Kifo cha Bernard Membe: Ufafanuzi kuhusu Madai na Malipo ya Mdaiwa aliyefariki

Kichuchunge

JF-Expert Member
Dec 2, 2020
338
891

Anaandika Ibrahim Mkamba

Inna lillahi wa inna lillahi raj'ughn, Bernard Camillius Membe ametutoka. Taarifa ilipopatikana tu, mara moja maswali yamekuwa mengi endapo sasa mtu aliyemdai hatalipa kwa sababu madai yalikuwa yanahusu mdai kukashfiwa na huyo mkashfiwa ameshafariki.

Najibu hapa ili kupunguza kazi ya kumjibu mtu mmoja mmoja. Kisheria kesi ikishaamuliwa, maamuzi yake yanaingia kwenye utekelezaji endapo hakutakuwa na maombi ya rufani au revision ambayo hayakuwepo kwenye kesi ya Membe.

Kwa msingi huo, taratibu za kumlipa zitaendelea na pesa yote iliyoamuliwa na Mahakama alipwe atalipwa. Katika orodha ya mali zake itakayotengenezwa na msimamizi wa mirathi, pesa hiyo itaorodheshwa kwani ni yake kisheria.

Hali ingekuwa tofauti kama Membe angefariki kabla ya uamuzi huo kutolewa hata kama ingekuwa inasubiriwa hukumu tu. Kwa hiyo rafiki zangu mliodhani mdaiwa 'amesevu' pokeeni ukweli huo. Lazima atalipa tu.

Kibaya kwa upande wake sasa ni kwamba mtu ambaye angempa punguzo la malipo hayo katangulia. Ni wazi warithi watahitaji kulipwa pesa yote. Ndugu zangu, majibu yangu ni hayo.

Bernard Membe apumzike kwa amani. Amina.
 
Anaandika Ibrahim Mkamba​

INNA lillahi wa inna lillahi raj'ughn, Bernard Camillius Membe ametutoka. Taarifa ilipopatikana tu, mara moja maswali yamekuwa mengi endapo sasa mtu
aliyemdai hatalipa kwa sababu madai yalikuwa yanahusu mdai kukashfiwa na huyo mkashfiwa ameshafariki.
Najibu hapa ili kupunguza kazi ya kumjibu mtu mmoja mmoja. Kisheria kesi ikishaamuliwa, maamuzi yake yanaingia kwenye utekelezaji endapo hakutakuwa na maombi ya rufani au revision ambayo hayakuwepo kwenye kesi ya Membe.
Kwa msingi huo, taratibu za kumlipa zitaendelea na pesa yote iliyoamuliwa na Mahakama alipwe atalipwa. Katika orodha ya mali zake itakayotengenezwa na msimamizi wa mirathi, pesa hiyo itaorodheshwa kwani NI YAKE KISHERIA.
Hali ingekuwa tofauti kama Membe angefariki kabla ya uamuzi huo kutolewa hata kama ingekuwa inasubiriwa hukumu tu. Kwa hiyo rafiki zangu mliodhani mdaiwa 'amesevu' pokeeni ukweli huo. Lazima atalipa tu.
Kibaya kwa upande wake sasa ni kwamba mtu ambaye angempa punguzo la malipo hayo katangulia. Ni wazi warithi watahitaji kulipwa pesa yote. Ndugu zangu majibu yangu ni hayo.
Benard Membe apumzike kwa amani. Amina.
Umeliweka vizuri. Common law jurisdiction more or less like ours Iko hivyo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom