Kifo cha Al Baghdad - De javu

Salim A. Msangi

JF-Expert Member
Apr 26, 2011
566
511
Alianza Bush, alipohitaji kura za wananchi wake, aliwajia na hadithi za Saddam kuhusika na 9/11, akaunda zengwe la maana na mwishowe akaivamia Iraq ilia pate pa kuponea, kilichofuatia ni historia.

















Rais George W. Bush akilianzisha

Staili hii akaja nayo kijana mtanashati, Obama, alipo hitaji kura na hisani ya wananchi wake kuendela kwenye kiti kile akiwa na ushaiwshi uleule, faili la Osama lilitafutwa na ‘alipatikana’ Pakistani, kilichofuatia ni historia.

















Rais Barrack Obama naye akapokea kijiti

Kama watu hawajui kuonganisha doti vile, au memory zao ni ndogo sana, ‘kuchambua’ mambo … Trump naye akaona isiwe ishu muda umekaribia, katafuta faili la Albaghadad hilo hapa … tunategemea kifuatacho ‘ITV’, ni kama hadithi za Busha na Obama.


















Trump naye kaamua kuinvest kwenye hii franchise ya kufufua wafu ili ushinde uchaguzi


Anyway, wale wenye akili zetu ambazo bado zipo ‘intact’, tunajua hizi ni zile zile tamthilia pendwa toka Hollywood, na director ni CIA.Tumuache Saddam kwa sasa, tuwatizame Osama na Albaghadad kwa ufupi sana ili tuchoshane.

Wakati Obama anatangaza kifo cha Osama, kile ambacho watu wengi hawakijui ni kwamba, Osama alikuwa ameshatangazwa kufa zaidi ya mara 9, hapo nyuma. Alitangazwa na serikali kadhaa, taasisi, watu wenye vyeo vizito kwenye majeshi au kwenye serikali na pia na vyombo vikubwa vya habari duniani.

Osama alikuwa ameuwawa au kufa kifo cha kawaida tangu mwaka 2001, wakati Obama anatangaza kifo chake mwaka 2013, Obama alikuwa ni mtu wa 9, kwenye orodha ya watu walio kuwa wakitangaza kifo cha Osama tangu mwaka 2001.

Kama kilivyo kuwa kifo cha mtu aliyeitwa, ‘Alzarqawi’, ambaye naye alitajwa kama kiongozi wa Alqaedah Iraq na baadae muanzilishi wa makundi ya kigaidi yaliyo pelekea kuundwa kwa IS na ISIS, Osama naye mwili wake haukupatikana, tulicho ambaiwa ni kuwa ‘DNA Match the Guy, its him.’ End of story.

Story hii ya Osama na namana movie nzima ilivyo tengenezwa, icheki hapa

https://salimmsangi.blogspot.com/2013/07/obama-alazimika-kumfufua-osama-bin-laden.html#more

Wakati Trump akiendelea na uwongo uleule wa watangulizi wake, akaongezea uwongo mwingine, akasema Albaghadad ndiyo muanzilishi wa makundi ya IS na ISIS na mengine yaliyo kuwa yanabeba ile brand kubwa ya Alqaedah.

Lakini tunajua aliye anzisha makundi haya ni ‘Alzarqawi’, ambaye naye kama alivyo kuwa bin Laden, na hatimaye Albaghdad, alisha kufa mara kadhaa, alishakamatwa mara kadhaa, lakini kila wakati aliachiwa kimiujiza na kila wakati alifufuka na kuendeleza mapigano dhidi ya Marekani.
ISIS imepitia mabadiliko kadhaa kama ifuatavyo.
  1. Jama'at al Tawhid w'al Jihad (JTJ)​
  2. Al Qaeda in Iraq (AQI)​
  3. The Islamic State in Iraq (ISI)​
  4. The Islamic State in Iraq and Sham (ISIS)​
  5. The Islamic State (IS)​
Kutoka JTJ mpaka ISIS ni kazi ya Alrazqawi, ambaye alitokea kwenye majivu ya Afighanstan, na kati ya sehemu zote alichagua kukimbilia Iraq, ambapo ndipo Washington, wakaja na ishu ya Saddam kuhifadhi magaidi. Alzarqawi kama walivyo kuwa watangulizi wake na walio fuata na watakao fuata, wote wafuata maelekezo toka Washngton.

Trump kumuhusisha Albaghdad na uasisi wa makundi hayo ya kigaidi, ambayo tunajua yametengenezwa kutoka Washngton tangu kipindi cha utawala wa Regan mpaka Obama, na sasa Trump naye anaogelea kwenye bahari ileile, ni kwamba Trump anataka kujenga jina, aoanekanae amefanya ‘bonge la misheni’, ‘bonge la ishu’ bonge la muvi kupita hata la Alrazqawi na Osama.

alra1.jpg

Lakini sababu, mtengenezaji wa muvi hizi ni director yule yule, jambazi kuu ni walewale, na sterling ndiye imefanyiwa ufranchise, mara Bush, mara Obama na sasa Trump, si dhani kama muvi hizo zitakuwa na jipya, labda mtazamaji akiwa na akili za kushikiwa.

Lakini wale walio tajwa kuwa ni washirika wakubwa kwenye operesheni hii, na kwamba walitoa ushirikiano wa kutosha wa kuuwawa kwa jambazi kuu, ‘Al Baghdad’, nao si wengine bali Moscow, wao wamekana kata kata kutambua kuwepo kwa kisheni hiyo, achilia mbali kutoa ushirikiano.

1.jpg

Kuhusu Al Baghadad, nani asiyejua kuwa alitengenzwa kipindi cha Obama, kwa nguvu kubwa ya Hilaary na McCaine?
Ushahidi wa kutosha, kutoka kwenye vyanzo visiyo na shaka, hata kwenye vinywa vyao wenyewe akiwemo Hillary Clinton, kwamba wao ndiyo wamewatengeneza hawa magaidi. Ushahdi wa kutosha upo unao muonganisha Albaghdad na McCaine.

Walipewa silaha za kutosha, fedha, vifaru n.k kutoka Washington, na utawala wa Obama ulikuja na ‘statement’ za kuchanganya ilipokuwa ikisema serikali yake itahakikisha inavisaidia vikundi, ‘vya kigaidi’ ili kumuondoa gaidi, ‘Albashar’ madarakani, ilikuwa wazi kabisa, na mana incharge alikuwa si mwingine bali, Al Baghdad.

al0.jpg

Hapa Al Baghdad ni ‘’Most Wanted Man’’
Al Baghdad ambaye kama walivyo watangulizi wake, alisha kamatwa, mara kadhaa, aliachiwaje, hatujui, alishakufa mara kadhaa, alifufukaje mpaka leo Trump akamuuwe tena hatujui.

al 2.jpg

John Mccaine akituambia mkakati wake wa kuwaunga mkono akina Al Baghdad

Sasa utaona ni muvi zile zile, nah ii ni kwamba Washington, inawaona watu ni wajinga sana, hasa wanachi wake, na ulimwengu kwa ujumla, kwamba kila wakati njoo sema chochote na ‘makondoo’ yataamini na kufuata, mradi anayesema ni Public Officer, toka kwenye chombo cha Serikali. Hii lazima ni kweli. Usisahau tayari IS wameshachagua kiongozi wa kushika nafasi ya ‘Al Baghdad’ kwa hiyo series bado linaendelea.

al3.jpg
Mccaine yupo uso kwa uso na mtu waliyemtangaza kuwa ni ‘’most wanted’’, na zawadi ya $ mil 10, akipatikana hai au kafa. Labda Mccaine hakuwa na njaa hizo ndiyo maana akapiga naye story na kumpa mkwanja Zaidi Ili aendelee kuua na kulipua watu.

Hapa ndipo ninapo jiuliza, mar azote hizo ambazo Osama alikuwa anatangazwa kufa, hujawahi wasikia Al Qaedah, wakisema tunamchagua muwakilishi mpya wa Osama, wala wakati CIA, wanato kanda feki za video na audio za Osama huwasikii wakisema hiyo ni feki Osama hayuko hivyo, lakini ikija move kubwa toka Washington, tena iliyo kinyume na wao, uatawaona na wao wanacheza na kuimba muziki huo huo.

al4.jpg

McCaine yupo na viongozi wa Free Syrian Army na Jabhat al Nusra, Al Baghdad (aliyezungushiwa duara)
Hapa tena, IS wamesha mtangaza, mrithi wa Al Baghdad, kitu ambacho ndicho Washington wanacho kitaka, sasa unajiuliza, Who is Washington na Who is Terrorist? Kama ni mtu yule yule anaye tucheza shere, hapana anaye wacheza shere wale wenye akili ndogo.

Endelea kushangilia kifo hewa cha Al Baghdad, muda si muda utaletewa episode nyingine kutoka Washington, Director CIA, stelingi sijui atakuwa nani, ila jambazi kuu limeshachaguliwa.

Till next Time. Tchao!
 

Attachments

  • al 1.jpg
    al 1.jpg
    24.6 KB · Views: 5
  • al 1.jpg
    al 1.jpg
    24.6 KB · Views: 4
... mbona ni simple tu; kama hajafa, huyo al-Baghdadi atokee kwenye TV japo kwa sekunde moja aseme tu "hi". Otherwise, unaota ndoto za mchana; al-Baghdadi is dead an will never be seen again forever and ever!
Sizungumzii kwamba yupo hai au amekufa, hiyo siyo ishu hapa, nadhani hjaelewa uzi mzima. Kwanza kama alivyo kuwa Osama, alzarqawi, na pia kulikuwa na Albaghadad mwingine kabla ya huyu, wote walikuwa wanakufa na kufufuka, kwenye haijalishi kafa ua yupo hai, ninacho zungumzia hapa ni namna watu wenye akili ndogo wanavyo aminishwa kuwa kuna 'gaidi' mahali na ili tuweze kumdhibiti, tupe haki zako za privacy, toa sheria hii weka ile n,k wakati mwisho wa siku waathirika ni mimi na wewe, sababu hapakuwa na kitisho cha gaidi, bali kimetengenezwa ili kutuporoka haki zote. Mwisho wa siku gaidi ni wewe na mimi, sababu ndiyo wahanga wa sheria hizo.
 
"Take any words from US politicians with a grain of salt", Syria’s Bashar Assad

good work, keep it up.
 
Sizungumzii kwamba yupo hai au amekufa, hiyo siyo ishu hapa, nadhani hjaelewa uzi mzima. Kwanza kama alivyo kuwa Osama, alzarqawi, na pia kulikuwa na Albaghadad mwingine kabla ya huyu, wote walikuwa wanakufa na kufufuka, kwenye haijalishi kafa ua yupo hai, ninacho zungumzia hapa ni namna watu wenye akili ndogo wanavyo aminishwa kuwa kuna 'gaidi' mahali na ili tuweze kumdhibiti, tupe haki zako za privacy, toa sheria hii weka ile n,k wakati mwisho wa siku waathirika ni mimi na wewe, sababu hapakuwa na kitisho cha gaidi, bali kimetengenezwa ili kutuporoka haki zote. Mwisho wa siku gaidi ni wewe na mimi, sababu ndiyo wahanga wa sheria hizo.

Acha propaganda hewa mkuu
 
Kwenye ulimwengu huu tulionao ni vema ukakaa kimya kuliko kufanywa ukae kimya. Mtoa mada naona kwa mbaaali kama umeanza kunawa tongotongo.
 
Kwenye ulimwengu huu tulionao ni vema ukakaa kimya kuliko kufanywa ukae kimya. Mtoa mada naona kwa mbaaali kama umeanza kunawa tongotongo.
“Those who are able to see beyond the shadows and lies of their culture will never be understood, let alone believed, by the masses.”

― Plato
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom