Heshima nyingi sana kwa wanajamvi wote wa JamiiForums.
Salaamu,
Tumemzika andrew aliyeuawa kikatili marekani je nini kinafuata? au itakuwa kama ilivyo kawaida yenu kuficha taarifa za mauaji kama mlivyofanya kwa watanzania wengine (waliochomwa visu, waliochomwa moto, n.k n.k)?
Wakuu Nimekuja kwenu kwa heshima na taadhima kuwaomba watanzania wote wanaoishi houston kutoa taarifa zozote muhimu wanazozijua juu ya mauaji ya mtanzania mwenzetu, kijana mwenzetu, mzazi mwenzetu na zaidi ya yote mhanga wa maisha ya ughaibuni.
Hata kama unaogopa kufanya hivyo fanya kwa ajili ya Mungu, kwa ajili ya nchi yako Tanzania, na yule mwanaye ambaye amempoteza mtu muhimu katika maisha yake.
Kwanini nimeileta JamiiForums?
1. Aliyepigwa risasi ni mtanzania hivyo basi ni jambo jema kuwa mzalendo na kutoa taarifa zitakazopelekea kupatikana kwa haki.
2. Watanzania wengi wameuawa vifo vya kikatili kama hivi huko Marekani ila watanzania hata wale ambao wana taarifa za wahusika waliamua kukaa kimya kuwalinda wauaji. Kumbuka leo ni Andrew kesho inaweza kuwa wewe. Tena bora ya Andrew amepata wa kumsafirisha akazikwa kwao, wewe unaweza usipate hata wa kulipia jeneza lako lije Tanzania uombolezwe na nduguzo. Hivyo basi kupatikana kwa wauaji ni njia moja wapo ya kutuma salamu kwa wengine wenye nia ya kujeruhi au kuua kwamba hakuna atakayewafichia siri.
3. Kulingana na taarifa ya Alex wa Swahili tv ni kwamba Andrew alipigwa risasi eneo ambalo palikuwa na watu meaning kwamba hakuwa peke yake. Anaendelea kusema kwamba watanzania waliokuwepo eneo la tukio walimuona muuaji na wanamjua iweje leo waamue kukaa kimya? Na yule jamaa aliyemuokota na kumpatia pumzi kama first aid baada ya kushutiwa na kuanguka chini na yeye ameamua kukaa kimya? Kama mnampenda Andrew kama mlivyojiliza na kama alivyokuwa anawanunulia bia na kuklia bili zenu basi ninawaomba mumtetee leo kwa kutoa taarifa zitakazopeleka kupatikana kwa muuaji kwa kuwa hawezi kujitetea yeye binafsi.
4. Taifa limepoteza nguvukazi ya taifa (hata kama alikuwa hafanyi kazi Tanzania bado alikuwa anatuma remittances ambazo zilichangia kukua kwa uchumi wetu) hivyo basi ninawaomba moderator muuache huu uzi hapa ili kwamba mwenye taarifa yoyote kuhusu hili tukio aiweke hapa na mwisho wasamaria wema waweze kuzipeleka kwa vyombo vya dola vya marekani.
5. Ubalozi wa Tanzania Marekani uweze kuona na kuchukua hatua haraka. Balozi zetu zimekuwa zikikaa kimya mauaji kama haya yanapotokea tumechokaaaaaa na ukimya wenu. Mmnatumia kodi za nchi kwa kazi mnazoitiwa huko ubalozini sasa kwanini mnashindwa kuwatetea watanzania ughaibuni? Kwanini mnashindwa kusimama kama wakala wa Tanzania Marekani mhakikishe raia wenu wanapata haki zao?
Tutazika ndugu zetu kwa vifo vya kinyama kama hivi hadi lini bila haki na sheria kuchukua mkondo wake? Ubalozi kazi zake sio tu kuandaa maonesho ya utalii bali kusimama bega kwa bega kwenye masuala kama haya.
Mwisho kabisa ninawaomba kutoka moyoni mwangu jitoeni mpeleke taarifa ili haki itendeke kwa ajili ya mtanzania mwenzetu. Juzi ile alikuwa mazula, juzi kati jamaa aliyechomwa kisu na mtanzania mwenzake, leo ni andrew kesho nani ajuaye yaweza kuwa wewe au ndugu yako.
Usipochukua hatua usifikiri kwamba hata wewe utakuwa salama.
#justiceforandrew
====================
UPDATE KESI YA RAFIKI YETU MAREHEMU ANDREW NICKY SANGA
Tunapenda kuwashukuru ndugu , jamaa , marafiki na Wanajumuiya wote kwa ujumla kwa kuwa pamoja nasi katika kipindi chote hiki cha kufuatilia kesi ya mauaji ya kinyama ya mpendwa wetu Andrew Nicky Sanga ( Baba Zoe ).
Tunapenda kuwafahamisha kuwa kesi imeisha rasmi leo ( 02/18/2019) saa 4 asubuhi kwa mtuhumiwa Villere Henderson Johnson kukiri makosa na kuhukumiwa kifungo cha miaka 35 jela bila parole.
Tunamshukuru Mungu kwa sala zenu.
Ahsanteni sana,
Emmy Matafu na Zoe Sanga