Kifo cha CCM kimetimia

Hii ni kutokana kuzuia watu kuhudhuria mikutano ya Chadema,huku mkiwatishia kufa. Watu wamewachoka na hawawataki tena...kwa nini mnalazimisha mkubalike? Umaarufu wenu ulishaisha...kwa nini mnalazimisha umaarufu? Umaarufu haulazimishe bali huja kulingana na jinsi unavyo timiza matarajio ya watu.
Sasa hivi,kila kukicha ni mabomu...watu wameshazoea mabomu kwa sasa na wanaona kama mlio wa pancha tu. Uhalali wenu wa kutawala haupo kwenye mioyo ya watz,kwa nini mnalazimisha? Kama mtaendelea na utaratibu huu wa kulazimisha kutawala hakika tunakoelekea ni hatari kubwa.
 

Jipeni moyo
 
Katika hali ya kusikitisha na ya kuhuzunisha,ccm wapo kama hawapo kuanzia mwenyekiti,makamu mwenyekiti,katibu mkuu na viongozi wengine wandamizi pamoja na wanachama wote.Mfano,niliwahi kushuhudia KIONGOZI FULANI KATIKA CHUO KIKUU FULANI,ALIWAHI KUSEMA HIVI,WALE WANACCM NAOMBA TUONANE HAPO NJE,NILISHANGA KUSIKIA WATU WANACHEKA,nikauliza kulikoni? Watu wakasema,haaa kumbe kuna wanaccm,nikauliza kwani nini tatizo, watu(wanafunzi) wakajibu ni aibu..kwanza wanaona aibu kusema kuwa ni wanaccm,hii ni dhahiri kuwa watu kuzungumzia ccm basi yuko chumbani na mke wake na sio mbele ya kadamnasi imekuwa ni aibu na kuonekana kuwa wewe ni mshamba.
Kwanza kabisa nawapa pole kwa dhahama inayokuja ahead of you.Nikitafakari jinsi viongozi na wanachama wa ccm,wanajipa matumaini ya kushinda chaguzi zilizoko mbele yao.Hii ni hatari sana,wamekaa wamebweteka hawajishughulishi na mambo yoyote ya chama,wabunge wake wakitoka kwenye vikao Vya Bunge Dodoma ni kwenda Dar kubweteka huku wakiwasahau wapiga kura wao wakitegemea ushindi kwa kuwapa kanga,t.shirt,kofia na pombe.Hizi ni siasa zilizopitwa na wakati.
Chukulieni mfano,CHADEMA wamekuwa wakizunguka nchi nzima kuongea na wananchi lakini CCM mmejiridhikia tu..mkiamini kuwa mtakuja kushinda,mnajidanganya! Inapotokea mmeshindwa ndio hapo mnaanza kurusha mabomu pamoja na kuiba kura ili muonekane kuwa ni washindi.Huu uvivu wenu wa kufikiri usituletee machafuko.Na hatuko tayari kuvumilia,yaani nyinyi mkae tu..halafu mwisho wa siku mtake kuwa washindi.Hapatatosha kwa kweli.Mabomu unipige,kesi unifungulie mwenyewe niliyepigwa,wananchi niwaelimishe mwenyewe halafu mwisho wa siku utake ushindi...nasema siku hiyo hapatatosha.
Nawashauri,japo hata kushauriwa hamtaki kwa kuwa mmevaa miwani ya mbao na kuweka pamba masikioni,zungumzeni na wananchi mjue wanataka nini,lini,wapi na kwa wakati gani..ili mtimize matakwa ya wananchi,bila kufanya hivyo mtawamaliza watu kwa mabomu yenu,watu wamepoteza matumaini kabisa.Huwezi kuwa na marketing strategies kama hujui wateja wako wanataka nini.Hapa lazima business fall down.Pili,acheni matumizi makubwa ya vyombo vya dola..kwa kuwa mnajenga chuki kati ya serikali na wananchi.Tatu,acheni siasa za matusi,kejeli na dharau kwani zinawaangusha mno.Nne,Nchemba na Nape sio brand nzuri ya chama pigeni chini.
Ni maoni yangu
 
Nimependa hapo, "HUU UVIVU WENU WA KUFIKIRI USITULETEE MACHAFUKO'' to me its a punch line.
 
nasikia raha sana ccm ya kikwete lowassa,makamba, akina chenge ikifa kifo cha mende
 
Awali ya yote nishukuru JF kunipokea jamvini.

Kwa muda nimekuwa nafuatilia siasa za CCM, na sasa nimeamini kuwa CCM kama chama cha siasa, ilishakufa miaka takribani kumi iliyopita na sasa ni masalia yanayomalizikia.

CCM imekuwa kama genge la watu wenye malengo fulani huku wakitumia jukwaa la siasa kufanikisha mambo yao.
Siasa anazofanya Mwigulu zingefanyika kabla ya facebook na mchina kutengeneza kila simu na facebook

Kwa speed ya Mwigulu, CCM haichukui miaka miwili unless abadilishe kabisa strategy zake (Siasa za matusi, uzushi,Kumwaga damu za watu kwa lengo fulani, kuwatishia wananchi kama wewe ndo wa milele, unrealistic debates, , siasa za kueneza chuki, udini, kuvuruga amani yetu hivi hivi mbele ya watu wa usalama na badae kusema CHADEMA ndo wanavuruga amani!!!!!!!.

Mimi naona kwa bali Mwigulu, Nape, Kinana, Serikali, na Vyombo vya ulinzi na usalama, wote kwapamoja na kwa speed kubwa wanapeleka katiba na makabrasha ya CCM makumbusho ya taifa na maktaba ya taifa.

Mimi nikiangalia kwa mbali naona CCM imebakia makumbusho na maktaba ya taifa!. Let us wait and see the very death of CCM 2014-2015,June.

Ushauri:CCM inauliwa na viongozi wake. Kupona kwake,lazima wachague moja kati ya biashara safi na siasa au biashara chafu bila siasa.
 
Nani kakwambia mwigulu ndio ccm inawezekana ni mnyonge wenu hukuhuku jf tu na atawatoa maji ya mkakio msipojistukia ccm oyeeeeeeereeeeeeeee :yield:
 
Watakuwa na bahati sana hata huko makumbusho wakipewa hifadhi. Kwa niaba yao tutaweka kumbukumbu za TANU na ASP siyo CCM!?
 
Watu kama nyinyi ndiyo mnaichinja cdm kwa kuwakuza. Badala ya kuwaambia wakomae unakuja kujambajamba hapa JF. Ccm haifi leo wala kesho na cdm kuongoza hawawezi....
 
Mbuzimtu nakwambia hawa watabaki kama kile chama cha majirani zetu Kenya walioizika KANU na kubakiza historia yake tu!
 
Last edited by a moderator:
itabakia makumbusho kwa siasa za kwenye keyboard na kujipiga mabomu wenyewe?
 
Nani kakwambia mwigulu ndio ccm inawezekana ni mnyonge wenu hukuhuku jf tu na atawatoa maji ya mkakio msipojistukia ccm oyeeeeeeereeeeeeeee :yield:

Leomimi,
Kama Mwigulu sio CCM ukizingatia ufront front wake kwenye siasa za maji taka na hatari kwa taifa letu basi CCM kama ipo inatakiwa kubadilisha strategy yake haraka sana lazivyo watajuta 2014-2015. Kwa siasa za mwigulu CCM lazima ife tu!!!.

Utakubaliana nami kuwa kwa sasa CCM imekosa dira kabisa na haijui what next. CCM imejikita katika siasa za maji taka chini ya utekerezaji wa Mwigulu pekee ambaye anazisimamia jukwaani bila hata aibu yoyote, anatekereza mipango michafu kwa amani ya taifa letu. Watanzania kimya!!!!. wanacheki kama CCM ndo hii!, basi!!!!. 2014-2015 tutaona mengi. we subiria pamoja nami.
 
Ccm is there to stay, mtakufa nyie ccm itaendelea kudunda miaka nenda rudi
 
Kumbe hasira yako ni mwigulu, acheni ugaidi wa kumwagia watu tindikali na kupanga kulisha watu sumu ndio itakuwa salama yenu
 
itabakia makumbusho kwa siasa za kwenye keyboard na kujipiga mabomu wenyewe?

Mkuu,
Wapo watu mpaka leo wanaona aibu tu kuhamia CDM. Chanzo cha aibu ni nafasi zao nyeti serikalini. wengi wao wameshachukua kadi CDM na wanasubiria 2014;2015 kabla ya uchaguzi. Baada ya hapo utaona kwa macho yako mwenyewe!!.
 
....Ushauri:CCM inauliwa na viongozi wake. Kupona kwake,lazima wachague moja kati ya biashara safi na siasa au biashara chafu bila siasa.

Karibu sana Mkuu,

Kwanza nakupongeza kwa kuingia JF na pia umekuja na hoja nzuri ya kusaidia wachache ambao wanapotea ....
Ushauri wako unatakiwa kuzingatiwa ili maendeleo ya hicho chama yawepo
 
wewe ni mgeni hapa jukwaani umekuja kwa pupa ili utumike. Kwa taarifa yako CCM ilikuwepo,ipo na itaendelea kuwepo. Cha msingi ni ww kuwashauri akina Lwakatare, Slaa, Ben sa8, Kilewo na genge lao lote la CHADEMA kuacha kuua watu kwa tindikali sumu na mabomu
 
Watu kama nyinyi ndiyo mnaichinja cdm kwa kuwakuza. Badala ya kuwaambia wakomae unakuja kujambajamba hapa JF. Ccm haifi leo wala kesho na cdm kuongoza hawawezi....

Mkuu kubali au ukatae, CCM ilizaliwa, ikakuwa, na sasa baada ya kuzeeka iko hoi na haina mvua mbili itakuwa tayari imeshaingia vitambu vya kumbukumbu. Kama hutaki tulia utaona nachokwambia very soon
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…