Ni ukweli usiopingika kuwa ccm iko mahututi na muda sio mrefu tutashuhudia anguko la ccm, sababu za anguko la ccm ni hizi
1.Uhuru waliopewa vijana hawa,Nape,Mwigulu,Shonza na Mtela hasa uhuru wa kusema chochote ndicho chanzo cha anguko lake,hawapimi kauli zao na hawajui siasa.Hii ni kutokana na kauli zao za kuropoka ambazo hata ukimwambia kichaa kuzungumza hawezi.Kauli kama hizi zina impact kubwa sana katika jamii,kwani wananchi wana reason na kujua ukweli uko wapi.
2.Kauli tata za viongozi wa chama na serikali.Hawa ni kutokana na kauli zao za kukejeli(wassira-kibanda ni nani),kuchochea mauaji(pinda-wapigeni tu maana tumechoka),na kauli hizi zinafocus kwa wananchi moja kwa moja.CCM mkumbuke kuwa mtaji wenu ni kwa wananchi kuwaletea maendeleo ya huduma za jamii,sasa mnapodharau,kutukana,kukejeli,kuua wananchi sijui mnategemea nini.
3.Matumizi makubwa ya nguvu ya dola.hapa tunaona waziri mkuu anabariki kuua raia kinyume na katiba ya nchi ibara ya 13 ibara ndogo ya 6(a),(b),(c) na (e),pia kinyume na utawala wa kisheria.Pinda akumbuke kuwa hakuna mtu anayependa kudharauliwa,kunyanyaswa,kudhalilishwa na kunyimwa haki yake.Hapa watu uvumilivu umefika mwisho.
4.Umaskini uliokithiri.Kila awamu imekuja na kila aina ya kaulimbiu ili kunadi sera,mfano MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA,leo hii iko wapi? Wananchi wanahoji maisha bora yapi,mbona hatujayaona? Huku mkitamba na kujisifu majukwaani kuwa mmeleta maendeleo,kujisifu sio kazi yenu bali ni kazi ya wananchi kuwasifia.Mfano nani anatakiwa kumsifia mwenzake kati ya muuzaji(serikali) na mteja(wananchi),bila shaka ni mteja.Halafu kujisifia wakati ni wajibu wenu ni upuuzi,dharau na kejeli.
5.Udhaifu wa jk na serikali yake.Hapa tunashuhudia madudu ya kila aina kama kwa watumishi wa serikali, rushwa,ufisadi,wizi,matumizi mabaya ya madaraka,huku rais akiwachekeachekea kwa kuwa ni maswahiba wake na pengine ndio walimfanya kuwa rais.Wananchi wanahoji rais hayaoni haya?
Rais akizumgumzia basi sio kukemea,kuonya au kukaripia bali ni kulalamika.Na kulalamika ni dalili za kushindwa.
Ushauri,ccm mkitaka kuzinduka Nape,Mwigulu,Mtela na shonza wapigeni chini na/ au wafute kauli zao zinaleta picha mbaya,kwani zinachochea vitendo viovu kwa jamii na kwenye chama.Pia viongozi kama wassira,pinda,Lukuvi wawajibike kwa kujiuzulu na/ au kufuta kauli zao na kuomba radhi kwa wananchi,bila haya kufanyika ccm haitopona kamwe.