Kifo cha CCM kimetimia


Wala CCM haihusiki na matatizo ya CHADEMA,Matatizo ya CHADEMA yanasababishwa Viongozi wa CHADEMA wasiopenda demokrasia ndani ya Chama.Yule Mwigamba anayeitwa kirusi tuhuma zake zilikuwa na ukweli mtupu kwani hata akina Mnyika walipojaribu kuyatolea majibu walijikuta kila mmoja akiongea lake,Mnyika akikubali kiaina na Dr Slaa akikataa na hivyo wakijikuta wakijivua nguo zaidi so tuhuma zote za Mwigamba zilikuwa za kweli kwamba Uongozi wa sasa umejaa uozo mtupu.
 
Kwa nini msimkabidhi nchi mchungaji Mtikila 2015...??? maana anajiamini, ameokoka, hana unafiki, anaifahamu vizuri historia ya nchi hii na ana uzalendo na nchi hii.
 

Hizo highlighted mkuu
1. nimesemea hoja zako kwa maana kwamba unaona na kukubali kuwa ccm ina matatizo hivyo inahitaji mbadala
2. kweli ccm na genge lake wangependa kuwa ktk system forever kwa maana ya wao sasa na watoto wao baadaye ila kwa duniani na historia za vyama haiwezi kuwa milele isipokuwa labda iwe km kanu ya kenya ambayo iko madarakani kwa form nyingine, so nakubaliana na wewe kuwa kwa sasa chadema ndiyo mbadala lakin kuna matatizo ya organization
3. tabia za binadamu ziko nyingi na kila moja ina umuhimu wake, kwa mbunge msingi ni hoja bila kujali ametoka kijiweni au hata tukienda mbali amepigiwa kura na watu gani kwa maana ya socio-economic status zao. zito na wengine wanaihujuma chadema hadharani na bado ni wanachama nikasema ni kwa sababu hoja yako kuwa chadema hawajajipanga ina ukweli na katika hilo usimpe exception zito maana na yeye ni moja wa viongozi wakuu wa chama, labda hatujaelewana, ni kuwa zito anaihujuma chama au chama kwa kupitia mbowe na slaa wanamhujumu zito?
 
1. Kawaida kwa Wabunge wake huwa wanapinga mambo yenye maslahi kwa Taifa mfano mzuri ni lile la muswada wa mabadiliko ya Katiba, tozo ya line za simu na mengine mengi mpakaa wabanwee sana ndo wanageuka na kuunga hoja mia kwa mia


2. Wabunge wao walio wengi akishachaguliwa na wananchi kurudi jimboni ni mgogoro kwa mwaka anaweza akaenda jimboni mara moja au asiende kabisa


3. Katika uchaguzi mkuu 2010 zilitolewa ahadi nyingi zikiwemo zile za ununuzi wa meli ziwa victoria, tanganyika, nyasa, treni ya mwendo kasi Dar Kigoma na zingine kadha wa kadha , hayo yote hayaonekani

4. Maisha bora kwa kila Mtanzania walihaidiwa wananchi , ni kama vile hayapo kwa hali ilivyo sasa

5. Madini yanachimbwa na kunufaisha wageni wakati watoto wa shule wanakaa 200 ndani ya chumba kimoja cha darasa, wengine wanakaa chini, na walimu hawalipwi vizuri na wengine wanadai madai yao miaka nenda rudi wala hakuna anayewasikiliza
6. Serikali ya CCM inasema ajira kwa vijana lakini ukweli mpaka sasa vijana wanaomaliza vyuo wapo wamejaa mtaani wala hakuna ajira

Hayo ni machache tu CCM na serikali yake ni ya Kilaghai
 
Ulikosa mada yakuleta! Kodi ya cm imehamia ktk magari ama wewe huna gari, hebu kalipie lesen yagari TRA uone. Sijui ulikuwa na maana gani. Wabunge walisema posho ni ndogo iongezwe. SAWAAAA!!!!? :
 
Co maccm tu WAZALENDO, wacotaka ujinga, bunge la wabunge la mwafrika baa ndilo lenyefikra hizo, wajumbe wake ni wale wanakula kwa shkamoo kulala jirani na ba na ma. Ndio asli ya kutoijua Inchi hii, imeanzia wapi, hao walojaa kula pesa ktk tenda za UMMA halimashauri za miji na majiji kna nan? Jibu hapo. Duka vifaa vya ujenzi, gareji za magari kampuni za ujenzi ktk HALIMASHAURI, ni nani huku kwetu hakuna hata mgoni ni huko kaskazn tu kila kitu wao, halafu wanajisahau. Hebu vyama vyote viunde tume ya pamoja vifanye uchunguzi kama mali yote ya UMMA haitakutwa kwenu.
 
Umekurupuka siasa Uhuru ni wa chama gani kama co KANU. MASAWE, KIMARO, MUSHI NI WA ENZI NA ENZI NA WATAENDELEA KUWEPO NA KANU IPO HAITAKUFA. CDM MLIKUJA KENYA KUSAIDIA LAKINI HAMKUFUA DAFU. Huko kwenu mtadanganya hao wavivu wasiopenda kufanya kazi nakuwafanya kuiba tu. NI KENYA KWANZA Siasa baadaye. Mtu wa siasa ni mwongo sana. Mtz angalia cv ya mtu anayetaka siasa co kutazama chama, kuna maharamia wengi ktk vyama wengine unawezakuta mtu hatari sana anajificha kwa siasa
 
Heri uugue malaria utatibiwa na kupona kuliko kuibiwa na kudhurumiwa na watu wanaojinadi kuwa wanakupenda. Heri uugue ukimwi na ukafahamu maana utatumia dawa za kuimarisha CD4 na ukaendelea kuishi kuliko kuwa unaambikwa mijikesi ya jinai na ugaidi ili kukutisha usiipinge ccm. Anayeshabikia ccm huyo huyo nae ni hatari kuliko maradhi yanayoweza kutupeleka hospitali...


Tuwasubiri hapa waje wabaya wetu, hao hao ninaowasema ni hatari, YAANI HAO CCM...
 
Huoni aibu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…