Watanzania wakijitahidi kuona mchawi anafariki, nachelea kusema sifa ya mchawi ni lazima aishi miaka mingi "Kitu mpaka uzeeni kama hakijafanyiwa ya shinyanga na mbeya kwa sasa", Kila anayemtishia uhai wake ujue siku zake zinahesabika kwa namna yeyote ile, Siku anakata roho watu waweza subiri hata siku 3 bado tu anarusha miguu na kufumbua macho.
Hivyo ni vyema kujiandaa vizuri maana bado kuna kazi ngumu mbeleni kama tunavyoona sasa hivi kesi za ugaidi nje nje, kubambikwa kesi ni kawaida sana tu, Rumande ndio hotelini kwa wasema kweli, Ukisema ufisadi na ujangili unaonekana mtovu wa nidhamu kwani hizo ni biashara halali kwa viongozi wetu, Ukisema madawa ya kulevya utaambiwa walioshikwa ni wale mateja wa pale ruvu, Kudhibiti silaha na matumizi mabaya ni kama kuzuia machinga kuuza mapanga, visu na bastola za bandia Dar kwenye foleni.
Ni vizuri kumuuliza kamanda MREMA alikosa hadi kura aliyopiga yeye mwenyewe pamoja na kwenda mahakamani lakini haikupatikana, Pia ushindi siku hizi unatolewa hadi mahakamani kama chama fulani kitaona kura hazikutosha. Tatizo la mahakama zenyewe ndio hizo za kufuta kesi na baada ya dakika 3 unakamatwa tena na kuhamishwa kwa hakimu mwingine anayejua kuendesha kesi, Au kama za Ponda bado hajahukumiwa kama kiongozi wa uvamizi lakini wafuasi muda mwingi tu washaanza kukalia debe.