeshi (Martial Law). Alifanya hivyo ili kuhakikisha anawafanya wananchi waogope, vilevile wapinzani wake warudi nyuma. Martial Law, utekelezaji wake ni kusimika maofisa wa juu wa jeshi katika nafasi muhimu za Serikali. Hivyo, Serikali ya Marcos Ufilipino baada ya tamko hilo, ilipambwa na mabosi wa jeshi. Hali hiyo ikasababisha kila wananchi walipompinga walikutana na sura za jeshi. Baada ya hapo, ukaitishwa mchakato wa mabadiliko ya Katiba. Vipengele vya ajabu vikawekwa. Januari 10-15, 1978, ikawa siku za kupiga kura za kuipitisha. Kwa vile aligundua watu wengi wanaweza kupiga kura za kuikataa, likatolewa agizo kuwa kura zingepigwa kwa sauti ya wazi kwa pamoja (viva voce plebiscite).

Maneno viva voce humaanisha tamko la sauti na plebiscite ni upigaji kura wa pamoja. Hii ndiyo mantiki kuwa viva voce plebiscite ni upigaji kura wa pamoja kwa sauti. Marcos aliamua Katiba ya mwaka 1973 ya Ufilipino ipitishwe kwa mtindo huo Mfano wa viva voce plebiscite kwa Tanzania ni vile ambavyo Spika wa Bunge au mtu anayekuwa na madaraka ya uspika, anapotaka kupitisha jambo bungeni, kwa hiyo anawauliza wabunge, “wanaoafiki weseme ndiyo” wabunge wanajibu ndiyooo, kisha anauliza “wasioafiki waseme siyo” wanasema siyooo, halafu anahitimisha: “Waliosema ndiyo wameshinda.” Wafilipino wakati wa upigaji kura, kila eneo walichomekewa maofisa wa jeshi katikati ili mtu atakayesema hapana aonekane. Matokeo yalipotoka, ilielezwa kuwa wananchi kwa asilimia 90 waliridhia Katiba ya mwaka 1973. Hata hivyo, Katiba hiyo ya utawala wa Kijeshi haikukubalika kwa wananchi. Maeneo mengi wananchi hawakupiga kura lakini iliripotiwa wamekubali Katiba. Mikutano ya pamoja ya wananchi kupiga kura za wazi kwa pamoja ilifanyika pia mwaka 1975, 1976 na 1978 ili kuihalalisha Katiba ya utawala wa kijeshi nchini Ufilipino.

VITIMBI VYA MARCOS.
Huyu mtu alikuwa mwonevu. Aliamini kichwa chake kuliko mtu yeyote. Alikuwa mbishi na jeuri, hakutaka kupingwa. Aliichukia demokrasia, hakutaka watu wawe na uhuru wa kutoa maoni, aliwachukia waandishi wa habari hasa walioandika habari ambazo hakuzifurahia. Marcos alipenda sana kuandikwa vizuri, kwamba alikuza uchumi wa nchi hiyo kuliko mtu mwingine yeyote.

Alijisikia raha alipoitwa mja aliyeshushwa kutoka mbinguni (the heaven sent) kwa ajili ya kuwakomboa Wafilipino. Alipenda kusifiwa, aling’ata meno alivyokosolewa. Wakati wa kuithibitisha Katiba ya mwaka 1973 Mahakama Kuu, Marcos alitumia mtindo wa carrot or stick, yaani uchague zawadi au adhabu. Carrot or stick ni msemo wenye maana kuwa una mamlaka ya kuchagua lakini unaambiwa ukifuata matakwa ya mtawala unapewa zawadi na ukienda kinyume kuna adhabu. Mahakama Kuu ilibidi iithibitishe Katiba hiyo ili kukwepa adhabu kisha majaji wakapata zawadi.

Wakati wa mchakato wote, zaidi ya watu 8,000, wakiwemo maseneta, wanafunzi, waandishi wa habari na viongozi wa wafanyakazi, walikamatwa na kuwekwa ndani pasipo taratibu zozote za kuwafikisha mahakamani. Chuki ya Marcos kwa vyombo vya habari ilikuwa wazi, maana aliviona vina kiherehere. Septemba 22, 1972, Marcos aliandika barua ya agizo la Rais Namba 1, akimwagiza Waziri wa Habari na Waziri wa Ulinzi, kudhibiti shughuli zote za vyombo vya habari. Kwamba Waziri wa Habari na Waziri wa Ulinzi, wanapaswa kufuatilia kila kinachofanywa na vyombo vya habari, kuruhusu yenye kuipendeza Serikali na kuzuia yasiyowafurahisha watawala. Katika hali hiyo, waandishi wa habari na wachambuzi waliokuwa wakijiweka wazi na kumkosoa Marcos, Serikali na hata familia yake, walichukuliwa na kuwekwa kwenye kambi za jeshi kisha walipewa mateso bila kufunguliwa majadala ya mashtaka. Wachache walioonja joto la jiwe ni Joaquin Roces, maarufu kama Chino Roces, huyu ni mwanzilishi wa gazeti kongwe Ufilipino, Manila Times.

Eugenio Lopez Jr ambaye alikuwa mmiliki wa gazeti la Manila Chronicle ambalo Marcos alilifuta jumla. Wengine walioonja machungu ya Marcos ni wachambuzi Max Soliven na Luis Beltran. Unyanyasaji wa Marcos kwa vyombo vya habari ulikuwa mkubwa, Alitoa Maagizo 11 ya Rais (11 Presidential Decrees) kwa vyombo vya habari, wale walioonekana wanakiuka miongozo iliyotolewa, walishtakiwa, walifungwa, waliteswa na wengine walilazimishwa kujiuzulu fani ya uandishi wa habari.

AKILI NDOGO ZA MARCOS
Aliamini kuwa kuwadhibiti wapinzani na vyombo vya habari ndiyo ataweza kutawala salama lakini matokeo hayakuwa hivyo. Kadiri alivyotumia nguvu ndivyo na vitendo vya uasi vya wananchi dhidi ya Serikali yake ya utawala wa kijeshi viliongezeka. Uasi ulipokuwa mkubwa hakujiuliza anakosea wapi wala hakuona umuhimu wa kuwapa wananchi uhuru waliouhitaji, suluhu aliyoiona ni kuongeza udhibiti, matokeo yake machafuko yakawa mengi. Kikundi cha ukombozi wa kitaifa (MNLF) kilianzishwa na kupata hamasa kubwa. Wanafunzi na wanasiasa wengi walijiunga MNLF kumpiga Marcos ambaye alitumia majeshi kudhibiti. Zaidi ya watu 13,000 waliuawa katika uasi huo, watu zaidi ya milioni moja walipotea katika mazingira ya kutatanisha.

Ilifikia hatua, Serikali ya Rais Marcos ilikuwa inatumia zaidi ya dola za Marekani milioni moja (kwa sarafu ya sasa ni Sh2.2 bilioni) kila siku ili kupambana na uasi huo. Hali hiyo, ikawa mtaji mkubwa kwa Chama cha Kikomunisti cha Ufilipino (CPP) ambacho kilipata uungwaji mkono mkubwa. Kutokana na harakati nyingi za wananchi kutaka uhuru wao, pamoja na wasiwasi mwingi aliokuwa, Marcos alianza kudhoofika kiafya.

Marcos aliripotiwa kuumwa kisukari na shinikizo la damu. Awali ilifanywa siri lakini baadaye iligundulika kuwa mzee wa utawala wa kijeshi Ufilipino hali yake ni dhaifu.

LIKACHOKOZWA JAMBO
Agosti 21, 1983, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Manila, aliuawa aliyekuwa Kiongozi Mkuu wa Upinzani, Benigno Aquino Jr, maarufu kama Ninoy Aquino. Marcos alihisiwa kumuua Ninoy kwa kutumia wanajeshi wake. Wengine walimtaja Imelda Marcos, mke wa Marcos kuwa ndiye alimuua Ninoy kwa sababu mwanamke huyo alikuwa na mipango ya kuwa Rais wa Ufilipino, baada ya kuona afya ya mume wake ni dhaifu. Ilikuwa hivi; Ninoy akiwa jela alikowekwa kwa amri ya Marcos, alipata matatizo ya moyo, baada ya kutibiwa na kushindikana, ilibidi asafirishwe kwenda Marekani kwa matibabu.

Ilidhaniwa kuwa Ninoy asingepona. Taarifa za Ninoy kufanyiwa upasuaji wenye mafanikio ziliwafikia Wafilipino. Hali yake ikiwa inaendelea vizuri huku akiendelea kuishi uhamishoni ilielezwa, ilitangazwa pia taarifa za kurejea nchini mwake. Ndipo siku alipowasili uwanja wa ndege akapigwa risasi na kufariki papohapo.

Kuanzia hapo wananchi wa Ufilipino walianza vuguvugu la mapinduzi, wakidai Marcos ajiuzulu na kujibu mashtaka ya kumuua Ninoy. Serikali ilipata wakati mgumu kudhibiti wananchi wenye hasira. Shughuli za maendeleo zilisimama na fedha nyingi ambazo zilikuwa zinamwaga kudhibiti wananchi, zilisababisha uchumi uyumbe. Hali iliendelea kutokuwa shwari mpaka ukawadia Uchaguzi Mkuu 1986.

Marcos kama kawaida alijitosa kwenye uchaguzi pamoja na afya yake kuwa dhaifu. Baada ya Ninoy kuuawa, nyota ilimdondokea mkewe, Corazon Aquino Corazon ‘Cory’ ambaye aligombea kwa kuungwa mkono na wapinzani wote. Matokeo yalitangazwa kuwa Marcos alishinda kwa kupata kura 10,807,197, wakati Cory aliambulia 9,291,761. Hata hivyo, taasisi huru ya uchaguzi (Namfrel), ilieleza kuwa matokeo hayo ni udanganyifu wa Marcos na usahihi ni kuwa Cory alipata kura 7,835,070, wakati Marcos aliambulia 7,053,068.

Ripoti hiyo iliwakera wananchi na kwa sababu walikuwa bado wana machungu ya kuuawa kwa Ninoy, maandamano makubwa yalifanyika, maelfu ya Wafilipino waliingia barabarani kuanzia Februari 22-25, 1986 na kufanikisha Mapinduzi ya EDSA (People Power Revolution). Marcos akaondolewa, Cory akawekwa madarakani.

MWISHO WA MARCOS
Marcos alikimbilia Marekani na kuweka makazi yake Honolulu, Hawaii. Wakati anatoroka alikuwa ameshaiba fedha nyingi mali za Wafilipino, kwa hiyo hata baada ya kuondoka madarakani, aliishi maisha ya kitajiri na Rais wa Marekani wakati huo, Ronald Reagan alimhakikishia usalama nchini humo. Moja ya simulizi ya kushangaza ni kuwa mke wa Marcos, Imelda, wakati anatoroka na mumewe, alifungasha pea za viatu zaidi ya 2700. Kwamba Imelda peke yake alikuwa anamiliki viatu vingi kiasi hicho.

Fanya yote mwisho utafika, Marcos aliendelea kuugua pamoja na utajiri aliokuwa nao. Alipata matatizo ya ini na oparesheni mbili za kupandikiza ini jipya zilifeli. Nyakati za mwisho za uhai wake, Marcos alitamani kufia nyumbani kwao Ufilipino lakini alikosa fursa. Mwanzoni mwa mwaka 1989, aliyekuwa Makamu wa Rais wa Ufilipino, Salvador Laurel, alimtembelea Marcos ambaye aliomba kutoa asilimia 90 ya utajiri wake wote kwa Serikali ya Ufilipino ili aruhusiwe kumalizia uhai wake nchi humo na azikwe jirani na kaburi la mama yake lakini alikataliwa.

Bora Watanzania walitamani mwili wa Idi Amin ili wautupe Mto Kagera aliwe na mamba, Wafilipino hawakutaka kabisa kuuona mwili wa Marcos. Wananchi walipaza sauti kupinga mpango wowote wa Marcos kurudi nchini humo na kuishi maisha kama raia wa kawaida. Septemba 28, 1989 Marcos aliaga dunia. Habari za kifo chake ziliibua sherehe kubwa Ufilipino. Watu walikula na kunywa kwa fujo, kwao kifo cha Marcos kilikuwa tendo lenye baraka kubwa kwa taifa lao.

Juhudi mbalimbali za kuuhamisha mwili wa Marcos Honolulu na kuzikwa upya Ufilipino ziligonga mwamba. Mwaka 1993, ilikubaliwa kuhamisha mabaki ya mwili wa Marcos kutoka Honolulu mpaka Ilocos, Ufilipino lakini tendo hilo lilizua maandamano makali. Wafilipino hawakutaka kabisa ardhi ya nchi yao ihifadhi kiwiliwili cha Marcos.

Novemba 18, mwaka huu, mabaki ya mwili wa Marcos yalihamishwa kutoka Ilocos mpaka Manila kwa siri na kuzikwa kwenye Makaburi ya Mashujaa wa nchi hiyo. Tukio hilo lilifanywa kwa siri na helkopta za kijeshi. Hii ni kwa sababu wananchi walikuwa na hasira mno mtaani. Hawataki kuona Marcos akitambulika kama shujaa. Kaa na hii; Uongozi unaweza kuwafanya wananchi wako wakupende na kukuenzi hata baada ya kuondoka madarakani. Ukiwatendea ndivyo sivyo, watakuchukia na hawatataka kukuona kama ilivyokuwa kwa Marcos.

Si kwamba Marcos alikuwa kiongozi mbaya kwa asilimia 100, wakati wake miaka ya 1970, aliweka rekodi ya kukuza uchumi wa taifa hilo kwa kasi ambayo haijawahi kutokea. Ila alipowanyima uhuru wananchi, akaminya uhuru wa vyombo vya habari na kuwadhibiti wapinzani alijiharibia. Uchumi wote ambao alisifiwa kuukuza, uliporomoka na kuiacha Ufilipino ikiwa hohehahe kwa sababu ilimlazimu kutumia fedha nyingi kudhibiti uasi dhidi ya Serikali yake pia wakati wa mapambano ya uasi shughuli za kiuchumi zilisimama. Umuhimu ambao Marcos hakuujua; Uhuru na demokrasia ni hitaji la kwanza la wananchi kisha uchumi na maendeleo yao kwa jumla hufuata. Ukiwapa watu maendeleo na kukuza uchumi wao vizuri kisha ukawanyima uhuru na demokrasia, watakupinga tu. Wataiasi Serikali hata kama kwa kimyakimya.

Wakoloni hawakupingwa kwa sababu za kiuchumi bali kwa madai ya uhuru. Watu hutaka kujitawala wenyewe kisha wajione wapo huru. Ukimlisha mtu pilau na vinywaji vya thamani kubwa lakini umemfunga mikono na miguu, atatamani uhuru kuliko pilau yako. Nasisitiza: Uhuru na demokrasia ni hitaji la kwanza.

Ndimi Luqman Maloto

Karibu sana:

mama chupaki

JF-Expert Member
Aug 23, 2015
906
1,000
Aisee tumejifunza jambo hapo ,bila kuwa na uhuru hata furaha na amani nayo hatakuwepo.
 
longi mapexa

JF-Expert Member
Jul 18, 2015
2,795
2,000
bado nawatafakari wale walio mpigia kura Marcos takriban 7058.....

nawafananisha na wale wala viwavi......
 
Hwasha

JF-Expert Member
Aug 22, 2015
1,271
2,000
Mmmmh haya bhana

Mchango mzuri,tuletee na historia ya maisha ya Mabutu Seseko,Kamuzu Banda na mwisho wao. Nikuombe nikumbushe na historia ya Mkwawa wa Iringa. Tanzania tunajua tunawaagaje viongozi wetu bila kujali wako hai au wafu.Rejea kustaafu na kifo cha J.K. Nyerere na kifo cha Waziri Mkuu wetu Edward Moringe Sokoine.Pima utendaji kazi wao kama uliwafurahisha wote linganisha na matokeo ya wengi kwenye mazishi yao.Hiyo ndiyo JMT, ina mengi ya kuufundisha ulimwengu si Ufilipino tu.

Nayalinganisha maisha ya mama yetu Maria Nyerere mumewe wapo waliomwita Musa na wengine wakasema anaitwa Haambiliki nayafananisha na maisha ya tuliye naye leo,sioni ndoto ya kumwona akiikimbia Tanzania baada ya muda wake kwisha.Najiuliza unaweza kuthubutu kumfanyia chochote na watanzania wakakuangalia tu hadi ije polisi au jeshi jibu langu ni hapana.Analindwa na MUNGU na watoto wake waitwao watanzania.

Napitia maandiko ya neno ninaloliamini likinipa hiostoria ya safari ya Waisrael kutoka Misri kwenda Kaanani sioni tofauti ya manunung'uniko yao na baadhi yetu.Napima idadi ya wapelelezi 12 waliotumwa na Musa na taarifa walizomletea.

Nachagua kuwa upande wa Joshua na Kaleb maana peke yao wa kizazi chao ndiyo waliofika Kanani.

Tutashinda hatutashindwa kwa kumtegemea MUNGU aliyeziumba mbingu na nchi kwa kutumia akili alizotupa.Hatutategemea akili za wengine wala maarifa na matakwa yao maana hakutuumba raia wa daraja la pili Duniani kama baadhi yetu wanavoota.

Hatutaruhusu kila ujinga ili tuuonekane wana Demokrasia,asili ya uasi wa shetani ni kutaka afanane na MUNGU japo alipewa daraja la juu la mamlaka hakuridhika.

Tutasalia Taifa linalosikiliza MUNGU anataka nini na siyo binadau anataka nini.Tutaheshimu,kuwatunza na kuwajali wajane,maskini,yatima na wasiojiweza.Hatutazitumikia fedha bali fedha zitatutumikia.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom