Wana jf
Kwa mtazamo wa haraka haraka, nimefuatilia midahalo mawili juu ya mchakato wa katiba. Mdahalo ulioandaliwa na Rosemary Mwakitwange last weekend pale Serena hotel na mdahalo ulioandaliwa na chama cha wanasheria Tanganyika. Wakati midahlo hii ikiendelea utaona kabisa mihemuko na jazba za washiriki juu ya chama tawala. Hata pale washiriki toka chama tawala wanapopata nafasi ya kuzungumza hujikuta kwenye wakati mgumu. Tulimshuhudia mh. Wasira akipata wakati mgumu kila alipojaribu kujibu au kutetea hoja, leo pia tumeshudia baadhi ya wawakilishi wa ccm wakipata wakati mgumu. Hizi ni dalili mbaya kwa watawala, ni vyema sasa wakasoma alama za nyakati waache kufanya shingo zao ngumu.