Kifo cha CCM kimetimia

Mtabaki kama fisi akiusubili mkono wa binaadamu uanguke wakati hauanguki kamwe. Na mwisho wa upinzani 2015 anaebisha aangalie tu
 
Yaaani katika post zilizotumwa humu ambazo ni za kipuuzi sijaona kama hii ya sir R utabaki na labda mpaka yesu arudi
 
Mtabaki kama fisi akiusubili mkono wa binaadamu uanguke wakati hauanguki kamwe. Na mwisho wa upinzani 2015 anaebisha aangalie tu

Mkuu, fikiri mbali zaidi, kwa nini unadhani kwamba ni upinzani tu ndio wenye matarajio ya kuiangusha CCM?

Kama unaijua vema historia ya TANU hadi kuzaliwa CCM 1977 na maendeleo yake hadi hivi sasa, mahali pengine huhitaji kuufikiria sana upinzani kama kaburi la chama hiki. Mchawi wa chama hiki ni wanachama wao wenyewe na jeneza lao wanatengeneza wenyewe, hata misumari watapigilia wenyewe!

Kwa hiyo hao wapinzani na wengine wasiokuwa na vyama ni wasindikizaji tu wa msiba huu. Kama unayo historia japo kidogo tu, ilikuwa huwezi kukijadili hiki chama hadharani hivi na ukabaki salama! Leo kimeingiliwa hadi chumbani, tena na wanachama wao wenyewe.

Inaonyesha ni kwa kiasi gani watu wamepoteza imani na ni kwa kiasi gani chama kimepoteza nguvu. Ni kama simba mzee anayetegemea mngurumo wake kumkimbiza adui ilhali kucha na meno yameshang'oka.

Mimi sio adui wa CCM, ila ndio tulioilea TANU Youth League hadi CCM yenyewe mpaka hapa ilipo; lakini hatuwezi kukimbia kivuli chetu wenyewe. Mchawi wa CCM ni CCM yenyewe!
 
Sayuni toka cdm na cuf mpaka leo hii nani? Kaziongoza hizo ngo kama c hao yaani wapo kama mugabe vile na zimbabwe
 
Ni kweli alafu wanajifanya eti wanataka kuwakomboa watanzania kumbe wanataka kukomboa matumbo yao. Tia mguu ugombee uenyekiti au ukatibu sasa hivi utaitwa msaliti
 

Kwani JK atagombea tena au kuna JK mwingine aliyetangaza nia?
 
mkuu una moyo sana,miaka 15 ?ili awe delete kufanya nn nchi hii,mchakato huu wa katiba mpya ndiyo sanda ya kuizikia ccm,wewe acha waendelee kujifanya viziwi
 
wewe una kisirani tu na umekata tamaa kaa kando acha wenye point za maana waongee
 

Kwani Jakaya anagombea tena?
 
Wana jamvi utabiri wa kifo cha ccm alio wahi kuutoa mwalimu nyerere unaelekea kukamilika,dalili zote zipo wazi maana laana za wazee waasisi wa ccm akina mzee warioba na butiku zinakwenda kukiangamiza ccm,laana za wasomi waaminiefu na weledi prof kabudi,prof mpangala na dr lwaitama sasa hakuna shaka ccm bye bye! Lakini kubwa zaidi kitakacho imaliza ccm kabisaa ni kiburi na dharau kubwa wanayo ionyesha kwa wananchi kwa kupinga na kuyakataa maoni yetu watanzania hii ni dharau kubwa na kiburi kilicho pitiliza,ni kawaida yao hata mtwara wananchi walidharauliwa na kulazimishwa kukubali wasicho kubali,hakika washauri wa ccm mnakimaliza chama chenu miaka 2 ijayo itabakia ccm,ahsanteni sana nimalizie kwakusema kidumu chama chamapinduzi jibu ni kimetobokaaa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…